Vitambulisho vya NIDA vina nini cha ziada?

Kivumishi Kielezi

JF-Expert Member
Nov 1, 2019
1,028
2,448
Wakuu, naomba kujuzwa, kwanini TCRA inang'ang'ania watu wajisajili kwa kutumia vitambulisho vya NIDA pekee na si vitambulisho vingine kama vile kadi ya mpiga kura, leseni ya udereva na passport!?

Kuna nini hasa nyuma ya hizi NIDA?

Kama zoezi la usajili wa fingerprints lingekuwa na umuhimu mzito unaosemwa, basi wangeruhusu watu ambao hawana vitambulisho vya NIDA wajisajili kwa kutumia vitambulisho vingine.

Maana, la muhimu linalosemwa hapa ni usajili wa laini za simu kwa fingerprints ili tuwe na usalama wa kimtandao.

Lakini kumbe inavyoonekana, cha muhimu sio usajili wa laini za simu, bali ni kale ka kadi cha NIDA.

Naomba kufahamu, ni ipi ajenda yao ya muhimu kati ya hizi mbili:

MOJA: Watu kusajili laini za simu au,

MBILI: Watu kuwa na kadi za NIDA?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni utambambulisho wa utaifa.... Kila raia ni lazima kuwa nacho tofauti na vitambulisho vingine

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli. Lakini kwa madhumuni ya utambuzi wa taarifa za mtu, na kwa madhumuni ya usajili wa laini za simu, vitambulisho vingine vingefaa pia kusajilia na kuchukua fingerprints!

Ukizingatia urasimu wa upatikanaji wa vitambulisho vya NIDA, ingekuwa ni busara kuwaruhusu watu watumie vitambulisho vingine.

Ninavyoona hapa, ajenda sio usajili wa laini za simu. Kuna ajenda ambayo haijawekwa wazi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi naona ni mihemko tu na kukurupuka, mbona hawajasema kama hivi vitambulisho vingine vina mapungufu? Kwamba labda mtu akisajili line kwa kutumia leseni au kitambulisho cha mpiga kura na akafanya uhalifu haiwezekani kumpata? Labda lengo ni kupunguza watumiaji wa simu!

Sent using Redmi Y2
 
Yaani kuna kaushamba ambacho bado sijakaelewa vizuri!

Watu milioni kadhaa watakosa mawasiliano kwa ajili ya ujuha tu wa watu wachache!

Kwa kweli, kuna nia ovu ambayo haijawekwa wazi kuhusu hili zoezi batili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vitambulisho vya NIDA vitasaidia kuongeza wigo wa mapato ya serikali kwa kumtambua kirahisi mlengwa - yeye ni nani na anafanya shughuli gani n.k.
Pia kumtambua fasta mhusika pale anapohitaji huduma mbali mbali kule serikalini; mfano ktk masuala ya afya, benki, shule n.k.
Kadi ya mpiga kura haiwezi kukusaidia ktk hayo hapo juu maana haina details za kutosha.
 
Hayo mengine yote uliosema sio tatizo, shida ni kumfungia mtu sim eti kwasababu hana kitambulisho cha nida!
Hivi leseni haitoshi kumtambua mmiliki!?
Kadi ya mpiga kura ni feki!?
Pasport haieleweki!?

Lazima kuna jambo nyuma ya pazia"

Back
Top Bottom