The Palm Tree
JF-Expert Member
- Apr 13, 2013
- 7,951
- 12,535
Sina hakika kama vyama shindani dhidi ya CCM vinalijua hili na kufanya counter attack kuona namna ya kuzuia na kukabiliana nalo....
Ndiyo. CHADEMA ama CUF ama UKAWA kwa ujumla mnaweza kuwa na mgombea Urais mzuri sana, na presentable katika uchaguzi mkuu wa 2020 ambaye ni very firm, aggressive na well informed kama Tundu Lissu, lakini kama hamtatambua mapema mbinu wanazozitumia CCM kushinda chaguzi na kuzikabili mapema, itakuwa ni kazi bure na kilio cha miaka yote cha kuibiwa kura chaweza kuwakumba pia mwaka 2020...
Sasa someni hii kwa utafiti usio rasmi sana nilioufanya mimi mwenyewe katika baadhi ya kata na vijiji MKOA WA SHINYANGA...
Kwanza ni vyema kufahamu kuwa, kwa mfumo wa utawala wa nchi yetu, ni ngumu sana kukitenganisha chama kinachotawala/ongoza serikali na chenyewe kama chama cha siasa. Hilo liko wazi kabisa...
Si tu kwa kuwa CCM ndiyo inatawala kwa sasa, bali hata kama itatokea kesho CHADEMA ama TLP ama NCCR - Mageuzi wakashika dola, nao wata enjoy mwavuli huu kama ilivyo leo kwa CCM.....
Kwa sasa na ambao labda hawajui, ni kuwa kuna mazoezi mawili ya aina yake yanaendelea nchi nzima....
Ukitafakari kwa kina namna mazoezi haya yanavyoendeshwa na kusimamiwa, unaikosa mantiki yake zaidi ya kuyaona ktk malengo ya kisiasa zaidi kinyume na inavyosemwa. Haya ni:
1. Zoezi la Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuandikisha wanachama wake upya kutoka ktk mfumo wa analogy kwenda mfumo wa kidigitali (kielektroniki)
2. Zoezi la kugawa Vitambulisho vya Rais kwa wamachinga vilivyopewa jina la Vitambulisho vya wajasiriamali wenye mtaji usiozidi Tshs 4,000,000 kwa kulipia Tshs 20,000 kila kitambulisho.
Shida yangu si mazoezi haya kufanyika. Tatizo langu kubwa ni malengo yake kwa kuangalia namna yanavyoendeshwa na kusimamiwa...
UANDIKISHWAJI WA WANACHAMA WA CCM KUTOKA MFUMO WA ANALOGY KWENDA KWENYE MFUMO WA KIELEKTRONIKI:
√Kwa sasa zoezi hili linaendelea nchi nzima kila kijiji/mtaa, kata, wilaya na mkoa....
√Kinachofanyika si tu kuwasajili wanachama wao ktk mfumo wa kielektroniki, bali ni pamoja na kuandikisha wanachama wapya ambao hawajawahi kuwa wanaCCM (hili sina tatizo nalo maana kila chama kina haki ya kutafuta wanachama)....
√Vituo vya waandikishaji hawa ni taasisi za umma kama shule, masoko, zahanati nk
√ Kwa kuwa vituo vya Uandikishaji kama nilivyosema ni taasisi za umma kama shule za awali, msingi, sekondari, zahanati, vituo vya afya nk, sharti la kwanza ni lazima kila mtumishi wa umma wa taasisi ile aandikishwe (hili lilinishangaza)....
√Unapokwenda kuandikishwa, sharti uwe na kitambulisho cha mpiga kura kama kigezo number one kwa wote wanachama wa kale na wanaoingia kwa mara ya kwanza (siyo kadi ya CCM!!).
√Ukifika unaonesha kadi yako ya mpiga kura, wanachukua namba yake, wanakipiga picha kwa kutumia simu maalumu walizopewa kwa kazi hiyo na baadaye nawe unapigwa picha na kurudishiwa Voter's ID yako na kisha unalipa Tshs 500 wanaita Registration fees.....
√Hili lilifanya nijiulize maswali haya:
1. Kwa nini wanalazimisha kila mtumishi wa umma aandikishwe kama CCM member?
2. Kwa nini voter's ID inakuwa ni kigezo kikubwa kuandikishwa?
3. Kwa nini ktk kuandikishwa mtumishi analazimika kutaja hadi umri wake kazini?
√ Binafsi, jibu nililolipata ni, hili, kuwa ni maandalizi ya uchaguzi wa Mwaka 2020 na hata wa 2019. Kuna hatari hata usipoenda kupiga kura siku hiyo, kwa mfumo huu utaonekana umempigia mgombea wa CCM kwa ngazi zote...... !
Wewe unalionaje hili? Vyama shindani dhidi ya CCM mpo? Mnayajua haya? Tundu Lissu aweza kuwa mgombea mzuri sana na kwenye fair playing ground, anaweza kushinda kirahisi kabisa kwa zaidi hata ya 90%. Lakini kwa mazingira haya yanayoandaliwa, itawezekana?
VITAMBULISHO VYA RAIS KWA WAMACHINGA:
√ Vina direct connection na chaguzi zote zinazokuja. Ni maandalizi ya wizi wa kura hayo na wala huhitaji PhD ya korosho ama kemia kulielewa hili.......!!
√ Just try to think. Tangu lini ofisi ya Rais ikishirikiana na ofisi za RCs, DCs, Maafisa Tarafa, WEOs, VEOs zikawa na majukumu ya moja kwa moja kuratibu shughuli za ukusanyaji mapato wakati ipo taasisi maalumu inayohusika kisheria kufanya shughuli hiyo, ambayo ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)?? Hamjiulizi hili na mkaja na kauli ya msimamo thabiti??
√ Kwa taarifa tu kwa wale wasiojua ni kwamba, hata kama huna Tshs 20,000, huna biashara yoyote ya hata genge la nyanya, kitambulisho hicho unapewa.....!!
√Watendaji wa vijiji wanachofanya ni tena kupita wenye taasisi za umma kama shule nk na kuwalazimisha walimu, manesi na yeyote aliye tayari kuchukua kadi hiyo buree haijalishi una biashara ama huna kama nilivyosema..!!
√ Kwa kifupi ni kuwa hivi Vitambulisho vya umachinga + kadi za lazima za uanachama wa CCM vina maana yake huko mbeleni, kwamba, vinaweza kuja kutumika kwa siri kubwa kama kigezo kwa watumishi wa umma cha kupata huduma, stahiki zako toka serikalini.....!!
• Niliongea na mtumishi mmoja aliyepata kadi ya CCM na ambaye hapo kabla (kwa maelezo yake) hakuwa mwanachama rasmi wa chama chochote cha siasa bali mpenzi na shabiki wa siasa za kimageuzi....
Nilimuuliza kipi kimemvutia sasa kuchukua kadi ya CCM. Jibu lake lilikuwa la kufikiririsha kidogo lakini lenye maana kubwa, na defenetely ndivyo ilivyo......
Alisema, ".....ndugu, if you can't beat them, join them.....!!!"
Namalizia kwa kusema, Tundu Lissu ama mwingine yeyote aweza kuwa perfect choice, perfect challenger wa CCM na Magufuli next 2020 General Election....
Lakini kama vyama vya upinzani vita - rely kwenye uwezo binafsi wa mgombea na personality yake pamoja na siasa za matukio ya kutengenezwa na washindani kisiasa kwa lengo la kuwatoa kwenye "focus" huku mkipuuzia kudhibiti mapema mbinu ovu kama hizi ambazo CCM huzitumia kushinda chaguzi, basi kilio cha kuibiwa kura kipo palepale ktk chaguzi zijazo...
Na mwisho mtakija kujiuliza kulikoni haya mambo??... Hiyo inakuwa haina maana tena kwani kwa waakati huo itakuwa imeshakuwa TOO LATE.....!!
Vyama shindani mpo??? .... Wake up. Mapambano yawe kotekote, kwenye mahandaki, milimani, baharini na nchi kavu na hata angani. Amkeni,!!
Msije mkasema hatukuwaambia. Tunahitaji uongozi wenu. Tuambieni ni nini cha kufanya.
Sisi wengine ni Jeshi kubwa ambalo tuko very unknown and invisible lakini tuko nyuma yenu, na tuko tayari kusaidia wakati wowote iwe mchana au usiku, mvua ama jua. What matters, ni onesheni uongozi uliotukuka na makini, toeni maelekezo YATATEKELEZWA!!