tatanyengo
JF-Expert Member
- Mar 30, 2011
- 1,134
- 280
Ukiwa umebaki takribani mwezi mmoja kufikia kilele cha ujenzi wa maabara katika shule za sekondari zote nchini, kumeibuka tafrani katika maeneo mbalimbal nchini. Tafrani hizo zinatokana na wanasiasa kutumia mbinu mbalimbali ikiwezo nguvu katika kuwachangisha michango.
Mfano, walimu katika halmashauri kadhaa wamekatwa mishahara bila ridhaa yao, baadhi ya viongozi kutoa kauli zinazokinzana (Lusinde - uchangiaji ni hiari, mkuu wa wilaya Fatma Ally - uchangiaji ni lazima), Waziri wa TAMISEMI Kasimu Majaliwa kukanusha kuwa serikali haikuagiza walimu wakatwe mishahara, Mkuu wa wilaya ya Uyui kumsimamisha mtendaji wa kijiji kwa kushindwa kufikia malengo ya uchangiaji na baadhi ya wananchi mkoani Singida kuasi na kuwashambulia watendaji waliokuwa wanachangisha michango ya maabara. Ilimradi tu ni mshike mshike. Kila kiongozi kuanzia wakuu wa mikoa hadi watendaji wa vijiji hakuna anayetaka kuonekana mzembe. Kwa jinsi hali ilivyo hasa vijijini, baadhi ya vijana wamekimbilia porini kukwepa sekeseke la watendaji.
Yawezekana katika eneo lako kuna vituko vinavyohusiana na michango ya maabara, tuendelee kujuzana ili watanzania wafahamu kinachojiri katika nchi yao.