Vitendo SACCOS - kukopeshana bila riba

Mna
Kama nilivyoahidi katika post yangu hii: Fursa ya kuwekeza kwa msingi mdogo kuwa tutafungua mjadala kujadili vipi tunaweza kuanzisha mpango wa kukopa / kukopesha / kuwekeza bila riba.

Duniani kwa sasa kumekuwa na wengi wanaousikia na wengineo wameshaanza kuutumia mpango wa "islamic Banking", lakini si wengi wanaoufahamu unafanyaje kazi ili kuhakikisha unakopa unakopesha na kuwekeza bila kutoa au kupokea riba.

Mpango wa "Islamic Banking" kwa sasa kwa hapa kwetu Tanzania unafanyika kwa njia za benki kubwa kubwa tu na hatujaona ukihusisha vikundi vidogo vya kukopa na kuwekeza kwa njia hiyo isiyokuwa na riba.

Njia sahihi za kukopeshana bila riba zinawezekana kwa vikundi vidogo vidogo na havihitaji ulazima wa kufanya hivyo kupitia benki ambako huwa kuna milolongo na ukiritimba wa hapa na pale.

Mfumo wa "Islamic Banking" umekuwa ni biashara kubwa sana nje ya nchi za Kiislam na haumaanishi kuwa ni Waislam tu wanaoweza kushiriki. Mfumo huu ni kwa yeyote.

Nafungua mjadala huu kwa lengo la kuanzisha kikundi kitakacho anzisha mpango huu rasmi kwa faida ya wengi.

Yeyote anaehisi kuwa anaufahamu au atapenda kushiriki katika mpango huu kuanzia awali anaweza kuwasiliana nami kwa PM au kwa whatsapp 0625249605.

Karibuni Tujadili.

UPDATE 1 (02-05-2017)

Wadau wote,
Ninapenda kuwafahamisha kuwa jana tarehe 1-5-2017 tulikuwa na kikao kuhusu kuanzishwa kwa SACCOS yetu mpya.

Wahudhuriaji walikuwa wa kutosha. Kati yao walikuwepo (wengi wao) ambao ni wawekezaji tayari katika miradi yetu ya awali (nje ya SACCOS tarajiwa), wengine ni wawekezaji watarajiwa. Pia tulimualika Mwenyekiti wa serikali yetu ya mtaa wa Vitendo, ndugu Salehe Dibebile, tulimualika pia na Katibu wa vyama vya ushirika vya kata ya Misugusugu bwana Kussi. Pia tulikuwa na wawekezaji wawili ambao tayari wana miradi yao (nje na yetu) ya machimbo ya michanga.

Kwa kifupi, tulitambulishana, tukajadili ushirika tunaoufikiria na tukakubaliana (bila kuwa na hoja za kupingana). Hoja zilizotamalaki zilikuwa ni za kupeana elimu zaidi ya ushirika na faida zake...

Ikaamuliwa tuuanzishe ushirika haraka iwezekanavyo...

Ikaamuliwa tuanze kwa kukusanya masharti ya saccos tofauti na samples zake, members wote wapitie ili tuweze kuwa na SACCOS yetu tarajiwa haraka iwezekanavyo...

Imeamuliwa pia Abdul Ghafur awe Mwenyekiti wa muda mpaka ushirika wetu utakapo sajiliwa ndiyo kutakapokuwa na masharti ya uchaguzi rasmi. Watakaojiunga wote watakuwa wajumbe mpaka hapo sheria na kanuni rasmi zitakapo patikana.

Pia Imeamuliwa kuanzia sasa kila atakaependa kujiunga kutakuwa na ada ya kiingilo itakayo saidia katika gharama za usajili na mpaka hapo tutapokuwa na masharti na kanuni zetu rasmi zilizopitishwa na wnahama wote kwa ujibu wa sheria...

Ushirika tutakaoanzisha utafata sheria na kanuni zote za nchi na sheria za vyama vya ushirika za Tanzania...

Ushirika hautakuwa na ukomo wa watakaojiunga mpka hapo itakapotangazwa rasmi baada ya kupata kanuni zilizokubalika na wanahama wote, kujiunga kutakuwa wazi kwa yeyote anaekubalika kisheria, awe popote Tanzania au duniani...

Ada ya kiingilo kwa sasa ni shillihgi 10,000 (elfu kumi) ambazo zitatumwa kwa Mwenyekiti wa muda kwa njia ya Mpesa. Namba ni 0756803528 jina Ghafur Abdallah Mohamed.

Mahesabu yote ya chama yatakuwa wazi kwa wanachama wote, kwa sasa yatapatikana kupitia group la whatsapp la waliojiunga.

Kila atakaelipa ataingizwa kwenye group mahususi la whatsapp litalokuwa kwa ajili ya wanachama tu waliojiunga katika ushirika wetu mpya.

Tumeanza kupokea ada za viingilio na hesabu zote zitapatikana kwenye group mpya ya wanachama walioingia kwa kulipia ada...

Uwe popote ulimwenguni unakaribishwa kujiunga kwa faida ya wote.

Group mpya imeshafunguliwa kwa jina la muda Vitendo SACCOS na members wawili waliolipia ada tayari tumepatikana, maelezo zaidi kwenye group mpya...

Ada ya kiingilo ni shillihgi 10,000 (elfu kumi) ambazo zitatumwa kwa Mwenyekiti wa muda kwa njia ya Mpesa. Namba ni 0756803528 jina Ghafur Abdallah Mohamed

Nawajulisha wote watakaotaka kujiunga muanze kwa kulipia ada ili tufanikishe usajili kwa haraka.

Ili kujiunga, (kwa sasa) inatakiwa utupatie jina kamili, namba za simu, email address na ulipo na utume 10,000 kwa Mpesa.

Tunakaribisha maswali.

Abdul
+255 625 249 605 (whatsapp)

Mna nia nzuri ila mmeanza vibaya.SACCOS ni jina linalopatikana baada ya kuandikishwa kwa mujibu wa sheria ya Vyama vya Ushirika Na.6 ya 2013.Pili hakuna cheo cha katibu wa Vyama vya Ushirika kwa mujibu wa sheria ya Vyama vya Ushirika.

Tatizo kubwa japo limesambaa si kwenu tu na wasimamizi wameruhusu kosa hili liedelee bila kuchukua hatua ni kitendo cha kuruhusu baadhi ya Vyama vya Ushirika kuanzishwa kwa misingi ya dini,madhehebu,Vyama vya siasa au makabila.

Mojawapo kati ya kanuni kuu za Vyama vya Ushirika Duniani ni uanachama wa wazi na wa hiari.Kuwa na vyama vinavyozingatia,dini,dhehebu,kabila au chama cha siasa ni kukiuka kanuni hii.

Ninawashauri kuwa wasilianeni na Afisa Ushirika wa Wilaya yako atakupa maelekezo sahihi ya uanzishaji wa SACCOS.

Kila la kheri.
 
Nimefurahi sana kwa maoni yako, naamini "criticism" yako ni kwa kututakia mema.

1) Hatuwezi "kuandikishwa kwa mujibu wa sheria..." kama hatuna jina na na hilo ndio jina letu tulilojichagulia "Vitendo SACCOS".

2) Hilo la vyama vya ushirika kuwa vya "dini" hatutakuwa nalo kwetu. Bali tutafata misingi ya undeshaji biashara na kukopeshana bila kutoa riba kwa mujibu wa Islamic Finance and Banking sharia. Mfumo ambao kwa sasa unakubalika duniani kote na unafanya vizuri sana hata katika nchi kubwa za Kimagharibi na ni vyema sana kuwa hata hapa kwetu upo na unatumika rasmi sasa hivi.

3) Asante kwa ushauri wa kuwasiliana na "Afisa Ushirika wa Wilaya", mwana JF CHIKIRA MTABARI hapo juu kidogo kwenye post namba 151 katushauri vivyo hivyo na zaidi kidogo, tumekubaliana na ushauri wake na huu wako kwa 100%. Tutafanya hivyo.

Tunakukaribisha sana ujiunge nasi kwa faida ya wengi, tunapenda vichwa vinavyochangamsha na si vile vya "Yes Sir" pekee.
 
Nafikiri una changamoto ya kujua taratibu za utoaji wa mikopo. Nakuahairi tembelea ofisi za saccos wakupe maelekezo ya namna ya utoaji mikopo usikurupuke. Tena mbali zaidi hata maana yenyewe ya neno saccos hujui
 
Tungefurahi sana ungejiunga nasi ili utuelimishe, tunahitaji sana watu kama wewe wenye uelewa wa kuelewa kuwa sisi hatuijui "maana yenyewe ya neno saccos". Ninakuhakikishia, sisi hatujui kweli na tungependa uje kutuelewesha kwenye ushirika wetu, tupo tayari kulipia mafunzo yako utakayotupa, mradi uhakikishe una course materials zinazoeleweka.

Karibu sana.

Whatsapp 0625249605
 
Mnanifurahisha sana mnavyojibu professionally. Lazima aingie mitini.
 
Nimesoma maelezo yenu kwa kina nimeshawishika. Hata kama mimi sitanufaika lakini naamini kuna mtanzania mwenzangu atanufaika kwa mimi kujiunga kwenye hii SACCOS, count me inn. Ungetupa uratibu kwa walio nje na Tanzania wanajiungaje? Asante.
 
Nimeona watu wawili kutoka nje wametumia Money Transfer - Send Money Online | WorldRemit na zimefika.

Unatuma 10,000 kwa namba +255756803528 Jina litatoka Mohamed Abdallah.

Nakushukuru sana kwa wazo lako jema, ninauhakika hata wewe utafaidika sana. Kwa kuwa upo China kuna vitu vingi tumeanza kuulizia kutoka huko, kwa uenyeji wako unaweza ukawa ndio macho ya SACCOS yetu mpya huko. Tukishakuunga nitakupa majina ya vitu ambavyo SACCOS inaviulizia huko.
 
Huu mfumo nausoma tuu kwenye matangazo siufahamu .....ningependa kushiriki kujifunza.

Sasa tumeanza rasmi kujiunga na kuunda ushirika wetu utaofata mfumo wa Islamic Finance.

Karibu ujiunge nasi kuunda ushirika wa kipekee Tanzania.
 
Nimeona watu wawili kutoka nje wametumia Money Transfer - Send Money Online | WorldRemit na zimefika.

Unatuma 10,000 kwa namba +255756803528 Jina litatoka Mohamed Abdallah.

Nakushukuru sana kwa wazo lako jema, ninauhakika hata wewe utafaidika sana. Kwa kuwa upo China kuna vitu vingi tumeanza kuulizia kutoka huko, kwa uenyeji wako unaweza ukawa ndio macho ya SACCOS yetu mpya huko. Tukishakuunga nitakupa majina ya vitu ambavyo SACCOS inaviulizia huko.
okay. Ngoja niangalie uwezekano wa kutuma kwa hiyo service sijawahi kuitumia kabda.
 
Back
Top Bottom