Vivutio vya kitalii ambavyo havitambuliki

Willy T

JF-Expert Member
Mar 21, 2016
253
91
Jamani habari ya muda huu natumahi mpo poa

Ebu tujaribu kupata angalau picha mbili tatu za maeneo ya Tanzania na maelezo kidogo ili tupate ufahamu
Wa pesa zinazopotea maana naijua Tanzania sana kwa kutozingatia

Tuache hizo national parks na game reserve zinazojulikana na mpya pia
Mfano:
Mt. Kilimanjaro
Mt.meru.
Serengeti national park
Mikumi national park.
Ngorongoro national park
Selous game reserve
Lake manyara

Naomba kujua mengine
 
120c77a2ba65815001573594496dc181.jpg

Lake ngozi
 
The lake is very very beautful n kusingekuwa na maji humo basi view yake ingefanana na ngorongoro
 
Kuna shimo la Mungu huko Mtwara. Liko porini na wala hakuna kijiji cha karibu lakini ukithubutu kupita utasikia watu wanaongea na kuku (jogoo) wanawika. Kuna legend inasema kuwa kuna watu walikwenda kuchunguza kuna nini huko na hawajarudi tena mpaka leo hii.
 
Shimo la Mungu lipo newala mjini, wenyeji wote wanaliheshimu, cha kushangaza hakuna anayetamka maajabu ya humo ndani!
 
Shimo la Mungu lipo newala mjini, wenyeji wote wanaliheshimu, cha kushangaza hakuna anayetamka maajabu ya humo ndani!

Newala (Mtwara)....imesemwa penye miti mingi hakuna wajenzi. Siku tukifa njaa na kwenda kwa Mungu kuhukumiwa huku Mungu akituuliza sie watanzania tumekufa na nini na tukisema njaa, Mungu atatulaani kwa kweli ama kutuzaba tu vibao. Utajiri wote tuluionao yaani bado tunashindwa kuutumia ipasavyo. Nchi za wenzetu wangetangaza vilivyo utalii wa ndani na kuliingizia taifa pato la ndani, ila sie bado tunasikiliza bongo fleva na kuangalia mitandaoni staa gani kalala na nani jana.
 
Back
Top Bottom