Vituko mitandaoni. Tupia chako

Iwe heri na fanaka kwako mama yetu na kiongozi wetu 2024.
Kwa vyovyote vile dhamana ya maisha kama taifa ipo katika mikono yako.
Tuna wajibu wa kukutakia matashi mema ,furaha yako na mafanikio yako ni yetu.
 
Aendelea kupumzika kwa amani , bado naendelea kutafaki aina ya uongozi wake ule, na kuzidi kumshukuru Mungu kwa zawadi ya maisha yake kwetu na huduma ya uongozi aliyojaliwa kwa ajili yetu.
Sio mimi tu naendelea kumkumbuka bali umma wa watanzania wengi tunamkumbuka si kwa mabaya bali kwa ile Karama ya uongozi alio kuwa nayo , hatuna litakalo zidi kutoka kwetu zaidi ya kumuombea pumziko jema la amani .
 
Endelea kusalia katika mwongozo wa Mungu 2024, mtumishi myenyekevu wa Mungu pope Francis,maombi sala na dua zote tunamuelekezea mwenyezi Mungu juu yako ili katika zamu yako hii ya uongozi kanisa libaki kuwa sehemu ambayo mwenyezi Mungu anapatika kwa watu wote jinsi alivyo.
 
Tumshukuru Mungu na kujivunia uongozi wako kanisa la dar es laam,
Hatuna budi kuendelea kumuomba Mungu azidi kuwa nawe 2024 kama alivyo kubwa nawe jana awe hivyo kwako na kuzidi kesho na wakati wote.
 
Endelea kupumzika kwa amani tukiendelea kumngojea kristo, historia ya kanisa haitakusahau daima.
Kama kuna zawadi ya pekee aliyotujalia mwenyezi Mungu jamii na kanisa kwa ujumla ni maisha ya huyu ndugu!
Matamanio ya wengi tungekuwa nawe tunapofunga hii 2023 na kuamkia 2024 pamoja nawe, lakini haiko hivyo ila lile pambazuko la milele litatukutanisha tena tukiwa hatuna udhaifu wowote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…