Vitendo SACCOS - kukopeshana bila riba

Zainab Tamim

JF-Expert Member
Jan 15, 2015
1,293
578
Kama nilivyoahidi katika post yangu hii: Fursa ya kuwekeza kwa msingi mdogo kuwa tutafungua mjadala kujadili vipi tunaweza kuanzisha mpango wa kukopa / kukopesha / kuwekeza bila riba.

Duniani kwa sasa kumekuwa na wengi wanaousikia na wengineo wameshaanza kuutumia mpango wa "islamic Banking", lakini si wengi wanaoufahamu unafanyaje kazi ili kuhakikisha unakopa unakopesha na kuwekeza bila kutoa au kupokea riba.

Mpango wa "Islamic Banking" kwa sasa kwa hapa kwetu Tanzania unafanyika kwa njia za benki kubwa kubwa tu na hatujaona ukihusisha vikundi vidogo vya kukopa na kuwekeza kwa njia hiyo isiyokuwa na riba.

Njia sahihi za kukopeshana bila riba zinawezekana kwa vikundi vidogo vidogo na havihitaji ulazima wa kufanya hivyo kupitia benki ambako huwa kuna milolongo na ukiritimba wa hapa na pale.

Mfumo wa "Islamic Banking" umekuwa ni biashara kubwa sana nje ya nchi za Kiislam na haumaanishi kuwa ni Waislam tu wanaoweza kushiriki. Mfumo huu ni kwa yeyote.

Nafungua mjadala huu kwa lengo la kuanzisha kikundi kitakacho anzisha mpango huu rasmi kwa faida ya wengi.

Yeyote anaehisi kuwa anaufahamu au atapenda kushiriki katika mpango huu kuanzia awali anaweza kuwasiliana nami kwa PM au kwa whatsapp 0625249605.

Karibuni Tujadili.

UPDATE 1 (02-05-2017)

Wadau wote,
Ninapenda kuwafahamisha kuwa jana tarehe 1-5-2017 tulikuwa na kikao kuhusu kuanzishwa kwa SACCOS yetu mpya.

Wahudhuriaji walikuwa wa kutosha. Kati yao walikuwepo (wengi wao) ambao ni wawekezaji tayari katika miradi yetu ya awali (nje ya SACCOS tarajiwa), wengine ni wawekezaji watarajiwa. Pia tulimualika Mwenyekiti wa serikali yetu ya mtaa wa Vitendo, ndugu Salehe Dibebile, tulimualika pia na Katibu wa vyama vya ushirika vya kata ya Misugusugu bwana Kussi. Pia tulikuwa na wawekezaji wawili ambao tayari wana miradi yao (nje na yetu) ya machimbo ya michanga.

Kwa kifupi, tulitambulishana, tukajadili ushirika tunaoufikiria na tukakubaliana (bila kuwa na hoja za kupingana). Hoja zilizotamalaki zilikuwa ni za kupeana elimu zaidi ya ushirika na faida zake...

Ikaamuliwa tuuanzishe ushirika haraka iwezekanavyo...

Ikaamuliwa tuanze kwa kukusanya masharti ya saccos tofauti na samples zake, members wote wapitie ili tuweze kuwa na SACCOS yetu tarajiwa haraka iwezekanavyo...

Imeamuliwa pia Abdul Ghafur awe Mwenyekiti wa muda mpaka ushirika wetu utakapo sajiliwa ndiyo kutakapokuwa na masharti ya uchaguzi rasmi. Watakaojiunga wote watakuwa wajumbe mpaka hapo sheria na kanuni rasmi zitakapo patikana.

Pia Imeamuliwa kuanzia sasa kila atakaependa kujiunga kutakuwa na ada ya kiingilo itakayo saidia katika gharama za usajili na mpaka hapo tutapokuwa na masharti na kanuni zetu rasmi zilizopitishwa na wnahama wote kwa ujibu wa sheria...

Ushirika tutakaoanzisha utafata sheria na kanuni zote za nchi na sheria za vyama vya ushirika za Tanzania...

Ushirika hautakuwa na ukomo wa watakaojiunga mpka hapo itakapotangazwa rasmi baada ya kupata kanuni zilizokubalika na wanahama wote, kujiunga kutakuwa wazi kwa yeyote anaekubalika kisheria, awe popote Tanzania au duniani...

Ada ya kiingilo kwa sasa ni shillihgi 10,000 (elfu kumi) ambazo zitatumwa kwa Mwenyekiti wa muda kwa njia ya Mpesa. Namba ni 0756803528 jina Ghafur Abdallah Mohamed.

Mahesabu yote ya chama yatakuwa wazi kwa wanachama wote, kwa sasa yatapatikana kupitia group la whatsapp la waliojiunga.

Kila atakaelipa ataingizwa kwenye group mahususi la whatsapp litalokuwa kwa ajili ya wanachama tu waliojiunga katika ushirika wetu mpya.

Tumeanza kupokea ada za viingilio na hesabu zote zitapatikana kwenye group mpya ya wanachama walioingia kwa kulipia ada...

Uwe popote ulimwenguni unakaribishwa kujiunga kwa faida ya wote.

Group mpya imeshafunguliwa kwa jina la muda Vitendo SACCOS na members wawili waliolipia ada tayari tumepatikana, maelezo zaidi kwenye group mpya...

Ada ya kiingilo ni shillihgi 10,000 (elfu kumi) ambazo zitatumwa kwa Mwenyekiti wa muda kwa njia ya Mpesa. Namba ni 0756803528 jina Ghafur Abdallah Mohamed

Nawajulisha wote watakaotaka kujiunga muanze kwa kulipia ada ili tufanikishe usajili kwa haraka.

Ili kujiunga, (kwa sasa) inatakiwa utupatie jina kamili, namba za simu, email address na ulipo na utume 10,000 kwa Mpesa.

SACCOS ITAENDESHWA KWA KUFATA MFUMO WA ISLAMIC FINANCE AND BANKING SYSTEM.

Tunakaribisha maswali.

Abdul
+255 625 249 605 (whatsapp)
 
naomba nichangie kidogo kwa ninachokifahamu kuhusu huu mfumo,kwanza huu mfumo haukopeshwi pesa,Bali unaenda benk unasema unataka kufanya biashara gani? na wapi,na business plan yako ikoje,utapate faida, baada ya benk kukuelewa biashar yako harari, basi wanakununuli hiyo bidhaa popote pale unapopataka,kisha baada ya hapo,wanaukabidhi kwa makubaliano maalumu,kwamba kwenye huo mzigo ukiuza wao watakuwa wanapata faida ya asilimia ngapi na kwa mda gani, yaani kwa maananyingine mnagawana faida,kwa kipindi Fulani,baada hapo wanakuacha unaendelea na biashara yako,kwa upande mwingine ukipata hasara basi hamtagawana hasara,kwa muda huo,......nimechokoza wakuu,wengine wafunguke sasa
 
Safi sana ndugu Zainab, ni kweli mfumo wa ISLAMIC BANKING umekuwa ukiwanufaisha watu wengi hasa ktk nchi za kiislam, lakn pia mfumo huu n world wide kwa sasa na mtu wa dini yeyote anaruhusiwa. Mfumo wa IB wenyewe haukopesh pesa taslim ila unakuwezesha mbadala wa hitaji lako. Kwa ufupi haudili na riba ila upo commercially. Mfano, ww unataka unataka kufungua duka la simu na unahtaji mtaji, mtaingia makubaliona yaan maelewano then wanakunulia hicho unachotaka, wanakupa kwa makubaliano then unaenda kufanya biashara yako.
 
Hapo kidogo ninahisi hapajakaa sawa.
 
Kwa maana nyepesi watoaji wanakuwa ni "financiers" na mnaingia ubia.
 
Maelezo zaidi hasa jinsi ya kupata washiriki na masharti muhimu husoka

Kuna "pilot projects" aina mbili tulianza kuzifanya na muitikio umekuwa mzuri sana, tukawaza kwanini tusiende mbele zaidi na tufikie kwenye "financing" bila riba.

Katika kuchimbua kutafuta namna nyepesi ya kuweza kupata "financing" sijaiona iliyo bora zaidi ya hii "islamic Banking" au to be precise "Islamic Finance".

Kutazama hapa Tanzania nimeona kuwa hakuna "Islamic Finance" nje ya bank. Nimeona kuwa Tanzania kuna biashara kubwa sana imeibuka ya kukopa na kulipa (officially na unofficially) nikaona kuna fursa kubwa sana ikiwa tu tutakuja na mfumo wa kukopa/kukopesha/kuwekeza kwa aina ya "islamic Finance" kwa faida ya wengi.

Inawezekana, na ndio nimeleta huu mjadala hapa ili tubadilishane mawazo. Mawazo tunayobadilishana hapa yanaweza kuwa na chachu za kutazama lipi lifanyike lipi lisifanyike.
 
Mimi nazungumzia wale wanaosema mfumo wa Islamic Banking kwamba unakopeshwa bila riba,kama wewe unaenda benki kukopa pesa ufanye biashara wakakupatia mfano million 1 lakini wakataka ukirudisha urudishe million 1.1 na wale wa Islamic Banking wanakununulia bidhaa unayotaka kwa kiwango kile kile kisha wakakukopesha ila ukilipa ulipe na nyongeza kidogo ndio nikasema yote ni yale yale.
Ndio Yale yale
 
Sio yale yale, ktk mfumo wa kiislamu mnaelewana wakt mifumo mingine unakuta mashart tayar. Pia mifumo mingne shart kubwa ni riba wakt huku hakuna riba.
 
naomba nichangie kidogo kwa ninachokifahamu kuhusu huu mfumo,kwanza huu mfumo haukopeshwi pesa,Bali unaenda benk unasema unataka kufanya biashara gani? na wapi,na business plan yako ikoje,utapate faida, baada ya benk kukuelewa biashar yako harari, basi wanakununuli hiyo bidhaa popote pale unapopataka,kisha baada ya hapo,wanaukabidhi kwa makubaliano maalumu,kwamba kwenye huo mzigo ukiuza wao watakuwa wanapata faida ya asilimia ngapi na kwa mda gani, yaani kwa maananyingine mnagawana faida,kwa kipindi Fulani,baada hapo wanakuacha unaendelea na biashara yako,kwa upande mwingine ukipata hasara basi hamtagawana hasara,kwa muda huo,......nimechokoza wakuu,wengine wafunguke sasa
na je lazima uweke dhamana? maana ukipata hasara wao wana recover vipi hasara yao? Mfano nahitaji mtaji wa operation kwa miezi sita. Ina maana watawalia wafanya kazi wangu kwa miezi na kupilipa bili zote kwa miezi sita? Hao huu mkupo ni kwenye rawa materials tu wao kukununulia?
 
Kuna "pilot projects" aina mbili tulianza kuzifanya na muitikio umekuwa mzuri sana, tukawaza kwanini tusiende mbele zaidi na tufikie kwenye "financing" bila riba.

Katika kuchimbua kutafuta namna nyepesi ya kuweza kupata "financing" sijaiona iliyo bora zaidi ya hii "islamic Banking" au to be precise "Islamic Finance".

Kutazama hapa Tanzania nimeona kuwa hakuna "Islamic Finance" nje ya bank. Nimeona kuwa Tanzania kuna biashara kubwa sana imeibuka ya kukopa na kulipa (officially na unofficially) nikaona kuna fursa kubwa sana ikiwa tu tutakuja na mfumo wa kukopa/kukopesha/kuwekeza kwa aina ya "islamic Finance" kwa faida ya wengi.

Inawezekana, na ndio nimeleta huu mjadala hapa ili tubadilishane mawazo. Mawazo tunayobadilishana hapa yanaweza kuwa na chachu za kutazama lipi lifanyike lipi lisifanyike.
Mkuu usiseme hakuna, zipo Mimi nazijua mbili ya kwangu na wamama flan hivi wameanzisha
 
Mkuu usiseme hakuna, zipo Mimi nazijua mbili ya kwangu na wamama flan hivi wameanzisha

Tusamehe sana kwa usemi wetu "hakuna", ni kutokuelewa kwetu. Tunafuta usemi huo.

Tunaomba sana tuwasiliane aidha hapa au kwenye whatsapp ili tuone namna tunavyoweza kushirikiana na kubadilishana uzoefu.
 
Back
Top Bottom