Vituko mitandaoni. Tupia chako



Tafakuri Jadidi:

Kwanini Tuwatafakari Wanafunzi Wasudan Na Wagonjwa Wetu Muhimbili..?

Ndugu zangu,

Nimeangalia kwa masikitiko namna wanafunzi kutoka Sudan wanaosomea tiba Muhimbili wanavyoelezewa kwenye media yetu na hususn mitandao ya kijamii. It’s a shame to our nation. Ni aibu na kwa hakika ni fedheha kwa nchi yetu.

Natafakari namna wanafunzi hawa kutoka Sudan wanavyotutafakari kwa namna tunavyowatafakari. It’s pure sexism and steriotype.
Kwa maana tunawaangalia kingonongono na kuwadhalisha kwa mtazamo wa kijinsia.

Hawa ni vijana wa kike waliopambana kwenye elimu na wangependa waangaliwe na kupimwa kwa uwezo wao kiakili na si kingonongono.

Ajabu wenye kushabikia upumbavu huu wengine wana mabinti zao wa kuwazaa wa umri wa kuwazidi wanawake hawa wasomi wa tiba kutoka Sudan.

Je, wangejisikiaje mabinti zao wangeangaliwa kingonongono badala ya uwezo wao kitaaluma?
Kimsingi kinachofanyika mitandaoni kinaweza kabisa kusemwa ni ‘ Sexual harassment’- Unyanyasaji wa kijinsia.

Kama taifa la watu wengi waungwana, tunapaswa kuwaomba radhi wanawake hawa vijana wasomi wa tiba kutoka Sudan.

Upumbavu mwingine?

Ni pale tunapowadhihaki wagonjwa wetu walio Muhimbili. Yaani, mtu mzima anadhihaki kwa kufanya utani wa kuwa ugonjwa ili apelekwe akalazwe Muhimbili ahudumiwe na wanafunzi wa tiba kutoka Sudan.

Hivi tunajua maana ya kuugua na kulazwa hospitalini?

Wagonjwa walio Muhimbili wako kwenye mahangaiko kupambania afya na uhai wao. Kwao hawamwangalii daktari kingonongono bali kama msaada.

Kama taifa la watu wengi waungwana tunapaswa kuwaomba radhi wagonjwa wote waliolazwa Muhimbili na kwenye hospitali nyingine huku tukiwatakia heri wapone haraka.

Ni Tafakuri Jadidi.

Maggid Mjengwa.

Zanzibar.
 
Mwenyewe nimetafakari sana,

Jibu nililolipata,Tz ngono mbele kuliko chochote.
 
Kwenye nchi za wenzetu hii ni sexual harassment...ila huku kwetu hatunaga huu msamiati kwenye kamusi zetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…