Vituko vya uchaguzi 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Vituko vya uchaguzi 2010

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by kalikenye, Sep 21, 2010.

 1. k

  kalikenye JF-Expert Member

  #1
  Sep 21, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 1,616
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  Ndugu wanajf

  Mambo mengine yanayoyasikika na kushuhudiwa kwa macho kuhusu uchaguzi mkuu wa 2010, yanastahili kupewa jina moja tu VITUKO VYA UCHAGUZI kwani naamini kuwa huwa ni nadra sana kufanyika katika kipindi tofauti na hiki.

  Kwa maslahi ya historia ya nchi yetu, nashawishi mambo haya kuwekwa kwenye kumbukumbu kwa kuanzisha thread kuhusu mambo ambayo yanaonekana kuwa si ya kawaida kusikika au kuonekana katika maisha ya kila siku japokuwa mengine hutokea.

  Lakini kwa kuwa yanatokea katika kipindi hiki cha uchaguzi na katika harakati za vyama vya siasa au wagombea kutafuta uhalali wa kuchaguliwa na kupewa ridhaa ya kuongoza, hayana budi kuhusishwa moja kwa moja na uchaguzi mkuu wa 2010.

  Aidha nashawishika kuyaweka kwenye kumbukumbu kwa sababu mengi yao, hayapewi nafasi katika vyombo vya habari aidha kwa makusudi, bahati mbaya au kutokuwa na mvuto kwa wahariri na waandishi wetu wa habari.

  Kwa upande wangu naanza na kituko kifuatacho.

  Mgombea Urais kupitia CCM, Bw. J.M. Kikwete, akiwa katika safari ya kampeni Mkoani Rukwa, gari lake lilipata ajali ambayo lau kama angalikuwemo, pengine habari ingekuwa tofauti kwani gari hilo limekuwa written off kiasi ambacho kama comprehensive insurance, basi Insurer ajiandae kununua gari jingine jipya. Mungu saidia JMK alikuwa ametangulia kwa Chopa.

  Lakini jambo la ajabu ni kwamba tukio hilo halikutangazwa na chombo chochote. Lakini kubwa kuliko yote ni kwa gari hilo kubanduliwa namba fasta baada ya ajali na kupekelekwa katika kituo cha polisi cha Namanyele likiwa halina namba.
   
 2. k

  kalikenye JF-Expert Member

  #2
  Sep 21, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 1,616
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  JK akataa kutumia jukwaa aliloandaliwa kwenye uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga. Ni baada ya Mzee Mzindakaya kukata kipande cha carpet lililotandikwa kwenye jukwaa hilo.

  Stori yenyewe ilikuwa hivi.

  Mafundi wakiwa tayari wametengeneza jukwaa la muda lililogharimu takribani Sh Laki Nne na kuwekwa Carpet lenye hadhi ya "Presidential" alitokea Mzee Mzindakaya kama vile mhusika alietaka kujua maendeleo ya maandalizi. Huku akijifanya kukagua uzuri wa Carprt hilo, ghafla akatoa kisu kidogo na kunyofoa kipande cha carpet hilo.

  Licha ya tukio hilo kufanyika fasta na kwa umahiri wa juu, lakini washkaji wa usalama walilinyaka japokuwa hawakumuuliza Mzindakaya kulikoni, na hivyo kuamua kumtonya JK, ambaye wakati wa kutoa hotuba, badala ya kutumia jukwaa aliloandaliwa, aliamua kubaki kwenye jukwaa la VIP, na kutoa hotuba hapohapo.

  Tukio hilo, liliwagusa wananchi wengi kiasi cha kusikika wakisema kuwa huyu bwana ni mzima kikweli.
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Sep 21, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hahahaah mkuu endelea kutujuza, nadhani Sheikh Yahaya alimtonya!
   
 4. p

  pierre JF-Expert Member

  #4
  Sep 21, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 211
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  aache woga.Amwamini Mungu aliyempa hiyo kazi kuwa atamlinda aache mambo ya wasiwasi na hofu.
   
 5. k

  kalikenye JF-Expert Member

  #5
  Sep 21, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 1,616
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  BBA
  Tangazo la mpigie kura Mwisho Mwampamba lazua maswali, watu wauliza "KWANI YUKO CHAMA GANI?"
   
 6. k

  kalikenye JF-Expert Member

  #6
  Sep 21, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 1,616
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  ETI MBOWE MTOTO WA NYERERE

  Wana JF nimeinyaka hii katika viunga vya Mjini Moshi kuwa ati Freeman Mbowe ni mtoto wa Nyerere. Katika maongezi baada ya kupata moja mbili kwenye baa moja iliyopo hapa Moshi maeneo ya Kiusa, niliwasikia jamaa wakibishana kuwa Mbowe ni mtoto wa nje wa nyerere.

  Mjenga hoja katika kuhalalisha hoja yake ya kuwa ati Mbowe ni mtoto wa Nyerere, alitoa mfano wa ujasiri wa Mbowe kuwa ni kielelezo tosha cha uhusiano wa Nyerere na Mbowe. " Bwashee, Mbowe ni mtoto wa Mwalimu ati, ni mchagga gani ana courage ya kihivyo kama ya Nyerere" Alisikika jamaa huyo akisema, na kuongeza " Ukiondoa makengeza, kila kitu ni copyright na Mwalimu"

  Du!!!!! nikaona hii kali nikajiondokea zangu kuwahi daladala.
   
 7. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #7
  Sep 21, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Wee ondoka zako!
   
 8. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #8
  Sep 21, 2010
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,507
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 180
  vituko vya uchaguzi hivyoo!!!!!
   
 9. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #9
  Sep 21, 2010
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  HAHA HAHA HA H AHHAHAHAHA HAHAHA HAHA AHAH HA HAH A:becky:
   
 10. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #10
  Sep 21, 2010
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,507
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 180
  UCHAGUZI WAITIA ADABU CCM

  Zile mbwembwe zilizozoeleka za wanachama wa CCM za kujaza Baa na kufurahi kila linapotokea tukio la ujio wa Kikwete, hazionekani katika kipindi hiki.

  Hali hiyo ilijitokeza jana mjini Iringa ambapo hadi saa 4 usiku baa zote maarufu zilikuwa tupu kama vile hakukuwa na tukio la ujio wa JK.

  Tofauti na siku nyingine ambapo ujio kama huo hushuhudia kufurika kwa sare za Kijani na Njano, hali jana ilikuwa tofauti.

  Ama kweli uchguzi wa mwaka huu ni kiboko.
   
 11. Tonge

  Tonge JF-Expert Member

  #11
  Sep 21, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 696
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  JK nae anaimani sana na mambo ya kishirikina, dnio maana akampeleka sheikh yahaya kutibiwa india na anamtegemea sana kwenye uchaguzi huu, mzindakaya ni mtoto wa mchawi lazima amuogope sana kwa imani yake.
   
 12. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #12
  Sep 21, 2010
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Yu wapi surayakwanza.
   
 13. coby

  coby JF-Expert Member

  #13
  Sep 21, 2010
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 342
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Katika kura za maoni za CCM, nec ilimuondoa Bashe hali iliyozua mazungumzo haya:

  Swali; Mbona mmemuondoa Bashe kwa kigezo cha kutokua raia wakati uhamiaji wamethibitisha yeye ni raia halali
  CCM; Uhamiaji hawana data za ukweli kama sisi na ni wababaishaji
  Swali; Wazee wamesema kuwa MKULO si raia halali wa Tanzania, mnalizungumziaje hilo
  CCM Hilo si kweli kwani Mkulo ni raia halali wa Tanzania hata uhamiaji wamemthibitisha
   
 14. coby

  coby JF-Expert Member

  #14
  Sep 21, 2010
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 342
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wote tunafamu kuwa Makamba akirushiwa dongo haipiti siku lazima awe amelijibu tena kwa mbwembwe na misemo kemkem. Safari hiyo alianza yeye kwa Dr. Slaa,

  Makamba; Eti ni mchumba wake!!, yule ni kimada wake tu

  Dr. Slaa akaijibu hiyo,

  Dr. Slaa; Makamba aache kunifuatilia la sivyo nitasema kwa nini alifukuzwa ualimu wa shule ya msingi!!

  tofauti na hulka yake, Makamba alikaa kimya kama siku mbili tatu hivi kisha akaibuka,

  Makamba; Dr. Slaa ninamueshimu sana kwani ana mchango mkubwa katika taifa hili!!!!!!!!!!!!!!!
   
 15. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #15
  Sep 21, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Tutasikia mengi uchaguzi wa mwaka huu
   
 16. Naloli

  Naloli JF-Expert Member

  #16
  Sep 21, 2010
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 416
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
   
 17. Naloli

  Naloli JF-Expert Member

  #17
  Sep 21, 2010
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 416
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  UZUSHI wa kwamba MBOWE ni mtoto wa nje wa MWL NYERERE ni uzushi ulio enea sana mjini moshi na wilaya za HAI na SIHA. Watoa uzushi huo wanadai wakati wa kudai UHURU Mwl alikuwa anafadhiliwa na mzee MBOWE na mara nyingi alipokuwa akitafutwa na serikali ya wakoloni alikuwa anajificha nyumbani kwa Mzee MBOWE sasa uswahiba huo ukapelekea Mwl ku cheat na mke wa Mzee MBOWE ndipo FREEMAN AIKAEL MBOWE alipopatikana na kuletwa duniani. Na watoa uzushi huo wana sema kuwa FREEMAN alizaliwa siku ya UHURU na ndio maana akapewa jina la FREEMAN ( kuhusu FREEMAN kuzaliwa tarehe na mwezi wa Tanganyika kupata uhuru nakumbuka MBOWE mwenyewe katika makala zake magazetini amewahi kuthibitisha hilo) Lakini suala la FREEMAN kuzushiwa ni mtoto wa NYERERE ni la ukweli na kunawatu ukibahatika kuonana nao katika viunga vya moshi wanathibitisha uhusiano wa Mwl. na FREEMAN utadhani walishuhudi wakati tendo la kumtafuta FREEMAN likifanyika. NILICHOTAKA KUWAJUZA WANA JF NI KUWA UZUSHI HUO UMEENEA SANA MOSHI(Vunjo, kilema,Marangu na kibosho),HAI, na SIHA
   
 18. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #18
  Sep 21, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,274
  Likes Received: 19,421
  Trophy Points: 280
  MJENGWA kashuhudia hili?? Itakuwa bora kama yupo na anashuhudia.
   
 19. k

  kalikenye JF-Expert Member

  #19
  Sep 22, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 1,616
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  MWAKALEBELA AMFUNIKA JK IRINGA.

  Jana baada ya Mwakalebela kumaliza kutoa salaam kwa wananchi wa Iringa, umati huo ulianza kuondoka kabla JK hajaanza kuhutubia. Je hii ina maanisha kuwa walikwenda kumsikiliza yeye tu?
   
 20. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #20
  Sep 22, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,650
  Likes Received: 21,865
  Trophy Points: 280
  He He He! hii nimeipenda sana, lile kombora kwa Makamba ilikuwa kiboko yake. Ukiona Makanba kanywea ujue wamemgusa pabaya.:smile-big:
   
Loading...