Tatizo hapo ni kuwa umeolewa. Ingekuwa mmeoana kusingetokea tatizo kama hilo.
Tatizo lingine, ni pale mume anapokuwa mwizi akiwa kazini, akiachishwa kazi maisha yanakuwa magumu X 3.
Ukiona mwanamme mvivu namna hiyo ujuwe ni mvivu kazini pia na mvivu bedroom. Kwa situation kama hiyo usitegemee kama kuna ufumbuzi wowote utapatikana, hicho ndio kichocheo kikubwa cha wewe kutembea nje ya ndoa kama bado hujaanza mpaka leo.
Hapo issue ni kuwa jamaa sasa kawa mzigo maana kama hizo tabia nina uhakika hazijaanza leo lkn ukawa unamvumilia sababu na yy anachangia tena labda zaidi kwenye pato la familia!
Jamaa kachokwa sababu haleti chochote home kuchangia na hii ndiyo zenu madada wengi!Yalinikuta kama haya nilifukuzwa kwa kuitwa "mbweha"usiku wa manane miezi 7 baada ya kupoteza kazi ehehehehe
Last week nilikuwa naosha Vyombo ,akaniita mama F naomba unitengenezee coffee akiwa ameshika remote anaangalia TV
Nikamwambia naosha vyombo my dear ila kila kitu kipo mezani please nisaidie kutengeneza wala hakunyanyua mguu anasubiri nikatengeneze ,na hapo mtoto nimeweka mgongoni wangu alikuwa mgonjwa
Nikatengeneza kikombe chake nikampa akasema asante basi
jamani hivi kweli ni sawa unaamka asubuhi unamwacha amelala unarudi jioni hata net haijatolewa hiyo ni sawa??mmmh
inategemea na m/ke last year mwenza wangu hakua vizur kibiashara yani mimi ndo nlitake responsibilities zote ila sikuwahi kumfanya chochote kibaya wala kumdharau na alikua anashnda home ila mimi nkirudi nifanye kazi zote na sikuwahi kumsemanga mpaka aliporevival MUNGU WANGU shahidi yangu
Huyu mleta mada hajakuwa wazi sana kuhusu mazingira yote ya ndoa yake. Hata hivyo hapa hapakuwa mahali muafaka sana pa kukimbilia, ilikuwa kwanza waongee wenyewe ikishindikana ndio achukue hatua zingine
Hivi nyie wanaume kweli hauwezi kufika kipindi uone mkeo kazidiwa na wewe upo hata kumsaidia tu kuweka chai kwenye Kikombe ni ngumu?
Hata kufua nguo zako za ndani ni kazi??
Mie sijasema aje kuosha vyombo no..basi wakati mie nadeki na kupika kuna ugumu wa kufua Boxer zako mwenyewe?
Kutoa net Kitandani na kuweka shuka vizuri ni kazi??
Tena wanaume wa hivyo wapo humu humu mmu....
Kiatu kinavuliwa barazani
Soksi inatolewa sebuleni
Shati linatupwa koridoni
Suruali chumbani
Singlend bafuni
Tena wanaume wa hivyo wapo humu humu mmu....
Kiatu kinavuliwa barazani
Soksi inatolewa sebuleni
Shati linatupwa koridoni
Suruali chumbani
Singlend bafuni
Mwenzako anamuona jamaa mzigo sababu hana kazi!Angekuwa na kazi hata kama angekuwa hambebi mtoto angevumiliwa tu ahahahaha
Sijawahi kuwaza kwa vile hana kazi kwani najua hii kitu inaweza kumtokea mtu yoyote,
Ninachojiuliza hapa hata Kutengeneza Chai yako mwenyewe ni ngumu?
Mbali na hapo huoni mwenzio ananyonyesha mtoto anasumbua ,mama hulali hata kusema mke wangu ngoja nimsaidie hata kutandika kitanda?
ama mtoto amekaa karibu na wewe anacheza akilia unamwangalia tu?
Na nikikaa nae sasa ataona ninamsema kwa vile hana ajira ..
mmh?
Hivi nyie wanaume kweli hauwezi kufika kipindi uone mkeo kazidiwa na wewe upo hata kumsaidia tu kuweka chai kwenye Kikombe ni ngumu?
Hata kufua nguo zako za ndani ni kazi??
Mie sijasema aje kuosha vyombo no..basi wakati mie nadeki na kupika kuna ugumu wa kufua Boxer zako mwenyewe?
Kutoa net Kitandani na kuweka shuka vizuri ni kazi??
Mimi naona kama mkuu unaenda mbali sana, hebu rudi tu nyuma kidogo, kutoa neti kitandani ukaitupia juu inajalisha kama una kazi au huna? Mbona mimi naona kama nikitu kidogo sana ambacho wala hakiwezi kuudhalilisha 'uanaume'?
Stress zinamfanya nini mtu?
Je mwanamke nae akiwa na stress awe hivyo?
Hiyo ni tabia tu ya mtu kiukweli.
Hata kama una stress ukikaa na mtoto na kucheka nae stress zinapungua.