Trainee
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 3,024
- 4,031
Mkiambiwa hakuna cha kumzidi akili binadamu mjue hakuna kwelikweli. Huyu jamaa wanamwita akili Mnemba au kwa lugha ya kuzoeleka zaidi akili bandia kwakweli ana vituko sana. Nitaweka hapa baadhi ya madhaifu yake ucheke kidogo na wewe
Jamaa kwenye kufikiri ni mtupu sana yaani ukimpa ngoma inayohitaji reasoning kidogo tu anachemka. Mfano kwenye mahesabu jamaa alichomeza ni kanuni tu kwahiyo ukimpa swali ukalichezesha kidogo tu lazima aende o.p
Huyu jamaa pia nimetambua anakariri na hataki kuwa nyumbufu kwenye kile anachokijua. Nimemchalenji kidogo tu kwenye maswala ya muda wa miji na jotoridi jamaa akapotea vibaya. Yaani kwa kuwa Dar tunatumia GMT +3 basi ukichezesha kidogo ukamtajia nyuzi za longitudo tofauti na 45°E basi jamaa kwenye calculation zake yeye anatumia 45°E.
Jamaa anasema hawezi kuchunguza picha akaichambua. Nilimpa picha mbili nikamwambia aangalie kama picha hizo ni mtu mmoja au watu wawili tofauti akabaki kujing'atang'ata tu. Nikamwuliza kama anaweza kutambua ukubwa halisi wa objects zilizopo katika picha akadai ataweza lakini mpaka apewe vitu fulani fulani ambapo nikiangalia nakuta vitu hivyo vyote ukivipata inakuwa haina haja ya kumtumia tena yeye maana kila kitu unamaliza
Kwa ufupi wanaomtegemea huyu jamaa wawe makini sana kwani anaweza kukupeleka chaka moja kwa moja kama utaamua kuweka akili yako kando na kumtegemea yeye. Nimemjaribu mara nyingi sana na vitu vingi sana kwa namna na muda tofauti tofauti. Nimejaribu ChatGPT, Ask AI, Chatbot AI
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, jamaa yupo vizuri kwenye lugha na historia japo sijamjaribu sana kwenye nyanja hizo.

Attachments
-
Screenshot_20240818-174504.png76.1 KB · Views: 18 -
Screenshot_20240820-162526.png120.2 KB · Views: 24 -
Screenshot_20240818-173445.png127 KB · Views: 20 -
Screenshot_20240818-173435.png188.3 KB · Views: 21 -
Screenshot_20240820-162547.png108.9 KB · Views: 19 -
Screenshot_20240820-162808.png127.7 KB · Views: 23