Vitu vya kufanya siku ya hukumu

french

JF-Expert Member
Aug 2, 2017
3,525
3,649
Nina kesi ya madai mahakama ya mwanzo- yaani mimi ni mdai. kuna kila dalili ya mimi kushinda hii kesi. sasa naomba kujua

1 Hukumu huwa inatolewa kwa maneno tu au maandishi au vyote.

2 Mdaiwa kawaida huwa anapewa siku ngapi kulipa deni, deni ni kama milioni 10 hivi.

3 Je, baada ya hakimu kutoa hukumu natakiwa nifanye nini na ndani ya siku ngapi?

4 Je, siku ya hukumu kuna ushahidi wowote natakiwa niende nao mahakamani?

Ni hayo tu wakuu na kama kuna jambo lingine naomba nijuzwe.
 
Kwanza hukumu hutolewa kwa njia zote mbili maneno Kisha maandishi

Baada ya hukumu atua inayofuata ni kukazia hukumu

Katika hatua hiyo madalali wa mahakama huusika kwa habari ya kukazia hukumu

Ni process tena ya kuimba mahakama ili yale maamuzi yaende kutekelezwa
 
hapa kwenye kukazia hukumu nafanyaje, madalali wa mahakama ya mwanzo ni kina nani hao
 
Hapo hukumu ikishasomwa, utaambiwa ni baada ya muda gani, uenda kuchukua nakala ya hukumu, ukishaipata hiyo nakala hiyo, itategemea inasema nini, kwani kesi za madai nazo huwa ni changamoto sana, kupata haki yako, hata kama mahakama imetoa uamuzi, lazima uwe mbishi kweli kweli!!ukiona hatekelezi kile kilichoamliwa na mahakama , ndio unaenda kukazia hukumu, nayo ni kesi tena!!tatizo la kesi za madai, kama hana kitu cha kukulipa, hawezi fungwa labda wewe ndio uingie gharama za kumtunza akiwa jela!!ndio maana siku hizi kesi za madai ni chache, nyingi sana zinasukwa zinakuwa za jinai!!ukimkuta mpelelezi, mzuri hiyo hiyo ya madai inatengenezwa inakuwa jinai!!
 
ok, safi sana. uzuri naidai kampuni na sio mtu binafsi. kawaida mdaiwa anaweza pewa,siku ngapi ili alipe? hii ni mahakama ya mwanzo
 
Inategemea ,na uwezo wa mdaiwa!!lakini kama ni kampuni, nadhani hakimu atakuwa amelizingatia hilo, hatawapa muda mrefu sana!!omba mungu wasije kuwa wasumbufu tu,
 
inaweza fika mwezi? nauliza hivi sababu nitatakiwa kusafiri.
 
Hapo hukumu ikishasomwa, utaambiwa ni baada ya muda gani, uenda kuchukua nakala ya hukumu, ukishaipata hiyo nakala hiyo, itategemea inasema nini, kwani kesi za madai nazo huwa ni changamoto sana, kupata haki yako, hata kama mahakama imetoa uamuzi, lazima uwe mbishi kweli kweli!!ukiona hatekelezi kile kilichoamliwa na mahakama , ndio unaenda kukazia hukumu, nayo ni kesi tena!!tatizo la kesi za madai, kama hana kitu cha kukulipa, hawezi fungwa labda wewe ndio uingie gharama za kumtunza akiwa jela!!ndio maana siku hizi kesi za madai ni chache, nyingi sana zinasukwa zinakuwa za jinai!!ukimkuta mpelelezi, mzuri hiyo hiyo ya madai inatengenezwa inakuwa jinai!!
Nisahihishe kidogo
Ukimkuta mpelelezi asiye na maadili na mla rushwa anaweza kubadili madai kuwa jinai, wengi wanabambikizia watu keshi za wizi wa kuaminika au kujipatia mali kwa njia isiyo halali kwa kesi ambazo ni civil purely.
 
Back
Top Bottom