Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,581
- 46,176
1. Mwaka 1994 Bakili Muluzi aliyekuja kuwa Rais wa Malawi aliwapa ahadi ya kila mwananchi kupewa pea ya viatu endapo watamchagua kuwa Rais wao.Baada ya kuchaguliwa akawaambia wananchi wake hakuna namna angeweza kujua saizi za miguu yao wote ili waweze kupata viatu vyao walivyohaidiwa wakati wa uchaguzi hivyo asingeweza kuitimiza ahadi yake.
2. Mawaziri nchini Cameroon mara nyingi huwa wanalazimika kukutana na Rais wao Paul Biya airport kwa ajili ya shughuli za kiserikali kwa sababu anaendesha nchi yake kutokea Intercontinental Hotel iliyoko Geneva, Switzerland, Ulaya.
Aliwahi kukaa kipindi cha miaka mitatu(2015-2018) bila kuitisha kikao cha baraza la mawaziri.
3. Museveni amemtua mke wake kuwa waziri. Yani waziri wa Elimu wa Uganda ni mke wa Rais. Mtoto wake ni Mkuu wa kikosi maalum cha jeshi.
4.Rais wa Kwanza wa Zimbabwe alikuwa akiitwa Canaan Banana. Wananchi walizoea kufanyia jina lake la Ndizi utani sana.Mwaka 1982 alipitisha sheria ya kuzuia kutumia jina lake katika kwa utani.
5.Mobutu aliyekiwa Rais wa Congo DRC alipiga marufuku matumizi ya majina ya kizungu na kutaka raia wote wabadili majina ya kizungu kwenda ya Kiafrika.Yeye mwenyewe alibadili jina lake kutoka Joseph-Désiré Mobutu hadi Mobutu Sese Seko Kuku Ngbendu Wa Za Banga.
Aliibadilisha nchi yake jina pia kutoka Congo na kuiita Zaire.