Kuna wakati unalazimika kumaliza mambo kihuni namna hiyo ili nidhamu ipatikane
.
Ikibidi mtu aliwe kiboga ili kutengeneza heshima.
Ninazo shuhuda kadhaa zilizolazimisha matumizi ya nguvu ya aina hiyo ili kumaliza sintofahamu za kuchapiwa
Sijui bhana, labda ni kwa sababu ya maeneo ya uswahilini tuliyoishi watu walikuwa hamnazo
Lakini zamani miaka kadhaa iliyopita nilimuona mtu mmoja, alionywa sana na wazee wa mtaa, kutokana na kile alichokuwa anakifanya kwa mke wa jirani yake,
jirani ambaye ni kipenzi cha watu kwenye eneo hilo.
Kilichomkuta mtu huyo hatakuja kukisahau ikiwa yupo hai huko aliko.
Huwezi kuamini, mikakati yote lilipangwa na majirani wa mwenye mke.
Kama kulikuwa na mihemko basi wale majirani walikuwa na mihemko zaidi kuliko mwenye mali zake.