Roving Journalist JF Roving Journalist Joined Apr 18, 2017 Posts 5,201 Reaction score 15,546 May 18, 2020 #1 Vitate, Vitawe na Visawe VITATE, VITAWE NA VISAWEKitengoMsamiatiMASOMOPrevN/ANextTarakimu Baadhi ya maneno ya Kiswahili yanaweza kuwa na maana sawa, maana zaidi ya moja au matamshi yanayotatiza. Vikundi hivi vitatu ni: Vitate - maneno yanayotatiza kimatamshi. ⇒ '' Vitate hutatiza kimatamshi Vitawe - maneno yenye maana zaidi ya moja. ⇒ Vitawe hugawanywa kwa matawi au maana zaidi Visawe - maneno tofauti yenye maana sawa. ⇒ Visawe huwa na maanasawa Vitate Maneno yanayotatiza kimatamshi. ndoa na doa : ndoa ⇒ kuungana kwa watu wawili na kuishi pamoja kama mume na mke doa ⇒ alama ya uchafu, kasoro au dosari baba na papa : baba ⇒ mzazi wa kiume papa ⇒ mnyama wa baharini fua na vua : fua ⇒ osha nguo, tengeneza vyuma vua ⇒ shika samaki kutoka majini; toa nguo faa na vaa : faa ⇒ inayostahili, inayopaswa vaa ⇒ weka nguo juu ya mwili ngoma na goma : ngoma ⇒ ala ya muziki itoayo sauti inapopigwa goma ⇒ acha kufanya kazi shinda na shida : shinda ⇒ ongoza katika makabiliano, mashindano shida ⇒ taabu au matatizo shindano na sindano : shindano ⇒ makabiliano baina ya watu wawili au zaidi ili kutambua atakayeongoza sindano ⇒ kifaa kinachotumika kushonea vitu pinga na piga : pinga ⇒ kutokubaliana na jambo fulani piga ⇒ kugonga au kuchapa fahali na fahari : fahali ⇒ ng'ombe wa kiume. pia ndume fahari ⇒ kujivunia, furaha haba na hapa : haba ⇒ kisichokuwa kingi hapa ⇒ mahali karibu } Vitawe Mano yenye maana zaidi ya moja paa : kwea (enda juu) mnyama wa porini anayefanana na mbuzi sehemu ya juu ya nyumba shinda : kaa au ishi mahali/wakati fulani ongoza katika shindano tupu kaa : sehemu yenye moto ya kuni mnyama wa majini keti chini kuwa mahali fulani kwa muda mbuzi : mnyama anayefugwa kama ng'ombe chombo cha kukunia nazi mlango : ukoo au watu wenye asili smoja sehemu ya kuingia kwenye nyumba kitu kinachotumika kifunga nyumba fua : unda vyombo/vifaa mbalimbali kwa kupiga chuma osha nguo vua : toa nguo kutoka mwilini toa samaki kwenye maji kiboko : mnyama mkubwa wa baharini silaha inayotumika kwa kuchapa au kupiga tembo : aina ya ndovu aina ya pombe } Visawe Maneno tofauti yenye maana sawa. msichana au banati : ⇒ kijana wa jinsia ya kike mvulana au ghulamu : ⇒ kijana wa jinsia ya kiume huzuni au majonzi : ⇒ hali ya kilio na huruma mazishi au matanga : ⇒ shughuli za kumzika marehemu wakati au mwia : ⇒ wakati au muda mtu au mja : ⇒ mnyama atembeaye kwa miguu miwili mwenye uwezo wa kuongea na kufikiri kimantiki barua au waraka : ⇒ kartasi inayoandikwa na kutumwa ili kuwasilisha ujumbe fulani siri au faragha : ⇒ jambo lisilopaswa kujulikana na mtu mwengine macho au maninga : ⇒ sehemu za mwili zinazotumika kuangalia na kuona mwangaza au nuru : ⇒ miyale inayowezesha watu kuona vitu Mungu au Mola au Rabana au Jalali au Rabuka : ⇒ Majina ya Mwenyezi Mungu
Vitate, Vitawe na Visawe VITATE, VITAWE NA VISAWEKitengoMsamiatiMASOMOPrevN/ANextTarakimu Baadhi ya maneno ya Kiswahili yanaweza kuwa na maana sawa, maana zaidi ya moja au matamshi yanayotatiza. Vikundi hivi vitatu ni: Vitate - maneno yanayotatiza kimatamshi. ⇒ '' Vitate hutatiza kimatamshi Vitawe - maneno yenye maana zaidi ya moja. ⇒ Vitawe hugawanywa kwa matawi au maana zaidi Visawe - maneno tofauti yenye maana sawa. ⇒ Visawe huwa na maanasawa Vitate Maneno yanayotatiza kimatamshi. ndoa na doa : ndoa ⇒ kuungana kwa watu wawili na kuishi pamoja kama mume na mke doa ⇒ alama ya uchafu, kasoro au dosari baba na papa : baba ⇒ mzazi wa kiume papa ⇒ mnyama wa baharini fua na vua : fua ⇒ osha nguo, tengeneza vyuma vua ⇒ shika samaki kutoka majini; toa nguo faa na vaa : faa ⇒ inayostahili, inayopaswa vaa ⇒ weka nguo juu ya mwili ngoma na goma : ngoma ⇒ ala ya muziki itoayo sauti inapopigwa goma ⇒ acha kufanya kazi shinda na shida : shinda ⇒ ongoza katika makabiliano, mashindano shida ⇒ taabu au matatizo shindano na sindano : shindano ⇒ makabiliano baina ya watu wawili au zaidi ili kutambua atakayeongoza sindano ⇒ kifaa kinachotumika kushonea vitu pinga na piga : pinga ⇒ kutokubaliana na jambo fulani piga ⇒ kugonga au kuchapa fahali na fahari : fahali ⇒ ng'ombe wa kiume. pia ndume fahari ⇒ kujivunia, furaha haba na hapa : haba ⇒ kisichokuwa kingi hapa ⇒ mahali karibu } Vitawe Mano yenye maana zaidi ya moja paa : kwea (enda juu) mnyama wa porini anayefanana na mbuzi sehemu ya juu ya nyumba shinda : kaa au ishi mahali/wakati fulani ongoza katika shindano tupu kaa : sehemu yenye moto ya kuni mnyama wa majini keti chini kuwa mahali fulani kwa muda mbuzi : mnyama anayefugwa kama ng'ombe chombo cha kukunia nazi mlango : ukoo au watu wenye asili smoja sehemu ya kuingia kwenye nyumba kitu kinachotumika kifunga nyumba fua : unda vyombo/vifaa mbalimbali kwa kupiga chuma osha nguo vua : toa nguo kutoka mwilini toa samaki kwenye maji kiboko : mnyama mkubwa wa baharini silaha inayotumika kwa kuchapa au kupiga tembo : aina ya ndovu aina ya pombe } Visawe Maneno tofauti yenye maana sawa. msichana au banati : ⇒ kijana wa jinsia ya kike mvulana au ghulamu : ⇒ kijana wa jinsia ya kiume huzuni au majonzi : ⇒ hali ya kilio na huruma mazishi au matanga : ⇒ shughuli za kumzika marehemu wakati au mwia : ⇒ wakati au muda mtu au mja : ⇒ mnyama atembeaye kwa miguu miwili mwenye uwezo wa kuongea na kufikiri kimantiki barua au waraka : ⇒ kartasi inayoandikwa na kutumwa ili kuwasilisha ujumbe fulani siri au faragha : ⇒ jambo lisilopaswa kujulikana na mtu mwengine macho au maninga : ⇒ sehemu za mwili zinazotumika kuangalia na kuona mwangaza au nuru : ⇒ miyale inayowezesha watu kuona vitu Mungu au Mola au Rabana au Jalali au Rabuka : ⇒ Majina ya Mwenyezi Mungu
Daudi Mchambuzi JF-Expert Member Joined Nov 25, 2010 Posts 62,190 Reaction score 128,263 May 18, 2020 #2 Asante kwa elimu maridhawa.
Kennedy Platinum Member Joined Dec 28, 2011 Posts 61,544 Reaction score 74,314 May 18, 2020 #3 Sawa Mkuu Tupo Pamoja Kwenye Kiswahili Sanifu
Culture Me JF-Expert Member Joined May 24, 2017 Posts 10,494 Reaction score 21,453 May 18, 2020 #4 Shukrani sana kwa elimu. Boost your Immune System to fight a Covid-19.
Auz JF-Expert Member Joined Apr 6, 2016 Posts 13,841 Reaction score 11,775 Jul 21, 2020 #5 Haya maneno kwa mara ya kwanza niliyasikia kutoka kwa Mwalimu Wanjiku, vichekesho vya Churchill kwenye YouTube.
Haya maneno kwa mara ya kwanza niliyasikia kutoka kwa Mwalimu Wanjiku, vichekesho vya Churchill kwenye YouTube.
King klax JF-Expert Member Joined Jul 10, 2015 Posts 4,774 Reaction score 3,279 Jul 21, 2020 #6 Kweli kiswahili kigumu aiseee