Baada ya kupata bingo wanaojiita matajiri wameanza kunipigia simu!

Nyamesocho

JF-Expert Member
May 5, 2023
476
1,244
Asikwambie mtu, kipindi cha nyuma alionekana si lolote mbele ya jamii kwa sababu hakuwa na chochote

Akiwa anatembea kwenye minada ya masoko mbalimbali vijijini kuuza viatu vya aina ya yebo yebo huku akiwa na baiskeli yake mkongojo hakujua siku moja angeamka akiwa tajiri

Anakumbuka siku moja akiwa anaenda mnadani kilometa 53 bahati mbaya baiskeli yake ikaharibika hatasahau siku hiyo, aliwaomba boda boda wamsaidie wamfikishie mzigo sokoni baada ya mauzo atawalipa walikataa, siku hiyo ilishindikana kufika sokoni akiwa katikati ya vijiji bado kilometa 20 afike mnadani

Iliposhindikana tajiri mmoja alipita na Toyota Hilux wakiwa wanafahamiana lakini tajiri alikataa kumbebea mizigo yake ili arudi nyumbani na ilibidi kuomba mji jirani na hapo atunze mizigo yake

Alianza safari kwa mguu kilometa 30 kurudi kwake boda boda wakiwa wanamfahamu lakini hakuna aliyempa lifti , akiwa amebakiza kilometa 10 afike kwake alikutana na mwalimu aliyekuwa wanafahamiana na kumuomba amkopeshe elfu 10 na mwalimu alimpa ambapo alipanda boda mpaka kwake na kulipa elfu 5 na kubaki elfu 5 ambayo aliiweka kwenye beti na kuibuka milionea zaidi ya milioni 274 alizopata

Baada ya uvumi kuenea mr K amepata mamilioni ya pesa,wanaojiita matajiri wanampigia simu ili wafanye biashara

Anasema ndugu zake ambao wanapesa na zaidi ya miaka 10 hawajawahi kumpigia simu hata salamu tu siku hizi kila baada ya dakika 5 wanampigia kumjulia hali

Cha ajabu tajiri aliyemuomba lift siku ile anampigia simu eti amuuzie gari

Alichokifanya ni kumpa mwalimu milioni 7 kama zawadi huenda yeye ndo alikuwa njia ya kupata hiyo pesa

Jamaa anasema kama umewahi kumuona kama takataka na sasa unampigia simu basi usitegemee atakupigia simu na hakuna chochote utapata kutoka kwake ni msimamo wake ameweka

Jamaa anasema anahama mkoa aende mkoa wa mbali akafanye biashara na hataki connection na watu waliokuwa wanamuona kama hohe hahe

Je jamaa yupo sahihi na msimamo wake?

Binadamu tupendane na kujaliana hujui kesho yake?
 
mmh!?
 
Sijui, ila ukweli ambao kila mtu anastahili kuulewa na kuuishi ni kuwa, kama huna kitu hakuna mwenye time na wewe,
Kwa hio alitaka hao matajiri wampigie wakati hana kitu kufanya nn? Kumsalimia au? Ukweli mchungu, duniani tupo kimaslahi tu, kikubwa kuhakikisha na wew unatumia watu wengine kama wew wanavyokutumia,

Hii ni unwritten law ya toka kuumbwa kwa dunia, leo huna hela, hata diwani hataki kuongea na wew, kesho ukiwa billionea utapewa mualiko na ikulu ya USA ukapate lunch na Biden huku mnapiga story mbali mbali, ndio nature, sio ubaya ila tuuishi huu ukweli utatusave
 
Back
Top Bottom