Rweye
JF-Expert Member
- Mar 16, 2011
- 17,052
- 7,609
Naelewa nchi yetu imejikita katika hii kauli mbiu ya viwanda. Halikuonekana wazi katika hawamu ya nne lakini sasa linaanza kutia shaka, hivi kujenga viwanda vyote eneo la ukanda wa pwani wa nchi yetu huku maeneo mengine ya nchi yakionekana kuachwa ni sahihi kweli? Na je hiki ni kitu gani hasa kinafanyika.
Inatia ugumu kuelewa adhima hii ni nini pale mfano unaposikia eti mkoa mmoja tu 'mkoa wa Pwani' mfano una viwanda zaidi ya 30 huku kukiwa na mikoa isiyokuwa na hata viwanda 5. Hii maana yake ni nini? Mkoa kama Tabora mfano hauna hata kiwanda1 na haionekani kama kuna hata wa kufikiri katika hili, ni kwanini mikoa mingine ifanywe kama vile si sehemu ya Tz.
Kutoka kanda ya magh, kusini mpaka kati ya Tz unaweza ukakuta viwanda vilivyo katika kanda hizo tatu ama ni vichache kuliko vilivyoko mkoa mmoja wa pwani kwa sasa hivi. Huu si ukanda mwingine huu? Wakati mwingine unajiuliza kama lengo la kwanza kuwa na viwanda ni kutoa ajira, utawezaje kupunguza hili tatizo kama viwanda vipya vyote vinaelekezwa mikoa ya pwani, Tanga, Pwani, Dar, Mtwara?
Ama ndo tunafanya zile zile sera za kikoloni, kupeleka vitu muhimu kwa maeneo fulani tu kwa sababu zao maalumu. Ama tunamaanisha watu wote wahame toka kanda zingine na mikoa mingine wazifate ajira pwani tu? Ni kwanini nchi hii kwa sasa hivi kila kitu kinaelekezwa huko tu? Utasikia magari, pikipiki, baiskeli, matrekta, vigae, mabati n.k kila kiwanda kinasemwa pwani tu. Is this fair kwa maeneo mengine ya nchi?
Najua wenye akili finyu wataona nimeleta kitu cha hovyo kwasababu sasa hivi wanataka za Makonda tu, lakini wengine tunajua ili nchi yetu iendelee Makonda si chochote sana, kesho Makonda hatokuwepo lakini Tz yetu itakuwepo na itabidi izidi kuwepo na isonge mbele.