Vitambulisho vya utaifa vimekwamia wapi? Mbona Zanzibar wameweza??

Vitambulisho vya utaifa vimekwamia wapi? Mbona Zanzibar wameweza??

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2012
Posts
4,572
Reaction score
26,896
Kwa kumbukumbu yangu toka waziri kabla ya Nchimbi walitangaza mpango huu tena kwa mbwembwe na rais akapewa kitambulisho namba 1 na wakaja na kelele nyingi eti wanaanzia mkoani Dar na cha ajabu hata wale walioandikishwa hawajavipata mpaka leo.

Naahindwa kuelewa hivi ni kweli hakuna hela au ni matumizi mabaya ya pesa za umma.

Pesa za wao kwenda kutibiwa nje na kufanya sherehe kubwa za kitaifa zipo ila ukiangalia zinamanufaa kwao lakini kwa mwananchi wa kawaida kwao haliwahusu.

Sasa hiii si dalili ya kushindwa kwa serikali na chama na ni moja ya kati ya ahadi hewa kwa wananchi?
 
Wewe upo mkoa gani? mbona sasa hivi wapo katika hatua za mwisho za kuchuku alama za vidole pamoja na picha kisha baada ya ndio itakuja hauta nyingine ya kutoa vitambulisho.
 
Hii ni agenda inayolifedheesha taifa na serikali ya ccm. Hoja hii hutawaona wachumia tumbo, hata wakja ni blablaaa tu. Watatwambia pesa wameipeleka wapi. It's a matter of time.
 
Kwa kumbukumbu yangu toka waziri kabla ya Nchimbi walitangaza mpango huu tena kwa mbwembwe na rais akapewa kitambulisho namba 1 na wakaja na kelele nyingi eti wanaanzia mkoani Dar na cha ajabu hata wale walioandikishwa hawajavipata mpaka leo.

Naahindwa kuelewa hivi ni kweli hakuna hela au ni matumizi mabaya ya pesa za umma.

Pesa za wao kwenda kutibiwa nje na kufanya sherehe kubwa za kitaifa zipo ila ukiangalia zinamanufaa kwao lakini kwa mwananchi wa kawaida kwao haliwahusu.

Sasa hiii si dalili ya kushindwa kwa serikali na chama na ni moja ya kati ya ahadi hewa kwa wananchi?
Kabla ya kuanza kulalamika fanya kwanza uchunguzi wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam wameishamaliza zoezi la kupata vitambulisho vya taifa wanakwenda kanda zingine.
 
viongozi wa tz waongo waongo hadi kinyaaaaaaaa
 
Wewe upo mkoa gani? mbona sasa hivi wapo katika hatua za mwisho za kuchuku alama za vidole pamoja na picha kisha baada ya ndio itakuja hauta nyingine ya kutoa vitambulisho.

Sasa huu ndio upuuzi hivi kweli muandikishe muondoke, mrudi mchukue vidole tena mkaee, tena mrudi mchukue saini mkaaeee, mrudi muhakiki tena mkaaeee ndo mje mgawe vitambulisho si miaka ishirini inayo kwa nchi nzima??

Semeni hela imeliwa
 
Kabla ya kuanza kulalamika fanya kwanza uchunguzi wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam wameishamaliza zoezi la kupata vitambulisho vya taifa wanakwenda kanda zingine.

Niko Dar wametuandikisha wanadai watarudi kuchukua alama za vidole , hivi utakaa hapo hapo hadi waje hatuna shughuri za kufanya??

Kwanini hilo zoezi lisifanyike kwa pamoja??
 
Niko Dar wametuandikisha wanadai watarudi kuchukua alama za vidole , hivi utakaa hapo hapo hadi waje hatuna shughuri za kufanya??

Kwanini hilo zoezi lisifanyike kwa pamoja??

ufahamu wangu unanikumbusha kuwa zoezi lilimalizika jana tarehe 9 wilaya ya kinondoni, kwa kuchukua alama za kibiolojia sasa wewe hiyo dar ambazo ndio kwanza wamewaandikisha ni wilaya ipi??
 
Niko Dar wametuandikisha wanadai watarudi kuchukua alama za vidole , hivi utakaa hapo hapo hadi waje hatuna shughuri za kufanya??

Kwanini hilo zoezi lisifanyike kwa pamoja??
Mkuu, zoezi linafanyika kwa makini sana. Si kama kugawa kadi za chadema
 
Sasa huu ndio upuuzi hivi kweli muandikishe muondoke, mrudi mchukue vidole tena mkaee, tena mrudi mchukue saini mkaaeee, mrudi muhakiki tena mkaaeee ndo mje mgawe vitambulisho si miaka ishirini inayo kwa nchi nzima??

Semeni hela imeliwa
Kweli kazi ipo
 
Kuna nchi ilitoa tamko la vitambulisho kwa wananchi na wasio wananchi waishio nchini humo ,zoezi lilitoka kwa amri kuwa ukipita muda fulani hujachukua kitambulisho basi itakubidi ulipie gharama zaidi na pia kuna huduma utakuwa huzipati kama huna kitambulisho na pia ikiwa utakuwa na mambo ya kuhitaji leseni basi kitambulisho ni lazima ,kuanzia leseni ya gari hadi ya mkokoteni. Ila serikali ilijitayarisha sana kwa kujenga vituo maalum vya kisasa vyenye tekinolojia ya kuchukua finga prints kwa kila kwenye kituo na unakwenda siku moja na unaletewa meseji kwenye simu yako ni wapi ukachukue kitambulisho chako ,zaidi wakikutumia kitambulisho kwenye posta iliyokaribu nawe ,kwa maana hiyo walijijenga kwanza na kujua wanachokifanya ila hapa Tz wamevamia mambu ya watu , na wenye nia sio watekelezaji bali kazi wamepewa walaji utoe chochote ndio upate kitambulisho.

Na bora vitambulisho iwe kwa kila mtu ikifuatiliwa na passport japo sio wasafiri vitu hivyo vitasaidia kupata mikopo kutoka mabenki na pia vitasaidia kuweka check point ili kusaka wahamiaji ,hili la kusaka wahamiaji kwa kutajana majina kuwa fulani si mzaliwa ni kusaidia wengine kuwatosa wengine.

Ila ya Zanzibar tuwaachie wenyewe wanasema huko Zanzibarhata mwananchi asie na ajira ataanza kulipwa muda si mrefu .
 
Niko Dar wametuandikisha wanadai watarudi kuchukua alama za vidole , hivi utakaa hapo hapo hadi waje hatuna shughuri za kufanya??

Kwanini hilo zoezi lisifanyike kwa pamoja??
Mkuu kila jambo lina utaratibu wake mimi mbona nimeishamaliza kila kitu na nimepewa Identification Card Collection Slip, nasubiri kwenda kuchukuwa kitambulisho changu.
 
mkuu, zoezi linafanyika kwa makini sana. Si kama kugawa kadi za chadema

mkuu lumumba wamepandisha dau nini??kadi za ccm ndio zinagawawiwa kama njugu hasa wakati wa uchaguzi!!!!!!!!!!
 
Mkuu Return Of Undertaker hili zoezi linaendelea lakini kasi yake ni ndogo mno.. Imagine mpaka sasa hivi zoezi la kupiga picha na kuchukua alama za vidole bado linaendelea hapa Dar.. Ina maana mkoa mmoja tu imewachukua mwaka mzima kwa kazi hii tu ya kupiga picha na kuchukua alama za vidole.. Tatizo kubwa nadhani ni uchache wa wafanyakazi maana hawa hawa ndo wanatakiwa wazunguke Tanzania yote.. Ina maana kwa mahesabu rahisi itawachukua miaka 27 kumaliza kazi katika mikoa yote ya hapa nchini..! Ni vizuri kwa Serikali kuongeza wafanyakazi ili zoezi likamilishwe ndani ya miaka michache.. Nimesikia kuna wafanyakazi kama mia hivi wamelamba ajira na wanaendelea na training kwa ajili ya kazi hii ila bado ni wachache sana.. Nadhani kila mkoa ungekuwa na wafanyakazi wake ingeweza kuwa nzuri zaidi..
 
Last edited by a moderator:
Nafikiri hawa watu hawana tarehe ya mwisho wa kutoa hivyo vitambulisho maana speed yao is almost zero. Hawana haraka na nafikiri kuna maelekezo fulani kwa makusudi fulani na kwa masilahi fulani!! Muda ukifika tutaelewa tuuu!!
 
Nakichukia UDSM maana ndio iliyoleta yote haya kikiwa kama chuo tegemezi cha TAnzania kwa miaka mingi,

Ramani nyingi ya mjini ziachwa na wakoloni hatukuziipliment.

Plan ya daraja la kigamboni ni ya miaka 40 kutokea.

Fly over sijui itatokea 2023 sijui ila ndio tylivyo
 
Back
Top Bottom