Vivuko vya waenda kwa miguu kwenye hii barabara ya Moroco-Mwenge

keyonce

Member
Jul 29, 2015
14
22
Barabara ya Morocco - Mwenge imekuwa pana sana kiasi kwamba inakuwa ngumu sana kwa wale wanaotembea kwa miguu kuvuka barabara kutoka upande mmoja kwenda mwingine ukizingatia ni ngumu sana kwa magari kusimama kwenye zebra na kuruhusu waenda kwa miguu kupita.

Maoni serikali iliangalie hili na kufikiria kuweka daraja la juu (Foot Over Bridge) kwani barabara ni pana mno kuvuka na haina hata median (garden ya katikati) hii inahatarisha usalama wa waenda kwa miguu.
 
Zinahitajika flyover lakini sio feasible kwa sasa, population ya wavukaji ni ndogo mno ukilinganisha na let's say Buguruni sheli
 
Daraja la kuvuka moja litasaidia nn?
sio daraja moja, atleast pale kwenye wavukaji wengi wanaweka kama section ya bamaga mpaka mwenge waweke moja, alafu makumbusho waweke moja na Victoria waweke moja. jumla matatu
 
Zinahitajika flyover lakini sio feasible kwa sasa, population ya wavukaji ni ndogo mno ukilinganisha na let's say Buguruni sheli
kwakuwa wavukaji ni wadogo unaona ni sawa tu usalama wao ukiwa hatarini? na kwa sasa majengo mengi ya ofisi yanajengwa so kwa mbeleni watakuwa wengi hivyo nimuhimu yakawekwa sasa... maana ni hatari sana kuivuka ile barabara
 
tunavuka hivyohivyo, mtu akigongwa siku yake imefika, tulikuwa tunavuka hivyohivyo kimagumashi tangu yalipokuwa yanapishana magari njia moja kwenda moja kurudi, labda kama mtu katokea nchi nyingine lakini kama ni dsm haitomsumbua
 
bora hapa hapa niwasema madereva jamani wanakimbiza magari hawataki kusimama hata kupunguza mwendo mpaka najiuliza hivi haya magari ya hii njia ni matreni au ? mnakimbiza magari mnoooo
 
Bara bara ya makumbusho naiogopa haswaaaaa. Yan nawazaga tu navukaje siku zote sasa ndio imekua pana hivyo naona watanitembeza had makumbusho kituon nikageuze na gari. Mm kufa sa hiz bado cjajiandaa aisee. Halafu wanahis wote tuna magari. Hawajatufikiria sis wakwea daladala tunaishije. Basi watenganishe barabara kati kati lasivyo tutakatishana maisha hapa halafu tuanze kukemea pepo la mauti kumbe ni uzembe( poor planning) ya barabara. Wahusika mtuhurumie watembea kwa ngondi loo
 
mnayosema ni kweli,,,muhimu wachore sehem zote za wavuka miguu na waweke matuta kabla ya hizo zebra,,ziwe bold na kuonekana ili mtu agongewe hapo dereva afungwe kifungo cha maisha,,maana ni kuua kwa kukusudia,,hakuna mtu asiejua zebra ni nini hata mdogo....pili,,,dar madereva hawana subra ndo maana magari mengi yana pass na kuchubuliwa sana,,,wana haraka huwezi jua hata wanakikimbilia,,hata fea za wao kwa wao hawapeani ,,utaona mtu kanuna kumbe kuna mwenzie alitaka kuingia au kuvuka upande mwingine
 
na hata wao wenye magari vile vile wanahatari ya head to head collision wangeweka hata boundary ya kutenganisha basi hata kwa toe wall hapo kati maana ya wanaoenda upande mwingine hawawezi ingiliana na upande mwingine.
ile bara bara ni hatari sana kwa sasa kwa wavuka miguu na wenye magari vile vile. hivii watu wa road safety wako wapi? hawayaoni haya? au kazi yao ni nini?
 
Back
Top Bottom