Mtangoo
JF-Expert Member
- Oct 25, 2012
- 6,163
- 5,623
Zoezi la uandikishaji wa vitambulisho vya uraia hasa kwa nchi kama yetu ambayo haina solid system ya vetting kwa sasa linapaswa kuchukua muda mrefu sana ili kuepuka raia wasio raia na mataifa mengine kupenyeza majasusi wao kama raia. Nashangaa uharaka wa serikali na wananchi kama wewe wa kutaka tu alimradi tuwe navyo. hii ni sensitive issue ambayo haipaswi kuingiliwa na siasa kabisa!Kwa kumbukumbu yangu toka waziri kabla ya Nchimbi walitangaza mpango huu tena kwa mbwembwe na rais akapewa kitambulisho namba 1 na wakaja na kelele nyingi eti wanaanzia mkoani Dar na cha ajabu hata wale walioandikishwa hawajavipata mpaka leo.
Kwa utaratibu na kasi hii ya umeme sitashangaa kukuta majasusi kibao wa nchi jirani wakiwa raia kabisa ilhali sio raia!
Hapa ungeweka statistics badala ya malalamiko. Facts na sio malalamiko ndio msingi wa majadiliano bora!Naahindwa kuelewa hivi ni kweli hakuna hela au ni matumizi mabaya ya pesa za umma. Pesa za wao kwenda kutibiwa nje na kufanya sherehe kubwa za kitaifa zipo ila ukiangalia zinamanufaa kwao lakini kwa mwananchi wa kawaida kwao haliwahusu.
Well sijaelewa wapi pameshindikana. na kama pameshindikana, Je Chama kinaingiaje hapa? Chama sio serikali na serikali sio chama. Lazima ifikie mahali tuchore mstari wa vyam kuiingilia serikali kimaamuzi na lawama za chama zibebwe a chama vivyo hivyo na za serikali.Sasa hiii si dalili ya kushindwa kwa serikali na chama na ni moja ya kati ya ahadi hewa kwa wananchi?
Hii nchi hatuendi kokote kwa kuwa tumegeuza kila kitu kuwa siasa. Ndio maana hata Uganda wanaanza kututimulia vumbi maeneo mengi.