Vitu gani vinakuvutia kutoka mkoa wa Morogoro (Mji kasoro Bahari)?

Zero IQ

JF-Expert Member
Dec 21, 2016
13,917
24,674
Kama wewe ni mkazi wa Morogoro au umeshawahi kupitia hapo mkoani sema hapa kitu gani ambacho kilikuvutia au umekifeel sana kutoka mkoani Morogoro.

Na mliopo Morogoro kama nyumbani tukutane hapa ili tuweze kupeana update mbalimbali za matukio ya mkoani kwetu Morogoro.

c8665da1765362ff64d1ae77558614ef.jpg
 
Tuna stand mpya ya kisasa ya mkoa, af wamachinga wameruhusiwa kuuza na kupanga bidhaa zao popote ndani ya stand, wasibughuziwe!

Update nyingine, St peters seminary Morogoro udumu milele, nikikutana na mkono wangu wa kuume na ukatike!!!
 
Maisha yangu ya utoto mpaka miaka 20 nimeitumia moro.Naipenda moro,shule ya msingi kiwanja cha ndege na sekondari Kigurunyembe,i miss Bahati camp,Rock garden,Tangeni,SUA kuogesha mbwa,shamba liti pale shule ya mji mkuu@naskia sasa ni hotel Nashera.Bahari yetu ya Mindu,jumapili mnadani sabasaba,Morogoro hotel,savoy,kwa mama pierina,mango garden,.mapumbani kuruka sarakasi,miss father kanute brass band,Dah kweli Happy days never return..ntarudi MORO.
 
Kama wewe ni mkazi wa Morogoro au umeshawahi kupitia hapo mkoani sema hapa kitu gani ambacho kilikuvutia au umekifeel sana kutoka mkoani Morogoro.

Na mliopo morogoro kama Nyumbani tukutane hapa ili tuweze kupeana Update mbalimbali za matukio ya mkoani kwetu Morogoro.

c8665da1765362ff64d1ae77558614ef.jpg
Nifeel hili jengo lipo site za stand ya mabus... lipo vzur sana kwa jinsi lilivyojengwa aiseeH
 
Maisha yangu ya utoto mpaka miaka 20 nimeitumia moro.Naipenda moro,shule ya msingi kiwanja cha ndege na sekondari Kigurunyembe,i miss Bahati camp,Rock garden,Tangeni,SUA kuogesha mbwa,shamba liti pale shule ya mji mkuu@naskia sasa ni hotel Nashera.Bahari yetu ya Mindu,jumapili mnadani sabasaba,Morogoro hotel,savoy,kwa mama pierina,mango garden,.mapumbani kuruka sarakasi,miss father kanute brass band,Dah kweli Happy days never return..ntarudi MORO.

Mjimkuu ipo.bado vile vile ila opposite yake kwenye like shamba LA kilimo ndiyo hiyo Nashera ipo. Mjimkuu chama LA wana.
 
Tuna stand mpya ya kisasa ya mkoa, af wamachinga wameruhusiwa kuuza na kupanga bidhaa zao popote ndani ya stand, wasibughuziwe!

Update nyingine, St peters seminary Morogoro udumu milele, nikikutana na mkono wangu wa kuume na ukatike!!!

Hovyooo, hiyo st. Peters mmejazana waluguru tu na ukabila umewajaa, yaan niliyokuwa hapo niliomba nimalize haraka niondoke hapo, ilikuwa sehemu ya ovyo mno na ndoto za upadre nilizizika hapo st. peters.
 
Napendekeza kuwa ile njia ya kuingilia stand ingebadilishwa ndiyo iwe ya kutokea na ile ya kutokea ndiyo iwe ya kuingilia ili magari yote yanayoingia stand yawe yanapita upande ambao ndiko stand iko kwasababu ya kupunguza foleni kwa magari yanayo cross zile lanes either yanapotoka stand kwenda barabara ya Morogoro - iringa na Dodoma au yanapotoka mikoa ya kusini na kuingia stand hiyo kuu.
  • Wazo ni kwamba, magari yanayotoka Dar yazunguke mzunguko na kuelekea pale yanapotokea mabasi kwa sasa ili kutozuia lane nyingine kama inavyotokea sasa wakati mabasi yanapotoka kuelekea mjini Morogoro, Iringa, Mbeya, Ruvuma nk yanalazimika kuzuia magari yanayotoka Dodoma, Iringa na kwingineko yasitumie lane ya Moro - Dar na kuzuia mabari yatokayo Dar na kuingia stand na kuelekea kwingineko
  • Pili kama mabasi yatatokea pale ambapo yanaingilia kwa sasa, ina maana hakutakuwa na haja ya magari yaendayo Dodoma kuzuiwa mpaka mabasi yanayotakiwa kuingia stand yaishe kuingia na pia hayatayazuia magari yatokayo Dodoma - Morogoro lane kusimama.
Kwa lugha rahisi utaratibu ufanywe kinyume chake na ikiwezekana ile lane ya Dodoma - Dar ipanuliwe kuelekea upande wa stand kiasi kidogo tu ili kutoa nafasi kwa magari mengine kuzunguka round about kirahisi.

Samahani mimi si mchoraji lakini nimejaribu kuchora kuonesha ninachoshauri, hivyo vimishale vinaonesha namna magari ya kuingia stand kutokea Dar, Mjini, Iringa na Dodoma yatakavyozunguka na kuignia stand na kutoka yakiwa upande mmoja wa kushoto wa barabara bila kuathiri magari yasiyokuwa na lengo la kuingia stand.

Wataalamu wa mambo ya michoro mtasaidia kufafanua hoja, yote ni kwa lengo la kujenga na siyo kukosoa endapo itaonekana hoja yangu imetazamwa kwa mtazamo wa kukosoa
 
Attachments

  • Mzamvu Document.pdf
    712.1 KB · Views: 84
Back
Top Bottom