Vitisho mgomo wa walimu vyazidi.

Olesambai

Member
Jul 31, 2012
39
4
Baada ya mahakama ya kazi kushindwa kutoa hukumu hadi Agosti 2, vitisho kutoka kwa wakuu wa mikoa na polisi vinazidi. Huku Arusha polisi wamesema wataanza kupita mashuleni kubaini walimu wasiohudhuria shule na kuwasaka eti wao ndiyo wanaowatisha wale wasaliti wachache ambao wanategemea migongo ya wanaogoma kana kwamba wao wanalipwa tofauti. Kana kwamba hiyo haitoshi serikali imetoa fomu ya walimu kujaza kukubali kugoma au kuendelea na kazi. Hapa udhaifu wa serikali unazidi kuonekana. Hao wanaohojiwa kwenye redio hasa TBC si walimu ila ni mbinu za kuwatisha walimu. Mgomo utaendelea hadi kieleweke! Hao wanaosekana kuhudhuria si kwamba wanafundisha ila wanajipendekeza wachaguliwe kusimamia sensa. Na hata hivyo hawawezi kufundisha masomo yasiyo yao. Yawezekana hawa ndio wale vihio wanaotumia vyeti bandia au za ndugu zao na wanataka wasijulikane.
 
Nimemdharau Ndikilo Rc mwanza..anaongea kimikwara kama tupo BENGHAZI.WALIMU WANADAI HAKI.
 
Jambo hili liko mahakamani. Kwa nini watoe vitisho? Mgomo huu una baraka za kisheria. Hongereni waalim, msibabaike.
 
Ni kujidhalilisha kutoa vitisho alafu unaempe hivyo vitisho asitishike na mtoa vitisho kushindwa kutoa adhabu yoyote
 
Vitisho ndio kazi ya maRC na maDC kwani kimsingi hawana kazi nyengine yoyote ya maana ya kufanya.
Kama vichwa vyao bado vinaclick waingie madarasani wakate nyanga!
 
Si waamue tu kuwa wajasiriamali kimoja kuliko kufanya kazi kwa kinyongo na kusababisha wanafunzi kumaliza darasa la saba bila kujua kusoma wala kuandika. Hakuna haja ya kuwa na walimu wengi wasiowajibika. Serikali ifukuze hao wagomaji na wale wasiogoma iwalipe mishahara mara dufu
 
Kama kesi ipo mahakamani,serikali inahaha kwa nini? Si iachie mahakama! Kila mtu atahukumiwa kwa kuvunja sheria! Kama walimu wanavunja sheria,basi aliyetangaza mgom,mwl. Mkoba atashtakiwa kwa uchochezi! Mabavu hayasaidii,serikali gani hii?
 
Hakuna kurudi nyuma liwalo na liwe hawa wanaozawadiwa vyeo siku zao zinahesabika kwenye katiba mpya tunapiga chini wote hawana kazi yoyote ndomaana wanakurupuka tu...Hiyo mivx wanayoitumia hizo pesa zingepelekwa kwenye haya madai ya msingi ya walimu nani angegoma!!Ndio maana Wenje aliwatolea uvivu pale Bungeni kwakuwachana mlivyokuwa mmejiachia kwenye viyoyozi mjengoni.
 
Si waamue tu kuwa wajasiriamali kimoja kuliko kufanya kazi kwa kinyongo na kusababisha wanafunzi kumaliza darasa la saba bila kujua kusoma wala kuandika. Hakuna haja ya kuwa na walimu wengi wasiowajibika. Serikali ifukuze hao wagomaji na wale wasiogoma iwalipe mishahara mara dufu

da! We ni bonge la "kichwa" mkuu. Ukiona mtu hajiamini wala haamini juu ya utetezi wa haki yake, ujue na tatitzo kichwani.
 
Kawambwa hivi akilizake ni timamu? Anasema cwt wametumia vibaya sheria ya ajira ya mwaka 2004 na kwamba tafsiri hyo ya sheria ni ndogo. Kisheria wanasheria au mahakama ndio hutafsiri sheria. Kawambwa nikuulize tangu lini umeanza kuwa mwanasheria? Usitutibue tukamshinikiza jakaya hutaamini utakavyorud kijijini. Nahuko tukaweke mpinzani akutoe, utabaki kuwa balozi wa nyumba kumi. Take care.
 
vyeo vya kuongwa vinamatatizo sana, sasa mahakama yenyewe imeona hakuna kosa mpaka sasa wao wanaendeleza wimbo wa vitisho na wanakiuka mahakama kwani suaka lipo huko wao tayari watoa hkumu,mfano yule muuza sura wa dar mpaka aibu
 
mpango ni kukataa kusign form au chochote toka serikalin,waelimishe na walimu wenzako,chama cha walimu kitajibia au kujaza form wao ndio muongozo we2.
 
wanaanzia wapi kushika walimu!? Nataman kukutana nao chochoro na huku hakuna mabwepande
 
Serikali wanaingilia mhimili mwingine.
.suala liko mahakamani polisi na serikali wanahaha nini?
Watulie kimya kama wananyolewa viyisho vitisho mpaka lini?
Hapa halmashauri ya Arusha V.
Afisa (E) anatuma sms kwa HMs kuwatisha eti watapita kuchukua rekodi za mahudhurio!
Anaitwa Nasoro cku zote hapiti kwa sababu ya mgomo tuuu!?
Walimu mgomo mbele mbele mpaka kieleweke!
DEOs nyamazeni suala c liko Mahakamani?
 
Laizer Ole Naibio, tatizo ni kwamba wanaofundisha sasa hivi ni wale wenye uwezo mdogo. Hivyo maoni yako maana yake wafeli zaidi na selikari ikubali hali hiyo.
 
Baada ya mahakama ya kazi kushindwa kutoa hukumu hadi Agosti 2, vitisho kutoka kwa wakuu wa mikoa na polisi vinazidi. Huku Arusha polisi wamesema wataanza kupita mashuleni kubaini walimu wasiohudhuria shule na kuwasaka eti wao ndiyo wanaowatisha wale wasaliti wachache ambao wanategemea migongo ya wanaogoma kana kwamba wao wanalipwa tofauti. Kana kwamba hiyo haitoshi serikali imetoa fomu ya walimu kujaza kukubali kugoma au kuendelea na kazi. Hapa udhaifu wa serikali unazidi kuonekana. Hao wanaohojiwa kwenye redio hasa TBC si walimu ila ni mbinu za kuwatisha walimu. Mgomo utaendelea hadi kieleweke! Hao wanaosekana kuhudhuria si kwamba wanafundisha ila wanajipendekeza wachaguliwe kusimamia sensa. Na hata hivyo hawawezi kufundisha masomo yasiyo yao. Yawezekana hawa ndio wale vihio wanaotumia vyeti bandia au za ndugu zao na wanataka wasijulikane.

If they hurt my relatives who are teachers, I will also go after their relatives including their kids!! It is gonna be a real terrorism!!
 
Back
Top Bottom