Vitendo vya wizi maeneo ya Mlimani City Dar es Salaam Tanzania

Come27

JF-Expert Member
Dec 1, 2012
7,503
7,107
Habari za siku ya leo, kwanza poleni kwa mapumziko ya weekend,

Naomba tujadili vitendo vya wizi maeneo makubwa ya kibiashara kama apa Mlimani City na maeneo ya Magomeni NMB bank.

Kumekuwepo na vitendo vya ukiingia bank za hapo Mlimani city kunakuwa na watu wanakufatilia mpaka utakapotoka na kama ukiingia kwenye maeneo ya Parking ya Mlimani City karibia na barabarani uwezekano wa kutolewa Bastola ni mkubwa sana, na wezi wengi wanakuwa wamepaki gari ya Noah kama watu wengineo uwezi kumtambua na maeneo ya pale Mlimani City karibia wengi wanajulikana mpaka kwa wale walinzi wa Mlimani City.

Na kuhusu ishu ya walinzi uwenda wakawa wana husika nao kwasababu jioni ikishafika pale Mlimani City kunakuwa na machangudoa wanajiuza maeneo ya parking ya magari kama wateja. Sasa pale serikali inaboresha vip? Ulinzi kwa watu wanaofika pale kuchukua pesa.

Na kwa upande wa Magomeni Usalama maeneo ya NMB bank. Kuna vitendo vya wizi sana, unamaliza kutoa pesa bank unatoka na mwizi ndani ya bank mule mule, hivi katika hizi Taasisi zinashindwa kuboresha ulinzi katika sehemu zao za kazi.
 
Duh! Hatari sana, nina imani humu kuna wanausalama watajaribu kulitafutia ufumbuzi hilo tatizo.
 
Kama mwizi anakupigia timing atakupata tu.

Haijalishi ni wapi na Kuna ulinzi gani
 
Hivi bado kuna watu wanaenda benki kuchukua rundo la hela katika zama hizi?
 
Hivi bado kuna watu wanaenda benki kuchukua rundo la hela katika zama hizi?
Rundo la pesa ni kiasi gani?mkuu hela yetu haina thamani,kununua kitu kidogo tu,inahitaji pesa mingi

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Kwani hukuona polisi we so unamihela mingi hadi ya kuweka pembeni gari ikisumbua...acha kutujazia server zetu Keleler nyingi utadhan baada ya kuandika hv hayo wezi watajikamatisha
 
benk huwa hazitakiwa kwenye mazingira ya watu wengi lakini pale mlimani city ndo kuna kila kitu
 
Watu wa Dar poleni sana...shida moja hao walinzi wanajuana na hao wezi
Natafuta justification ya wewe kuandika hii comment halafu siioni.

Unamaanisha Dar peke yake ndiyo kuna benki, ATM, parking na wezi au?
 
Back
Top Bottom