Vitengo vya habari na mawasiliano msaidie katika hili.


Vitendo

Vitendo

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2009
Messages
603
Likes
11
Points
35
Vitendo

Vitendo

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2009
603 11 35
Habari za leo WanaJF.
Kumekuwa na ongezeko kubwa sana la watu kuulizia kama ofisi/kampuni/shirika fulani limeshaita watu kwenye usaili/interview au kazini kupitia JF,na majibu ambayo wamekuwa wakiyapata kati yake mengi ni ya kukatisha tamaa na yamekuwa yakionekana kuwa hayana uhakika yani sio ya ukweli.
Imani yangu ni kuwa JF ni sehemu ambayo ina watu wengi na wa kila aina,nina imani maafisa habari wengi wapo humu,maafisa waajiri na hata wakurugenzi mbalimbali.Ombi langu ni kuwa fanyeni vitengo vyenu vya Habari na mawasiliano kuwa kimbilio la watu hawa wanaotaka kujua kama usaili umefanyika au watu tayari wameitwa kuanza kazi.Mimi naamini ni rahisi na inawezekana kabisa.Kuweni wazi kwenye michakato ya ajira na mtoe taarifa za ukweli ili muweze kuwasaidia maelfu ya watanzania ambao wanatafuta sehemu za kufanyia kazi.
asante.
 

Forum statistics

Threads 1,215,128
Members 463,036
Posts 28,536,807