Viungo Vinavyosafisha Mwili

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
40,292
Points
2,000

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
40,292 2,000
Viungo Vinavyosafisha Mwili (kiingereza Excretory Organs) ni viungo katika mwili wa binadamu ambavyo vinahusika katika utoaji wa taka mwilini. Binadamu kama viumbe haiwengine wanahitaji kutoa uchafu. Hakuna mfumo maalumu katika mwili wa

binadamu
ambao unahusika moja kwa moja katika utoaji wa uchafu kama vile kwa mfano mfumo wa upumuaji ambao unahusika moja kwa moja na upumuaji. Viungo mbalimbali kutoka katika mifumo mengine kwa pamoja huweza kufanikisha suala la

kusafisha mwili. Mfano viungo kama mapafu, mafigo na ngozi ambavyo vipo katika mifumo mengine hutumika katika mpangilio uliotajwa kutoa hewa chafu, mikojo na jasho. Viungo hufanya kazi zingine pia zaidi ya utoaji taka, kwa mfano ngozi pia

huhusiaka katika kutunza joto la mwili na kadhalika. Viungo hivi kwa pamoja hata kwa kuwa sehemu mbalimbali katika mwili wa binadamu kwa pamoja huwekwa katika mfumo wa utoaji taka.Mapafu na moyo,

Utangulizi

Wanadamu hula chakula na kunywa maji kwa sababu miili yao hupaswa kulishwa ili isidhoofike wala kuwa na afya mbaya. Lakini katika chakula na maji zimo sehemu nyingine za vitu hivi zisizotufaa, na hizi sehemu lazima zitengwe na kutolewa nje ya miili. Kama sehemu hizo hazitolewi tutapatwa na magonjwa na hatimaye tutukufa. Viungo vyenye kazi ya kusafisha mwili ni mapafu, mafigo na ngozi.

Mapafu

Kila kiumbe hai kinahitaji hewa ya oksijeni ili kiweze kuishi. Kila kiumbe kina namna ya kujipatia hewa hii muhimu kwa uhai. Kwa mfano samaki huipata kutoka majini kwa kutumiamatamvua, mimea hutumia majani wakati wa usiku. Halikadhalika wanyama jamii ya mamalia hujipatia hewa kwa kutumia mapafu. Binadamu ana mapafu mawili yaliyo ndani ya kifua. Kwa maelezo zaidi kuhusu mapafu angalia mapafu.
Binadamu hutumia hewa ya oksijeni katika kujitengenezea nishati kutoka katika chakula kwa ajili ya matumizi mbalimbali mwilini. Miongoni ya matokeo ya pambano la chakula na oksijeni pamoja na vimeng’enyo mbalimbali ndani ya seli ya binadamu, pamoja na vitu vingine ni hewa ya carbondioxide. Hewa hii husafirishwa katika damu mpaka ndani ya mapafu ambao huitoa nje kama uchafu ndani ya mwili. Kiwango cha hewa ya carbondioxide kinachotolewa nje kila mtu anapopumua kinaweza kufikia asilimia nne au zaidi ya hewa yote inayotolewa nje. Zaidi ya hayo mapafu hutoa maji mengi kwa namna ya mvuke.

Ini

Ini ni miongoni mwa ogani muhimu katika mwili wa binadamu. Pia ini ni mojawapo ya viungo vinavyohusika katika kutoa uchafu. Ini hutumika pia katika uhifadhi wa chakula katika mwili wa binadamu. Chakula kinapofonjwa kuingia mwilini katika utumbo mwembamba huelekea kwanza katika ini. Ini husafisha sumu katika mwili. Kunapokuwa na uongezeko la chakula cha protini, ni jukumu la ini kurekebisha. Uchafu unaotolewa na ini huingizwa katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula na hutolewa pamoja na kinyesi.


Mfumo wa mkojo


MafigoKatika mwili wa binadamu mafigo yamewekwa nyuma ya tumbo; moja kwa kila upande wa pingili za juu za kiuno. Sehemu ya juu ya mafigo imehifadhiwa kwa jozi mbili za mbavu zinazoelea. Kila figo kwa umbo lake hufanana na haragwe, lakini kwa ukubwa ni tofauti

sana. Figo la kulia kwa kawaida ni fupi na nene zaidi, nalo, kwa sababu ya ini, hukaa chini zaidi kuliko figo la kushoto.
Mafigo yametengenezwa yawe mfano wa chombo cha kuchujia maji. Kazi yake ni kuchuja maji na kutoa uchafu na vitu vyote

visivyohitajika mwilini vilivyochukuliwa na damu katika safari zake. Maji hayo pamoja na vitu hafifu vilivyomo ndiyo mkojo. Mafigo yameshehenezwa na vifereji vilivyonyongwanyongwa, navyo vyote huunganika pamoja kufanya bomba lile litokalo katika kila figo na kufika mpaka katika kibofu cha mkojo. Kutoka hukoo mkojo hutolewa nje kwa mshipa wa kupitia mkojo na uume/uke.

Kibofu cha Mkojo

Kibofu ni mfuko wa mkojo uliopo mvunguni mwa matumbo. Kwa hiyo mkojo hauwezi kutoka mojamoja mara tu unapotengenezwa na mafigo. Kibofu kinapojaa mkojo, mtu huhisi haja ndogo. Kiasi cha mkojo unaotolewa kila siku hubadilika siku hadi siku. Hii hutegemea

na hali mbalimbai. Mtu mwenye afya njema hutoa lita moja na nusu hadi lita mbili na nusu za mkojo katika muda wa masaa 24. Kiasi cha mkojo, huongezeka kama mtu amekunywa sana vinywaji, kwa mfano, pombe, divai, maji ya machungwa au mananasi, au kama

amepatwa na magonjwa ya figo. Hapa mkojo huwa si wa manjano sana. Kiasi cha mkojo unaotolewa kila siku hupungua kama mtu

hakunywa sana kinywaji cho chote au kama ametokwa na jashosana. Hali hiyo hutokea pia mtu ashikwapo na homa. Hapo mkojo huwa na rangi ya kimanjano sana, pengine ni wa hudhurungi, na pengine hatakikahawia.

Ngozi

Sehemu ya nje ya mamalia imefunikwa na ngozi. Kutegemeana na mamalia kiwango cha nywele kinachoweza kutoa juu ya ngozi kinategemea asili au mahali ambapo mamalia anapatikana. Ngozi ya binadamu inaweza kuwanywa katika sehemu mbili; nazo ni ngozi ya ndani na ngozi ya nje.

Ngozi ya Nje


Ngozi ya nje ni matabaka mengi ya magamba. Ngozi inaposuguliwa magamba haya hutoka. Hayo yanaonekana katika ngozi ya kichwa. Matabaka ya chini hayana magamba mengi nayo huwa na rangi maalum ionekanayo katika mataifa makuu ya jamii ya wanadamu. Ngozi ya nje hulinda sehemu za mwili zilizo chini yake na ambazo zina kapilari. Kwa hiyo mtu asiye na ngozi iliyochubuka anaweza kugusa na kutumia vitu vya maji maji vilivyo na sumu naye asidhurike navyo

Ngozi ya ndani

Ngozi ya ndani au ngozi halisi iko chini au baada ya ngozi ya nje. Ndani ya ngozi ya ndani vimo vinyweleo vya jasho vingi visivyoweza kuhesabika. Karibu na vinyweleo hivyo zipo kapilari. Kila kinyweleo kimefanana na kifereji kilichonyongwanyongwa, na katika kuta zake

vimo vifuko vidogo sana kama vile vilivyomo katika
mafigo. Vifuko hivyo vinaweza kuondoa uchafu uliomo katika damu na kuupitisha katika vinyweleo mpaka kuutoa nje ya ngozi. Kwa kawaida jasho huwa halionekani kwa sababu linatoka kwa namna ya mvuke na

hutolewa katika hewa. Hapo huitwa
jasho lisiloonekana, lakini tukifanya kazi ngumu au kutikiwa na jotosana, basi hapo huwa tunatoa jasho linaloonekana wazi wazi.
Zaidi ya vinyweleo viko pia vitundu vidogo vingi sana vya malaika, na kila kutundu kina laika yake. Katika vitundu hivyo yamo mafuta, na kazi yake ni kulainisha ngozi isiwe ngumu wala isipasuke kwa baridi.


Kazi ya ngozi


Kimsingi ngozi ina kazi mbalimbali. Kwa ufupisho baadhi yake ni kama ilivyofupishwa hapa chini

  • Kutupatia mlango wa maarifa yaani kugusa.
  • Kusafisha mwili kwa kutoa nje ya mwili vitu vyote vichafu na visivyohitajika.
  • Kusawazisha joto la mwili.
  • Kulinda kapilari na sehemu zingine zilizomo ndani ya mwili.

Hitimisho


Utoaji uchafu katika mwili ni moja kati ya sifa ya msingi ya
kiumbe hai. Inapasa mwili wa kiumbe hai uwe katika uwiano sawa ili uweze kufanya kazi kwa afya bora na kuongezamuda wa kuishi. Sumu na uchafu ndani ya mwili husababisha kutofanya kazi vizuri na hivyo

kusababisha baadhi ya sehemu mbalimbali za mwili kufa mapema. Afya bora hasa katika ulaji wa
mlo kamili vinasaidia kwa kiwango kikubwa katika uboreshaji wa viungo hivi muhimu katika kusafisha mwili mzima wa binadamu kwa ndani.

Dhamana ya kusafisha mwili kwa nje kama vile kuuosha kwa maji na kuondoa uchafu unaoachwa nje ya mwili (mfano jasho) na viungo vya ndani, imeachwa kwa kiumbe chote kwa ujumla. Hivyo umetupasa kutunza miili yetu kwa kuiosha kila wakati inapochafuka.
 

Forum statistics

Threads 1,390,150
Members 528,096
Posts 34,044,022
Top