Vitumbuwa Vya Mchele | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vitumbuwa Vya Mchele

Discussion in 'JF Chef' started by X-PASTER, Aug 6, 2011.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Aug 6, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,650
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Vitumbuwa Vya Mchele

  [​IMG][​IMG]

  Mahitaji
  Mchele …......…………2cups
  Tuwi zito ….....….……1cup
  Ute wa yai ...…..….…1
  Unga wa Sembe ...…1tbsp
  Unga wa Ngano ...…1tsp
  Hamira..........………..1tsp
  Hiliki ……......……....…1tsp
  Sukari …….......………½ Cup


  Jinsi Ya Kupika
  Saga mchele na tuwi kwenye blender mpaka uwe laini uhakikishe hauna chenga hata kidogo tia yai, hamira na hiliki endelea kusaga tia sukari endelea kusaga na mwisho utatia unga wa ngano na wa sembe saga tena kidogo towa weka kwenye bakuli wacha uumuke.

  Ukisha umuka teleka chuma cha vitumbuwa na uwanze kuchoma kwa mafuta pole pole, mpaka uone vimebadirika rangi.
   
 2. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,432
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  dakika ngapi kuumuka mkuu?
   
 3. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #3
  Aug 19, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,650
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Dakika 15 - 25 mkuu, na hata hivyo utaona tu unga ukija juu.
   
 4. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #4
  Aug 19, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,215
  Likes Received: 1,623
  Trophy Points: 280
  salaaale,nnavyopenda vitumbua,kila siku najiuliza ntapata wapi unga wa mchele! kesho naenda kusaka chuma cha kuchomea! sasa baba, kwanini yai tunatia ute tu? mchele hauhitaji kulowekwa b4 blending?
  <br />
  <br />
   
 5. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #5
  Aug 19, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,650
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Mchele unaitajika kulowekwa mpaka uone umebadirika rangi na kuwa mweupe, almost 6hrs.

  Kutia ute wa yai kunasaidia pia kwenye kuumuka na kushikana kwa unga.
   
 6. Prince Nadheem

  Prince Nadheem JF-Expert Member

  #6
  Sep 6, 2012
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 982
  Likes Received: 140
  Trophy Points: 60
  Thanks for this educative thread x-paster
   
Loading...