Nimekuwa na mawazo yangu, lakini kwa sasa nataka kuyaweka in reality, nataka kufungua kampuni hapa tanzania ila sijui pa kuanzia, sijui natakiwa kuwa na vitu gani ili niweze kufungua iyo kampuni. Wataalamu au wenye uzoefu naombeni msaada wenu
Mkuu hapo juu ameleza vizuri sana.Ila tatizo utamaliza soli za viatu..sababu hata kusearch jina kwenye website yao haitasaidia sbabu database haiko updated nafikiri kwa makusudi ,na ukifuate utaratibu wa pale ofisini kwao sijui kujaza fomu nk utakesha...cha kufanya waone wataalamu ya mambo hayo amabo wanajua jinsi ya ku fast track the process....documents ni zilezile zenyewe ila mbinu tu tofauti...kama ukihitaji service hiyo ni pmNaam mkuu C6 ili uweze kufungua kampuni unatakiwa uwe na vitu vifuatavyo:
- Kwanza kabisa unatakiwa uwe na jina la kampuni ambalo unataka kulitumia...ukishalipata nenda BRELA kuhakikisha kama limeshachukuliwa na mtu au la...kama bado unaweza kulilipia ili lisichukuliwe.
- Baada ya hapo utatakiwa kuandaa document ambayo inaitwa Memorandum and The Articles of Association ambayo inaelezea kwa kina kuhusu shughuli ambavyo ziatafanywa na kampuni na namna ambavyo kampuni yako itaendeshwa. Kazi hii hufanywa na wanasheria japo siku hizi kuna watu wa kawaida ambao wanaweza kuandika hii document.
- Baada ya kumaliza kuandika hii document utaenda BRELA kuchukua fomu kuijaza na kulipia malipo yote yanayotakiwa then utapewa muda wa kusubiri na siku ambayo utatakiwa kwenda kuchukua Certificate of Incorporation.
- Baada ya kumalizana na registration kabla ya kampuni kuanza kufanya kazi lazima uwe na leseni na TIN number. Unaanza kwanza kwenda kuchukua TIN TRA ambayo inatolewa bure japo kuipata ni mbinde hadi utoe kitu kidogo then ukishapata hiyo TIN number unaenda manispaa kuchukua leseni yako ambayo nayo pia ina gharama zake.
- Ukishamaliza hayo yote then kampuni yako inaweza ku-operate.
Nimekuwa na mawazo yangu, lakini kwa sasa nataka kuyaweka in reality, nataka kufungua kampuni hapa tanzania ila sijui pa kuanzia, sijui natakiwa kuwa na vitu gani ili niweze kufungua iyo kampuni. Wataalamu au wenye uzoefu naombeni msaada wenu