Vituko vya Rais Kikwete dhidi ya Albino

Ileje

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
13,234
Reaction score
20,594
Wakati bajeti ya wizara ya afya imekwisha somwa na kupitishwa bungeni kwa mwaka 2015/16, eti JK atahakikisha vifaa na madawa kwa ajili ya watu wenye albinism yanatengewa fedha na kununuliwa na kwamba vyote vitakuwa bure! Ahadi hii ameitoa leo huko Arusha katika sherehe ya siku ya kimataifa albinism!

Hiki ni kituko kwani waziri wake wa afya hakuzungumzia cho chote kuhusu suala hilo wakati wa bajeti ya afya! Na kama JK atalazimisha kutekelezwa kwa ahadi basi ama bajeti ya wizara itavurugika au itakuwa ahadi mpya ambayo haitatekelezeka hadi anamaliza muda wake October mwaka huu!!

Cha kujiuliza hivi JK hakomi kuahidi ahadi hewa au haoni aibu kwa kutotekelezeka kwa ahadi lukuki alizowaahidi wananchi nchini kote mwaka 2010?!


====================================

Chanzo: Mwananchi
 
huyu naye naona anaomba bora liende
 
Anadhani mwaka kesho atakuwa bado ni rais.
 
Jamani hebu tuache kumdhihaki mkulu waziri wake aliyasema hayo kwa ufasaha kabisa
 
Tatizo JK na mawaziri wake siku zote husoma misahafu tofauti.
 
Watanzania ni wajinga sana. Dawa yao kuwaambia uongo kwa sabb uongo ni mwepesi kueleweka. Big up my president!
 
Naye Jk na CCM yake akawaambia MAWAZIRI wake na wanachama wa CCM

KESHENI mkiomba kwani hamjui siku wala saa atakayokuja Dr
Slaa na UKAWA yake,Nami naenda Ulaya kuwaandalia MAKAZI ya kudumu,ili nitakapokuwa nanyi
muwepo,kwani CHADEMA ikichukua nchi mwaka huu,lazima mafisadi tuhame nchi.

Nanyi muonapo wa-Tz wanaipinga sana CCM na kuisapoti CHADEMA ,huku tume mbalimbali zikiundwa, basi mtambue muda wa wa MATESO kwa MAFISADI
umekaribia.

Wala msitishwe na wingi wa watia nia wenu wa CCM,kwani hata Lowassa mwenye pesa nyingi za KIFiSADI,lakini kamwe hawezi kuwa rais wa nchi hii.

Kisha Lowassa alipoyasikia hayo na kauli za makutano,basiakakwea tena IKULU kumuomba Rais ASIMFILISI,ASIMFUNGE WALA ASIKUBALI LOWASSA AJIUZURU, Lakini kabla ya wananchi hawajamsahau Lowassa na ufisadi wa RICHMOND,EPA,na RADA na ndicho kipindi yule katibu mkuu wa CCM mwizi wa tembo akijiandaa kuanzaa ziara za kuwahadaa wananchi mikoa mbalimbali,
akatokea Kafulila,Mbowe ,Mnyika na Zitto na jeshi lao lote wakaibua ufisadi wa ESCROW,na Kafulila akasema na "Nitakaowabusu hao ndio wezi waliokula pesa za Escrow na kulifisi taifa",basi akiwa bungeni akawataja jaji Werema,Pinda na Chenge nayo kamati ya PAC kupitia Zitto Kabwe ikawataja wengine wengi hata wale waliokuwa wamefichwa na wengine walioiba na kubeba fedha kwenye magunia kule kwenye benki ya Stanbic,bt Ikulu ikawalinda.

Mara AG WEREMA akatoa UPANGA ALANI na kumtishia Kafulila,mfuasi wa UKAWA kutaka kumkata shingo,ndipo PINDA kwa fedheha kubwa akamwambia WEREMA"rudisha upanga wako
alani,KIKOMBE tulichotupiwa na Kikwete hatunabudi Kukinywa.

Moja kati wa mayahudi wale aitwaye Muhongo hakuamini kama Kafulila
anaweza kitikisa serikali,mara TIBAIJUKA akasimama na kusema yeye hakujua kama pesa aliyokula ilikuwa ni ya kifisadi ya Escrow na Rugemalila aliyempa,ati alimpa kama kaka yake kwa ajili ya shule zake za Kajumulo

Basi siku ya3 wezi wakaenda pale ofisini kwa spika na ofisi ya PAC ili waibe nyaraka,lakini wakazikosa.

yule morani waliyemkuta getini
akawaambia mnayemtafuta(document za PAC) hazipo..Kafulila na Zzk wameshapaa nazo kwenda Kigoma na wapo
kuume kwa UKAWA

Basi wanaCCM walipoyaona hayo,kwa masikitiko wakasema"HAKIKA MWAKA HUU LAZIMA CCM ING'OKE NA CHADEMA KUPITIA UKAWA WACHUKUE NCHI"
 
President anauwezo na mamlaka kikatiba kutamka lolote na likatekelezwa...over!

Kama ndio hivyo ile meli mpya na kubwa ziwa victoria na uwanja wa ndege wa kimataifa wa bukoba vitapatikana mwaka huu,ndugu zangu wahaya mpooooooo?
 

Kwani kwenye bajeti hakuna fungu la madawa? si hilo hilo ndiyo atatenga za hao ndugu zetu.

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…