Vituko mitandaoni. Tupia chako

kuna siku nilienda kijiwe cha Ps kupasha kidogo, ile natoka nirudi zangu geto nakuta mlangoni hivyo vikobaz pair tano, pair tatu ni size 42 mguu wangu nyingine hazieleweki, aisee nilitumia zaidi ya dk 30 natafuta actually kobazi zangu ni zipi halafu zilikuwa mpya ndo nimetoka kununua few days tu hapo na ilikuwa usiku mnene. Bahati kobazi la mguu wa kushoto lilikuwa na kialama, niliondoka pale na viatu mguu mmoja kipya mguu mwingine kimechakaa kesho yake asubuhi nkaviangalia nikasema hapana hiki cha kulia sio changu
ikabidi nipige simu kijiweni kumbe kuna jamaa ambae alinitangulia kuondoka ndio alikuwa amechukua mguu wangu mwingine ikabidi nivirudishe nimuachie mpaka yule jamaa alivokuja kurudisha mguu mwingine nayeye kumbe mguu wa kushoto pia haukuwa wake yani ile siku aliondoka na viatu vyote sio vyake
yule mwamba alilalamika kinyama tangu siku ile ilikuwa nikienda pale viatu vyangu naeka kwenye mfuko naingia navyo ndani nilikaa siku tatu natembelea kobaz hazielewek
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…