Vitu 10 vinavyomfanya mwanamke apate heshima katika jamii

Vitu 10 vinavyomfanya mwanamke apate heshima katika jamii

Usher-smith MD

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2015
Posts
9,576
Reaction score
12,375
1.Kuwa mama

Mwanamke anaweza akawa na kila kitu duniani, ila kama hajazaa mtoto, sio tu jamii iyomzunguka hata yeye mwenyewe atajiona kuna kitu amekikosa.
Mama ndio nguzo ya familia, kaya, taifa na dunia kwa ujumla. Mama anaheshimika duniani kote. Watoto wanawapenda na kuwaheshimu mama zao.
Sawa, kuna baadhi ya kina mama wanazingua ila wengi wetu tupo tulipofikia kwa sababu mama zetu walipambana, kwa asilimia kubwa baba wanakuwa wazinguaji katika familia.

2.Ndoa

Mwanamke mwenye mume anaheshimika na kila mtu.
Hilo lipo toka enzi na enzi, hata wanawake walio katika ndoa wanajua kuwa urafiki na shosti asiye na mume ni hatari, hawachelewi kupindua meli. Mwanamke hata uwe na cheo cha uwaziri mkuu kama huna mume usistuke siku mlinzi wako akakupiga mistari.

3.Ajira / Kujiajiri / Anayejishughulisha

Wakati wa sasa katika maisha ni kusaidia, zamani ilikuwa jambo la kawaida mume kumwachisha mke kazi ili alee familia. Nyakati zimebadilika mwanamke mwenye ajira au mwenye kujishughulisha anaheshimika na kila rika. Na Wanaume tunazingatia hilo katika kutafuta mke.

4.Mali

Mwanamke mwenye Mali hanyanyasiki katika jamii, na mwanaume marioo ndio wanaowapenda wanawake mwenye Mali, maana ni kitonga kina raha yake.
Pia mume huwa na uhakika kuwa hata asipokuwepo watoto hawatoteseka na umasikini.

5.Elimu / Cheo

Mwanamke mwenye elimu anakuwa na kujiamini katika jambo lolote, ingawa kuwa na elimu isimfanye udharau watu wengine. Elimu inampa mwanamke uelewa mpana wa maisha, jamii , sheria na jinsi mambo yanavyotakiwa kuwa.
Cheo ni fursa ya kumsaidia mwanamke katika maamuzi ya kuuongozi na kuleta maendeleo katika jamii.

6.Usafi

Mwanamke msafi anapendwa sio na mume wake tu hata na majirani zake hasa kwenye nyumba za kupanga. Usafi uleta afya na kupunguza magonjwa.

7.Mwenye mahusiano mazuri na wazazi wake

Kama mwanamke haeshimu wazazi wake usitegemee aje haeshimu wakwe zake. Kama unatafuta mke zingatia hili.

8.Ukweli, ukarimu, heshima na Hekima

Mwanamke mkweli upendwa na kila mtu, asiwe na kisirani, gubu. Aheshimu kila mtu, mavazi ya heshima, kutoposti vitu vya ndani na picha zisizo na staha mitandaoni, mwanamke mwongo na asiye na hekima hata mambo ya chumbani atayaweka hadharani (mfano : mume wangu ana kiba100)

9.Asiwe mmbea

Mwanamke anayealika ngoma na matarumbeta kwenda kusuta watu huwa anaogopeka sana, na sidhani kama wanaume wengi wanapenda mwanamke wa aina hiyo.

10.Urembo / Msambwanda

Mwanamke mrembo atapata fursa nyingi katika jamii, ajira kama mwanamitindo, "TV presenter", "Receptionist", "Flight attendant".
Ajira nyingi vigezo vya chini ya kapeti ni urembo, tena ukikutana na bosi mwanaume, wakati kuchagua kati ya wanawake wawili kwenye vigezo na sifa sawa kitaaluma, mwanamke mrembo ana nafasi kubwa ya kupata hiyo ajira.
Msambwanda ni asili ya mwanamke wa kiafrika. Mwanamke akiwa na wowowo anaongeza "attention" kila apitapo, idadi wanaume wa kumposa ni kubwa kuliko kawaida.
Kuna imani kuwa mwanamke mwenye nyonga kubwa anazaa watoto wenye afya.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo namba 10 hapo umepiga mule mule. Hayo mengine mi simo [emoji16][emoji16][emoji16][emoji2099][emoji2099][emoji2099]
57100278-a80b-4b90-a7e7-f2b458333e7f.jpg
 
Back
Top Bottom