VITUKO VYA WHAT'S APP..........

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,315
33,111
Huku Whatsapp kuna vituko watu na status zao:

1. Mtu ameandika Sleeping, sasa leo siku ya tano, si kishakufa huyu
2. Mwingine kaandika Driving toka mwaka
jana Agosti, naona atakuwa anakaribia
Afghanistan saa hizi
3. Haya jamaa najua kalazwa anaumwa
lakini kaandika Happy we vipi ndugu
yangu?
4. Huyu mdada kaandika Available?. Sijui anajua maana yake? Tukikuibukia utaanza mitusi
5. Mbosi huyu hajabadilisha status mwaka wa pili sasa, Hey there! Im using
WhatsApp sasa unadhani sijuiTungekutanaje kama hutumii Whatsapp
6. Superstar wetu mmoja kaandika Urgent calls only?. We vipi? Kwani we fire(fanya), au ambulence au polisi
7. Haka kabishoo kameandika Can't talk, WhatsApp only?. Sasa una simu ya nini? Si uitupe uwe unashinda Facebook? Simu kazi yake ya kwanza kuongea sio
Whatsapp
8. Huyu mshamba kaandika At the movies? wiki ya saba sasa, sinema gani ndefu hivyo wewe Au unafanya kazi ya kuuza tiketi hapo sinema?
9. Dogo kaandika At school? sasa Whatsapp ya nini? Utapata Div O wewe
10. Hahahahahaha eti ?Battery about to die?
miezi sita mfululizo, badilisha hiyo betri?
Au mtaa wenu hakuna umeme miezi sita
hujachaji simu? Si kalalamikeni TANESCO? Au nikununulie jenereta?
Unaudhi
11. Hivi najiuliza we mdada huu mwezi wa
nne sasa eti ?At the gym? unajitayarisha
kwa Olympic
12. Bosi status yako ya ?In a meeting?
mwezi mzima inachekesha, maliza huo mkutano rudi kwenu.

WAHUSIKA BADILISHENI KABLA SIJAWABLOCK


What's App.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom