Vituko vya Corona Afrika

Vituko vya Corona Afrika

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
359,995
Reaction score
828,731
Ni wazi sasa baadhi ya nchi ya kiafrika zimeamua kwenda kinyume na kanuni za kimataifa za kitaalam za kupambana na virus vya Corona. Ni kama vile Afrika inataka kutoka kivyake na kuithibitishia dunia kuwa AFRIKA IKIAMUA INAWEZA...

Huko Madagascar rais wa nchi hiyo ametangaza kuwa majani ya aina fulani ya chai yanatibu virus vya Corona huku akithibitisha wagonjwa 20 kupona.. Shirika la afya duniani limesema dawa hiyo haijathibitishwa kitaalam na inaweza kuwa na madhara makubwa kiafya

Nchini Tanzania mkuu wa nchi amesisitiza maombi na matumizi ya kuvukiza maji ya mvuke kama tiba na kinga sahihi ya corona lakini wakati huo huo waziri wake wa afya akisema kuvukiza sio njia sahihi na salama kwakuwa njia ya hewa haikuumbwa kupitisha moto... Wananchi wamebaki na kizungumkuti kikubwa kushindwa kujua wamuamini nani

Nchini DRC wao wametoka kivyao... Wanasema virus vya Corona ni uzushi mtupu na wananchi wameanza kuhamasishana kwa njia ya muziki na kula bata.. Kwamba ukijichanganya kwenye kucheza na kurukaruka (dhana ya kutoka jasho) kama ile ya kuvukiza tuu... Virus vinakimbia

Nchini Uganda hali ni tofauti kidogo.. Spika wa Bunge la nchi hiyo ameidhinisha USD million 3 kinyume na maagizo ya mahakama ili zikasaidie mapambano dhidi ya corona huku kila mbunge akiingiziwa USD 3000 toka kwenye hilo fungu.. Ukostaajabu ya Musa utaona ya firauni.. Eti Museveni hana habari na hilo jambo na amewatahadharisha wabunge wasitumie hizo pesa kwakuwa ni kinyume na maamuzi ya mahakama

Huku mitaani mafundi nguo wamepata biashara ya kushona barakoa.. Usalama wake ni kiasi gani? Hilo sio muhimu kwa sasa.. Kikubwa kuziba pua... Utadhani corona ina harufu...
Vyovyote iwavyo Afrika inajaribu kutoa ujumbe fulani kwa mabeberu na hii inaweza kuwa mwanzo wa kuwindana hasa kama njia za Afrika zitafanya kazi.. Lakini mpaka hii corona ipite tutashuhudia mengi mno
Je umesikia na hiki kilio cha nchi za Afrika kutaka kusamehewa madeni yake makubwa na mabeberu ili pesa hizo zitumike kupambana na korona?

Nje ya mada: corona imeua biashara ya lipstick

Jr
 
Ninachoenjoy n kwamba kila mtu anambinu zake za kujikinga africa maana hata wao waliouleta china hawajatoa mbinu zao hadharan mpaka ugonjwa unaisha china, vip mataifa yaliyopukutika kama majan ital marakan na mengine kikubwa uhai tu Africa lazma tusimame kivyetu vyetu

Unachotakiwa ukijue kutoka kwa mabeberu n hawatupend wanatuchukia zaid unavyomchukia mtu aliyekukosea maishan mwako hawana huruma na sisi hata kidgo wanataman tungepukutika wote na corana naona inazid kugonga mwamba

Ushaur wangu hao mabeberu kipind hich sio wakuwasikiliza hata kidgo akili ya kuambiwa changanya na yako
 
Angalau uganda imechukua hatua za moja kwa moja kuwasaidia wabunge wake,sisi hata tukisamehewa hayo madeni hizo hela hakuna mnyonge atakayejua zimemsaidiaje!! Sanasana zitatumika hapi kidogo kuwahamasisha wanyonge wavae barakoa ambazo hawana,na pesa za kununulia pia hawana,Mungu awalinde wanyonge.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ule mkopo wa World Bank kwa nchi ziliathirika uzingatie hatua za nchi hizo katika kupambana na corona.
Waandikie barua uwashauri hivyo. Ila ujue wao pia wanafanyabiashara ya kukopesha pesa. Wateja wao ni hao hao.
 
Huku kujitia chizi kulitokea Belarus. Rais wao akasema kwakua huu ugonjwa ni mafua na mafua yanapona kwa mazoezi basi wananchi wapige mchaka mchaka, ligi hamna kusimama ili misuli ipashwe moto na vodka zinywewe kwa wingi. Hilo tangazo akalitoa Aprili 4 mwaka huu, Kilichofuata ITV? Kesi 6264 za corona within 16 days.

Hii njia ya kujifukiza mtaalamu Isaac Ndodi ndiyo alikua anapenda kuitaja kama tiba ya mafua alipoku na kipindi chake pale channel 10. Now if you think he is a credible nigga when it comes to health and stuff endelea kusoma. Nilikua nasoma na dada wa makamo akwa anahangaika kupata mimba, na mtaalamu Ndodi (ni mchungaji by the way) wapo kanisa moja.

So mdada akamuomba ushauri Ndodi, afanyaje ili apate mimba. Ndodi akamuambia "Hizo dawa za nywele jua likiwaka zinayeyuka majasho yenye kemikali yanasambaa mwili mzima, wewe hautakuja kupata mimba" mwaka baada ya utabiri wa Ndodi yule dada akapata mtoto wa kiume.
 
Niko nje ya mada...biashara la Lipushaini na lipustiki imekufa..aisee we jamaa 😀 😀 😀 😀 😀

Everyday is Saturday.................... 😎
 
1587615228565.jpeg



Ni mashing ya kisasa ya kujivukiza.
 
Masikini akiomba hela kwa kusingizia kitu halafu ukampatia anajiona mjanja na wewe fala
Pia ina apply kwa wazungu pia viongozi wa Africa wanaomba wasamehewe madeni ila wapambane kwa kushona mask maana dawa hakuna
Ila hizo hela wakipewa tu wanaanza kutukana wazungu na kuwaona mafaaala
Nchi nyingi zinapewa hela zifanyie hiki wao wanabadilisha matumizi lakini wanatuchora na ukienda tena wanasema wapeni masikini hao
Mungu atunusuru na yote mabaya
Corona inauwa jihadhari


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Back
Top Bottom