vitu vinatembeatembea mwilini

vitu vinatembeatembea mwilini

ngoshwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2009
Posts
4,141
Reaction score
950
Wakuu salamu.

Kwa muda wa zaidi ya miaka saba sasa nimekuwa nikisumbuliwa na mauzauza mwilini.

Najisikia vitu vinatembeatembea mwilini na mwili unawaka moto, pengine kama vichomi na hivi karibuni presha ilianza kupanda na kila ninapoamka muda wotewote miguu inakuwa kama inakamatwa na baadae mwili lzima unashambuliwa na nguvu zinazokunyima raha siku nzima.

Nimekuwa naomba sana na bado naendelea lakini ukimaliza kuomba ndio mashambulizi yanaibuka kama unapigwa viboko.

Kama kuna mdau ana uzoefu wa hali kama hii, tushirikshane.

Ninaendelea kumtumaini Mungu katika yote.
 
Pole sana Mkuu .... usiache maombi hata kama unapita katika majaribu mengi ,MUTUMAINI BWANA YESU . Pili nenda Hsp kapime Sukari ,presha, na kuangalia mzunguko wa damu katika mishipa yake .... Mungu atakuponya .
 
Nenda hospital mzee, pole sana. Kwa hili tatizo lako inawezekana una Tatizo la Neva (Neuropathy), High Blood pressure au Msongo wa mawazo(Anxiety).. Kama Hospital watasema hakuna shida kwa upande wa kiafya basi inawezekana haya yamesababishwa na nguvu za giza. Ni vizuri ukaingia kwenye maombi, ikiwezekana nenda kwa Mwamposa au Kuhani Musa.
 
ENDELEA KUMTUMAINIA MUNGU IKIWA UMEJIBWETEKA HAPO KWA MAOMBI.....HUJISHUGHULISHI NA TIBA...VIKIANZA KUTEMBEA KICHWANI UJUE TUNAKUKAMATA TUNAKUTIA KAMBA, SHWAAAAH MILEMBE HII HAPA😁😁😁
 
Kafanye evaluation ya maumbile ya seli zako za damu.. pima na kiwango cha vitamin B mwilini mwako..
 
Back
Top Bottom