SIJUI NIANDIKE MAKALA AU KITABU??
kweli wanaume mna wake wa ajabu sana, mke anataka utandike kitanda? mke anataka ukae ukafue mashuka , mtoto amekojoa ukafue na kuanika matandiko? anataka uingie jikoni uanze kupika, ukate nyanya, ukate kituu na uonje chumvi kwenye mwiko...anataka upike chai/cofee na uonje kama sukari imetosha>>....INAWEZEKANA NINA MKE MWEMA, NINA MKE ALIYELELEWA AKAJUA KAZI ZA MWANAUME NA ZA MKE...tangu niwe na mdogo wenu katu haniruhusu kufanya izi kazi, uwa tunagombana sana asubuhi, naamka mapema , nashika brashi na dawa ya viatu ghafla namuona nyuma yangu...'dia unafanya nini???' ...nanyanganywa brash, naandaliwa nguo na kila kitu, yani mwanzoni ilikuwa taabu kufanyiwa kila kitu ila nshazoea na kuona haki yangu...WATOTO WA KICHAGA MIXER TANGA mna mambo sana...mnajua baba anataka nini na wakati gani...mimi ni kuleta fweza nyumbani, kulea mke na watoto na kuleta maendeleo.
TURUDI KWA TOPIC
Mleta mada kwa nini unameanza misala tu baada ya mzee kukosa kazi?
Mbona miaka imekatika haujawahi kumwambia aingie jikoni, afue nepi na kujipkia cofee?
Kama unakwazika weka binti wa kazi afagie nyumba, alambe mwiko-aonje chumvi
Shida yangu kubwa ni kuona unaonekana kuelemewa na mzigo wa familia kwa mwaka mmoja tu wakati mmesaidiana na mzee kwa zaidi ya miaka 6.
- Mama unashaurije waume wenye wako kibao ambao wake uwa hawafanyi kazi wanasubiri baba alete, je nao wachoke kama wewe? Hapo ndo ujue wanaume wenye wake wasiofanya kazi wana busara sana, ikitokea mme ndo hana kazi daah anatangazwa JF , uwazi na sani, ooh mume anakaa kwenye Tv, ooh mume hana kazi, ooh analelewa... nk nk ayo ni mambo ya ajabu best!!
Kama una kazi nyingi, tafadhali muweke dada au kaka wa kazi, hatukukupa kaka yetu akapike, akafue nguo za watoto, na mbona wakati ana kazi aya yote uliona poa??
Nakumbuka wakati ana kazi, na wewe haujawa na ka duka ka kusaidia kusogeza maisha ukisaidiana na mshahara wako haikuwa shida, leo hii unataka akafue?
Nakuomba dada yetu tafadhali muache mumeo apunguze stress, na mshahara ujao naomba umnunulie CD za kutosha, naomba uongeze channel za DSTV , uweke na binti wa kazi...Baba muache ajiriwaze, mpende kama ulivokuwa unampenda wakati ana kazi....nakuhakikishia mtu wenye ujuzi na mwenye maono kuna siku atapata kazi na utaanza kuona aibu kwa aya yaliyojitokeza wakati hana kazi.
Kuna mzee mmoja aliwahi kupitia hali hii akiwa injinia wa wakati wa Tics ya karamagi, akapata shida sana na madharau kibao hadi kufikia hatua ya kunyimwa gari na mke au hata nauli na kipesa cha kujikimu mpaka tukawa tunamsaidia....Baada ya kupata tenda na kurudi bandarini kitengo kingine, leo hii anamiliki canter, ana gari2 za kutembelea, na ghorofa lake limeisha pale kimara na amehamia july toka ki-jumba chake cha Morocco.
MKE UPENDO UMERUDI KANA KWAMBA NDO WAMEOANA JANA, WATOTO WALIKUWA WAJEURI SASA WANAMSALIMIA BABA KAMA MFALME, JAMANI TUJITAHIDI KUONESHA UPENDO WAKATI BABA AU MAMA AMEKWAMA. NINA MENGI ILA DADANGU TAFAKARI AYO KWANZA!!