Vituko mitandaoni. Tupia chako


Yote hayo nayafahamu, historia na mengine mengi tu, ila suala nzima hapa ni kuhusu kuheshimu utawala wa sheria, kama sote tumekubaliana hiyo sheria na katiba ndio itatupa muongozo, haipaswi tuwe na baadhi yetu ambao tukihisi mambo hayaendi tutakavyo basi tuichome nchi. Unamvamia muuza mkaa na kupora magunia yake yote kisa umekerwa kwamba mungu mtu wako amedhulumiwa.

Historia hizo mbovu zipo, huyo hapo Zuma alikua rais wa nchi mwenye mamlaka yote, alipaswa kuongoza kwa mbele kwenye kurekebisha, ila yeye aliendekeza ufisadi na ukabila, sasa ndio haya matunda yake. Hata huyu rais wangu Uhuru, napenda sana utenda kazi wake na uchumi wetu unakua kwa kasi, nchi inaendelea vizuri sana kiuchumi, ila amegoma kurekebisha ukabila, teuzi zake zimekaa hovyoo, kesho akiingia uraiani ujaribu kumkamata aisei huo upumbavu wa Afrika Kusini utakua cha mtoto maana kwetu hapa huwa tunakinukisha kinanuka.
Sasa hivi huyo Zuma anachekelea maana chaos zote hizo anazitumia kujilinda.
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…