theriogenology
JF-Expert Member
- Oct 7, 2016
- 8,748
- 15,731
VITU VYA KUZINGATIA KATIKA UKATAJI MIDOMO YA KUKU (DEBEAKING)
★ Utangulizi
Ukataji wa midomo ya kuku ni mojawapo wa majukumu ya kawaida kwa mfugaji na huusisha kuondolewa kwa ncha kali ya mdomo wa kuku kwa kutumia vifaa mbalimabli vinavyohusiana na shughuli hiyo.
Zoezi hili linahitaji kufanywa kwa uangalifu wa hali ya juu ili kuepuka madhara ya uvujaji damu na hivyo linahitaji mtaalamu.
Kwa kawaida zoezi hili husababisha stress kwa kuku, hivyo basi zoezi hili linashauriwa kuwa na maandalizi ya kutosha ili kupunguza stress kabla, wakati na baada ya zoezi zima la ukataji midomo.
★ Umri wa ukataji wa midomo
Kwa kawaida ukutaji wa midomo hufanyika wakati vifaranga wakiwa na umri wa siku moja hadi wiki ya kumi na nane
• faida ya ukataji wa midomo kwa kifaranga cha siku moja;
✓ Hupunguza udonoaji katika umri mdogo
✓ Mdomo huwa mlaini na hivyo kuepuka uvujaji wa damu
✓ Vifanga wanakuwa ni wepesi kuwadhibiti
✓ Zoezi zima laweza fanywa katika kiwanda cha utotoleshajina mara nyingi
zoezi zima linachukua muda mfupi
• Hasara;
✓ Vifaranga hupata maumivu pale wanapojifunza kula na kunywa kwa mara ya kwanza
✓ Kosa dogo linaweza pelekea kuharibika kwa mdomo wa kifaranga
✓ Vifaranga huvuta hewa yenye joto
✓ Na mara nyingi itakulazimu kurudia zoezi zima mara tu kuku waanzapo kutaga mayai
• Faida ya ukataji midomo vifaranga wa siku 6-10:
✓ Midomo bado huwa ni laini na hivyo zoezi zima linaepuka kusababisha stress kwa kuku
✓ Bado kuku ni wepesi kuwadhibiti na hivyo zoezi zima huchukua muda mfupi
✓ Upotezaji wa chakula ni kwa kiwango cha chini
• Hasara;
✓ 20% ya kuku watahitaji kukatwa midomo mara tu wakaribiapo kutaga
✓ Ukutaji mbovu waweza pelekea uharibifu wa midomo hivyo kuongezeka kwa vifo kwa vifaranga wako
✓ Umri wa utagaji wa mayai (sexual maturity) waweza ongezeka
• Ukutaji wa midomo kwa kuku wa wiki 8 mpaka 18;
✓ Unashauriwa baada ya ukataji wa mdomo ufanye leveling kwa kutumia kifaa chenye joto.
• Changamoto:
✓ Zoezi zima linahitaji uangalifu wa hali ya juu hivyo zoezi zima huitaji nguvu ya ziada
✓ Kuku hupata stress maradufu zaidi na hivyo huweza athiri utagaji wa mayai kwa muda
✓ Kuku hupoteza uzito na hivyo humchukua kuku wiki 2-3 kurudisha uzito wake wa awali
✓ Kuku huvuja damu nyingi na zoezi zima hupelekea kuku kupata shida katika kula na kunywa
✓ Ukataji mbovu waweza ongeza ulaji wa chakula kwa kuku
• Hatua za kufuata katika ukataji wa midomo ya kuku; (zingatia)
✓ Kwa kuku wa kuanzia wiki 8 na kuendelea unashauriwa kukata mdomo (lips moja baada ya nyingine) na mara nyingi unashauriwa kukata lips ya juu ikifuatiwa na lip ya chini ya mdomo
✓ Kwa kawaida inashauriwa kukata 1/3 au ½ ya lip ya juu na kata lip ya chini kwa usawa sawa na lip ya juu au unaweza ifanya yenyewe iwe ndefu kiasi kuzidi lip (mdomo) wa juu wa kuku.
★ Zuia stress kwa kuku kadli uwezavyo kwa kuzingatia yafuatayo;
• Kabla ya kukata mdomo;
✓ Hakikisha kuku wako wote wana afya nzuri nay a kuridhisha
✓ Hakikisha kuku wako hujawapa chakula kwa muda wa masaa mawili kabla zoezi zima la ukataji midomo haujaanza, mara nyingi mfuko wa kuhifadhia chakula cha kuku unapokuwa hauna chakula hupunguza stress
✓ Hakikisha huwapi chanjo kuku wako baada ya zoezi zima la ukataji midomo
✓ Zoezi zima hakikisha linafanyikia ndani ya banda au nje karibu na banda hii pia hupunguza stress kwa kuku
✓ Hakikisha unatumia kifaa chenye makali ya kutosha
✓ Wape kuku wako vitamin K kwa siku kadhaa kabla ya zoezi la ukataji midomo kuanza
• Katika zoezi zima la ukataji
✓ Kuwe na mwanga wa kutosha ili kuepuka ukataji mbovu wa midomo
✓ Tumia kisu kikali au tumia chuma chenye joto la kutosha
✓ Hakikisha huchomi ulimi wa kuku
✓ Unapotumia kisu au plaizi hakikisha upo na chuma cha moto kuu shape mdomo vizuri
✓ Unapotumia vifaa vya umeme hakikisha umeme upo katika kiwango sahihi na kama chuma cha moto hakikisha kiwekuwa chekundu kwelikweli
✓ Hakikisha hakuna uvujaji wowote wa damu katika midomo ya kuku
✓ Hakikisha umemshika vizuri kuku kabla ya kuanza kuukata mdomo
✓ Hakikisha unasafisha vyombo vya ukataji mdomo katikati ya zoezi zima
• Baada ya ukataji midomo
✓ Usiwazue kuku kula ama kunywa maji hakikisha unawaongezea chakula na maji maradufu
✓ Kuku wakishindwa kula na kunywa kwa muda hakikisha unawachanganyia chakula na maji
✓ Ongeza vitamins na antibiotic katika chakula kwa muda wa wiki moja (vitamin zinazoongezwa ni A,B complex, D3 na K)
✓ Kama kuku wanatoa damu hakikisha unauchovya mdomo kwenye chakula au mchanga kuepuka uvujaji damu zaidi
✓ Hakikisha unawaongezea muda wa mwanga kwa siku ili kuwawezesha kuku kula chakula kwa muda mrefu na hivyo husaidia zoezi zima la uponaji
✓ Wakague kuku wako mara kwa mara kuona kama wapo na chawa maana baada ya kuwakata midomo wanakuwa hawana uwezo wa kujisafisha vizuri
Imeandaliwa na C.E.O
JM Veterinary Service (JMVS)
Phone: +255686236365
+255712784472
Motto: We save You and your animal as family