Vituko vya January Makamba

Vituko vya January Makamba

Jamani naibu waziri wa mawasilano Mh January Makamba kumbe hana nyumba ya kuishi kwenye jimbo lake anafikia hotelini na kufanya kazi zake hotelini na kuondoka Dar es saalam huwa anafikia Lushoto .
Mwenye data atupie hapo

Umetumwa wewe Mushi Kweka! Yaani posti yako ya kwanza hapa kusalimii wanaJF wala nani, umeanza kwa kuleta majungu na uwongo. Ndio mmeshafungua rasmi kampeni yenu ya kumpaka matope January? Tumepata habari zenu.

Kwa taarifa yako na wengine, January Makamba amejenga nyumba yake binafsi kijijini kwao Mahezangulu ndani ya shamba la ukoo wao, ambalo humo ndani yake kuna nyumba ya Babu yake na pia kuna ya Baba yake Mzee Yusuph Makamba. January alijenga hii nyumba kabla hata ya kugombea Ubunge na huwa anaitumia akiwa kijijini.

Lakini kwa vile Mhezangulu ni ukingoni mwa Jimbo la Bumbuli, mara nyingi hulazimika kulala Soni (sio wilayani Lushoto) kwa vile Soni ni kati kati ya Jimbo na akiwa pale inarahisisha shughuli zake za uwakilishi kuliko kurudi Mahezangulu ambapo ni mbali kufanyia shughuli za kila siku.
 
Back
Top Bottom