Najuwa hujavuta bangi hivyo nashindwa kukuelewa una maanisha nini kuwa hujaelewa? Wewe kama hauuzi unga wenzio wengi tu wanafanya hivyo, tena mbona hapo Amsterdam wanakuja sana? Si siri juu ya watanzania na biashara za uuzaji unga duniani. Vijana wengi tu hapa Bongo bishara yao ni hiyo, utakuta mtu kila siku yuko shambani Nigeria ama South Afrika kujitafutia bidhaa na kuzileta huko. Wakija huko wanaziuza kisha wananunua magari na kuleta huku Bongo, wanafanya hivyo kwani hawataki kukamatwa na pesa taslim uwanja wa ndege. Then magari yakija Bongo wanayapeleka show room kuyauza ili wapate hela zao. Huu mchezo unaeleweka sana, tena wengine wanasingizia wao ni ma agent wa clearing na forwarding huku kazi zao kubwa ni hizo za uuzaji unga.