Vitambulisho vya Taifa kutolewa wiki ijayo

Vitambulisho vya Taifa kutolewa wiki ijayo

Kimbori

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2012
Posts
6,292
Reaction score
4,785
HATIMAYE vitambulisho vya taifa vitaanza kutolewa rasmi siku saba zijazo, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imetangaza.
NIDA imebainisha hayo wakati ujumbe wake
ulipomtembelea Rais Jakaya Kikwete, Ikulu jijini Dar es Salaam, kukamilisha taratibu za kitambulisho chake.

Ujumbe huo ukiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, Dickson Maimu ulieleza kuwa kuanza kutolewa rasmi kwa vitambulisho hivyo kunatokana na kukamilika kwa utengenezaji huo.

Maimu alimwambia Rais Kikwete kuwa uzinduzi wa utoaji wa vitambulisho hivyo utafanyika kwenye Viwanja vya Karimjee, jijini Dar es Salaam kwa kuanza kuvigawa kwa viongozi wakuu wastaafu.
“Baada ya sherehe hizo za uzinduzi wa utoaji
Vitambulisho vya Taifa, maofisa wa NIDA watatoa
vitambulisho kwa wabunge na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar,” alisema Maimu.

Alimwarifu Rais Kikwete kwamba wanakadiria kutoa
vitambulisho kwa Watanzania milioni 21, wenye umri wa zaidi ya miaka 18.
Katika mazungumzo hayo, Rais Kikwete alitaka kujua
namna nchi nyingine zinavyoendesha suala la
Vitambulisho vya Taifa hasa namna ya kuvitoa bure kwa wananchi.

Maimu alimjibu kwamba kwa Tanzania gharama za
Vitambulisho vya Taifa zitabebwa na taasisi zinazotumia habari na takwimu zilizoandaliwa na NIDA. Kauli hiyo ilionyesha kumfurahisha Rais

Kikwete ambaye alisema: “Nawashukuru sana kwa kufikia hatua ya sasa. Tumeanza mbali mno na suala hilo, tangu mwaka 1968. Nafurahi sana kuwa tumefikia mahali pa kuweza kutoa Vitambulisho vya Taifa.”

NIDA ilianza zoezi la kuandikisha wananchi kwa ajili ya kutoa Vitambulisho vya Taifa mwishoni mwa mwaka 2011 baada ya kukamilisha mchakato mzima wa maandalizi.

Awali vitambulisho hivyo vilipangwa Kitambulisho cha
kwanza cha Taifa kuwa kimetolewa kwa mtumishi wa
umma Aprili mwaka uliopita, lakini ilipofika Novemba, 2012 Maimu licha ya kukiri mpango huo, alisema kwambal ifikapo mwaka 2014 utoaji vitambulisho hivyo utakuwa umekamilika ili viweze kutumika katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na baadaye Uchaguzi Mkuu, mwaka 2015.

Mkurugenzi huyto wa NIDA alitaja sababu za kuchelewa kutolewa kwa watumishi wa umma kutokana na mamlaka yake kukabiliwa na upungufu wa vifaa vinavyotumiwa kuchukua alama na vidole na picha.

Alisema kuwa mamlaka yake ilitakiwa kuingiza mfumo unaotumiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), pamoja na anuani za makazi unaoratibiwa na Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA).
Zoezi la uandikishaji wananchi kwa ajili ya vitambulisho hivyo lilianza mwaka uliopita ambapo ulifanyika kwa kanda mbalimbali.
Chanzo: Mwananchi Jumapili
 
Ok ngoja tuone jinsi mambo yanavyokwenda
 
Kuwapa wazanzibar vitambulisho vya taifa ni kupoteza pesa za walipa kodi, kwa maana haijajulikana hatma ya zanzibar, kujitenga ua kubaki katika muungano, na hii itategemea maoni ya wazanzibar wenyewe katika mchakato huu wa kukusanya maoni ya katiba mpya.
 
Ngoja vije tuone 2015 wataendelea na biashara yao ya kununua shahada, maana vitambulisho vya NEC walifanya, hivi vya NIDA nafikiri itakuwa ngumu.
 
Sasa kwanini waanze kupewa vitambulisho ambao hata wakipita tu barabarani''hupigiwa ving'ora'' na wengine wanajulikana sana kwa wananchi kwa jinsi wanavyo uchapa usingizi na kupiga madawati wawaa wakiwa mjengoni Idodomya utafikiri watoto wa chekechekea wakiwa kwenye vipindi vya radio watoto shoo siku ya jumamosi.Nchi hii kweli nimeamini raia wa kawaida ni wa mwisho kwa kila kitu,kwanza wao halafu ndio sisi jamani hata vitambulisho navyo vinafuata ukubwa?
 
je ambao hawakuandikishwa itakuwaje?
 
Mi siwaamini hata punje ni mpaka nione wananchi wakiwa na vitambulisho mkononi!
 
Wataanza kugawa vitambulisho siku Saba zijazo!! Samahani naomba kujiuliza, si walisema kuna zoezi la picha na kuchukuliwa Alama za vidole? Zoezi hili limefanyika? au liliwahusu wakubwa tu?
Samahani lakini!!
 
Wataanza kugawa vitambulisho siku Saba zijazo!! Samahani naomba kujiuliza, si walisema kuna zoezi la picha na kuchukuliwa Alama za vidole? Zoezi hili limefanyika? au liliwahusu wakubwa tu?
Samahani lakini!!

Kwa baadhi yetu ambao ni watumishi wa umma zoezi la picha na alama za vidole tayari, na zoezi linaendelea kwa kada mbalimbali za watanzania.
 
Ukiachilia mbali ni kitambulisho, kazi yake nyingine ni nini? mana wanataka detals nyingi sana.....
:confused2:
 
Kwa baadhi yetu ambao ni watumishi wa umma zoezi la picha na alama za vidole tayari, na zoezi linaendelea kwa kada mbalimbali za watanzania.

Hata hao watumishi si wote wamefanya zoezi hilo
 
Kwa wale watumishi wa serikali ambao bado hawajafanyiwa zoezi hilo hatima yao ikoje?
 
OK karibuni mtupatie vitambulisho vyetu. Lakini mimi nilipojiandikisha awamu iliyofuatia ilikuwa ni kuhakiki majina kama ni sahihi (spellingwise) Baada ya hapo sijapata taarifa za NIDA kurudi kwa ajili ya kupiga picha. Je vitambulisho vitakuwa bila picha? Au watakuwa wanapiga picha hapo hapo unapata kitambulisho chako??? Kama sivyo basi NIDA wamemdanganya Mh. Rais.
 
Na kwa walio ughaubuni watapewa lini au ni lazima warudi bongo kwanza ?
 
Back
Top Bottom