Mlevi na Mlokole..
MLOKOLE
I; “Unakunywa bia!?
MLEVI; “Ndio.
MLOKOLE
I; “Kwa siku unakunywa bia ngapi!?
MLEVI; “Nakunywa bia tano!
MLOKOLE
I; “Bia moja bei gani!?
MLEVU; “2500/
MLOKOLE
I; “Ulianza lini kunywa bia!?
MLEVI; “Miaka 18 iliyopita!
MLOKOLE
I; “Kwa hiyo kwa siku unatumia zaidi ya 10,000??
MLEVI; “Ndio!
MLOKOLE
I; “Kama ungekuwa unatunza hiyo pesa 10,000 kwa siku leo hii si ungekuwa na Range Rover!?
MLEVI; “Samahani, naweza kukuuliza swali!?
MLOKOLE
I; “Uliza!
MLEVI; “Unakunywa bia!?
MLOKOLE
I; “Hapana!
MLEVI; “Nionyeshe Range Rover lako!
MLOKOLE
I akasepa upesi..