Vituko vya Rais Islam Karimov wa Uzbekistan

Baraghash

JF-Expert Member
Dec 18, 2012
2,713
1,786
Rais Islam Karimov, wa Uzbekistan. nchi kutoka kati ya bara la Asia,amefariki dunia kwa ugonjwa wa kiharusi akiwa na umri wa miaka 78.

Alitawala nchi yake kwa mpini wa chuma kwa zaidi ya robo karne tokea nchi yake ilipopata uhuru wake baada kusambaratika utawala shirikisho la Urusi.

Aliweza kutawala muda wote huo kutokana na Sifa yake kuu,yaani kuudumaza,kuukandamiza na hatimae kuusambaratisha kabisa upinzani nchini mwake.

Hakuna habari zaidi zilizopatikana kutokana na tasnia ya habari na uhuru wa kutoa maoni humo ulivyo dhibitiwa na kuminywa nchini humo.Kutokana na utawala wake kuwa wa ki- imla, hakuna mrithi wa moja kwa moja anaetambulika, hivyo kifo chake kmeacha mwanya wenye ufa ya uongozi.

Karimov atakumbukwa kuwa Nduli, katili, mwenye hasira kali, kauli za kutisha na uamuzi wa haraka.Majeshi yake yaliwaangamiza kwa kuwapiga risasi mamia ya waandamanaji wasio kuwa na silaha kwa kosa la kupinga utawala wake mwaka 2005.

Aliwatia ndani Maelfu ya wapinzani wake lakini kubwa zaidi,lisilioweza kusahaulika ni kitendo cha vikosi vyake vilipo wachemsha wapinzani wake kwenye maji ya moto mpaka kufa.

Atakumbukwa pia kwa tabia yake ya kuwapigia makelele, kuwaadhibu, kufuta nyadhifa na kuchagua maofisa wake katika mikutano ya hadhara.

Alikaririwa akisema "niko tayari kunyofoa vichwa vya watu 200 ikiwa kwa kufanya hivyo kuta kuwa ni muhanga wa kuleta amani katika nchi - ikiwa hata mwanangu atafuata njia hyo, basi nita mkata kichwa mimi mwenyewe"

Karimov alipotembelea Jumuia ya ulaya na kukutana na kiongozi wa juu walipeana mikono;kitendo kilicholeta taharuki kubwa na kutuhumiwa kimataifa kwa mkuu huyo wa EU kukubali kupeana mikono na Karimov!

Karimov amezikwa jana

Tumejifunza nini?
 
Dunia tunapita watakuja wataiacha dunia, huwa nikiona vituko vya watu kijiona Miungu watu nafikiria kuwa wanasahau kuwa ni wapitaji kwanini tusiifanye dunia sehemu salama ya kuishi. Tujifunze kuwa ubinafsi sio mzuri angalia roho alizoziangamiza lakini mwisho wa siku nae kaenda inasikitisha.
 
article-urn:publicid:ap.org:e8ebbb847bca4493844a7578ba9b725e-I4kDSdE1z3a170e4dd850ab8755-924_634x423.jpg

Tunajifunza kwamba huyu ni mmoja wa madikteta halisi waliokuwepo duniani.
 
Tumejifunza kuwa watu wenye roho za kiuaji na kichawi wanakubwa na Magonjwa ya mfadhaiko wa moyo,kiharusi na kupelekea wao kufa kwa mateso na hatimaye kuiacha nchi ikiendelea kuwepo huku ukiwaachia tabu familia yako na ndugu zako maana hujui anaekufuata atakuwaje
 
ajabu inaonekana ni nchi iliyoendelea sana kiuchumi kuliko sisi
 
Tumejifunza mbele ya Mungu hakuna asiejaribiwa na kupatwa na mauti. Utajifanya mbabe lakini hatima ya yote unaishia kaburini peke yako.
 
Usawa wa kibinadamu na utawala wenye kuzingatia sheria ndilo suluhisho pekee la maisha yenye Amani hapa duniani,wakati na baada ya utawala wa kiongozi yeyote hapa duniani.
Japokuwa viongozi wengi duniani hawapo tayari kuona na kujifunza kwa wenzao wakiamini kuwa wao ndio mwarobaini wa amani zilizohujumiwa
 
Siwezi jifunza chochote kwa kiongozi dikteta haijalishi wa wapi,dikteta ni dikteta tu mwisho wa siku nae atakufa tu.
 
Back
Top Bottom