Vitu vilivyotupotezea muda darasani, wakati wenzetu wachina wanavumbua mambo muhimu kwenye teknoloji

PAGAN

JF-Expert Member
Aug 19, 2014
11,852
19,466
adultlabelled.gif
 
ni kweli mkuu,kama hii mada ya kumkaririsha mwanafunzi sehem za panzi, somo hili linakuwa na faida gan???

Mmmhhhhhh Sina hakika. Pale unachopata ni knowledge. Na hamsomi huyo panzi muda wote. Ukifika nadhani form III unaweza kuendelea na Biology au ukachukua Arts na kadhalika. Halafu kuna shule za vipaji na sijui zimeishia wapi kama Kilakala, Mzumbe na Msalato.
 
Elimu ina umuhimu pale Elimu inapotumika.

Huwezi kusema ayo mambo yalikupotezea mda au hayana faida wakati elimu au ufahamu ulioupata kwa kusoma hizo sehemu za mwili wa panzi hujazitumia katika maisha yako....

ila kuna watu wanaona faida yake kwasababu walichokipata kwa kusoma hizo parts za panzi kimewasaidia au kiliwapa motisha ya kutaka kujua zaidi kuhusiana na uyo mdudu na pengine leo hii wanaitumia iyo elimu na wanaona umuhimu wake...
 
sijui ni ili baadae uje kuwa daktari wa panzi afadhali mi sikwenda hata chekechea lakini najua kusoma na kuandika na nanufaika na elimu yangu
 
elimu ya viumbe vidogo kama panzi ni primary source ya utambuzi wa elimu ya
vitu vikubwa kimfumo kama binadamu n.k.

ndio maana kwa madaktari wanafunzi kama wakiweza angalau kumfanzia kiumbe
ndogo kama mende,panya n.k huko mbeleni wanaweza kufanya mambo makubwa
zaidi.

Masomo ya sayansi kwa awali huwa ni kama kujifunza ujinga fulani na kupoteza muda
lakini ndivyo wanavyofanya hata kwenye operation kubwa kubwa,kwa madaktari bingwa
upasuaji ufanyika kimzaha mzaha tu lakini kwa umakini mkubwa.

Hata hao wachina nao walianzia huko,kwa ufupi ni kuwa 1+1=2 ina maana kubwa sana
katika maisha (akiba,bidii,umoja,chachu,utawala,maarifa na ubunifu n.k)
 
kwani katika maisha ya kila siku ya mgumu ana apply nini katika hizo sehemu hapo juu?
 
Hii kama wewe sio daktari au mambo ya viumbe utaona kupoteza muda. Ni sawa na daktari umuulize mwaka wa sultan Said Said kuhamia Zanzibar inamsaidia nn
 
Hapo hakuna elimu yoyote zaidi ya lugha! Elimu yetu ina mambo mawili kwanza ujifunze lugha ya kiingereza then uje ujifunze mada yenyewe. Mfano mtoto yeyote ukimuuliza sehemu za panzi kwa kiswahili kwan atashindwa?
 
Back
Top Bottom