Dume la Mende
JF-Expert Member
- Mar 23, 2011
- 423
- 66
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading"]
[/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Monday, 11 July 2011 08:56
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]
BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limeridhishwa na uwezo wa kiteknolojia
alionao mkandarasi aliyeshinda zabuni ya kutengeneza Vitambulisho vya Taifa.
Hayo yalisemwa jana na timu ya wabunge waliotembelea Kampuni ya Iris Corporation Berhad ya Malaysia, iliyoshinda zabuni ya kutengeneza vitambulisho hivyo walipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia ziara hiyo, Mkuu wa msafara huo, Anna Abdallah, alisema serikali imechelewa kutoa Vitambulisho vya Taifa na kwamba sasa lazima iharakishe mchakato huo kwa sababu vina faida nyingi kwa ustawi wa maendeleo ya kiuchumi na kijamii Tanzania.
"Sisi wabunge tunasema Vitambulisho vya Taifa, lazima vitolewe haraka kwa sababu ni muhimu kutambuana. Huwezi kumtofautisha Mtanzania na watu wa mataifa mengine kwa rangi au sura tu. Lazima tuwe na Vitambulisho vya Taifa," alisema.
"Wenzetu Malaysia wanatoa vitambulisho hata kwa watoto wadogo kwa nini sisi tushindwe," alisema.
Akiizungumzia Kampuni ya Iris alisema, "mi kampuni namba moja duniani katika kutengeneza vitambulisho vya kisasa. Hata mataifa ya Ulaya yanakwenda kujifunza kwa kampuni hiyo. Tutegemee kitu kizuri."
Mbunge wa Mlalo (CCM), Brigedia Jenerali mstaafu, Hassan Ngwilizi alisema Kampuni ya Iris ina uwezo mkubwa na italisaidia taifa, kutengeneza mfumo wa utambuzi na usajili wa watu na hatimaye kutoa Vitambulisho vya Taifa vyenye ubora wa hali ya juu.
Alisema teknolojia itakayotumiwa kutengeneza vitambulisho ambayo pia imetumiwa na Malaysia ni ya kisasa na kwamba inaweza kuhifadhi taarifa nyingi katika kitambulisho kimoja.
"Wenzetu wamepiga hatua, wameweza kuweka hata hati ya kusafiria katika vitambulisho vyao vya taifa," alisisitiza.
Kwa upande wake, Mbunge wa Maswa (Chadema), John Shibuda, alisema Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida) inapaswa kuungwa mkono ili ipate fedha na kuanza utekelezaji wa mradi huo.
"Vitambulisho ni mbegu ambayo itazaa matunda mengi, tuiwezeshe Nida ili tuvune
matunda yake haraka. Ni mradi utakaoleta neema kwa sababu ukianza kutekelezwa
ndani ya mwaka mmoja tunaweza kupata zaidi ya trilioni mbili," alisisitiza.
Alisema nchi kama Kenya haitegemei wafadhili, na kwamba inakusanya kodi inatokana na vitambulisho vya taifa.
Wabunge waliozulu Iris Corporation Berhad ni Anna Abdallah (CCM), Brigedia Jenerali mstaafu Ngwilizi (CCM), Hamad Rashid Mohamed
(CUF), Betty Machangu (CCM), Moses Machali (NCCR-Mageuzi), Jasson Rweikiza
(CCM), Rebecca Mngodo (Chadema) na Anastazia Wambura (CCM).
Wengine ni Rachael Mashishanga (Chadema), Mohamed Sanya (CUF), Mussa Hassan Mussa na
John Shibuda (Chadema).
Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa ilisaini rasmi mkataba na Mkandarasi, Iris
Corporation Berhad ya Malaysia Aprili 21, mwaka huu
Mkataba huu ulitiwa saini na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha kwa niaba ya Serikali.
Source?: Mwananchi