Vitabu nilivyosoma mwaka 2018 – Zitto Kabwe

Vitabu nilivyosoma mwaka 2018 – Zitto Kabwe

Hongera sana Zitto sio tu kwa kusoma vitabu 49 (vingi sana) kwa mwaka, bali pia kuleta hamasa ka Watanzania wengine (japo kwa uchache) kutokana na hulka yetu ya kutopenda kujisomea. Mwenye vitabu ndiko hazina ya maarifa ilikofichwa.
Laiti viongozi wengi wangekuwa wanasoma vitabu, wange tuepusha na majanga mengi yanayoweza kuonekana ni yakujitakia kumbe ni yatokanayo na kukosa maarifa.
Inasikitisha hata waalimu/wahadhiri wengi bado hawasomi vitabu hivyo kujikuta wakifundisha mambo yasiyokwenda na wakati.
Tuichukue hii kama chachu ya kujipatia maarifa yatakayotuwezesha hatimaye kujiletea maendeleo yetu.
Nafahamu wengi tunaweza kujiuliza tutapata wapi muda wa kusoma vitabu? Lkn tukijiuliza tunatumia muda kiasi gani kuangalia TV, wengine kwenye viti virefu kwa moja baridi, muda was kulala n.k.
Asante sana kwa kutushirikisha hazina uliyoendelea kuwekeza. Ni hazina kubwa kuwa na viongozi waliotayari kujifunza kula iitwapo leo. Keep it up Mh Kabwe!
 
Vitabu niivyosoma mwaka 2018 – Zitto Kabwe

Tangu Mwaka 2012 nimekuwa naorodhesha vitabu nilivyosoma katika mwaka. Si vitabu vyote huviweka hapa kwani vingine huwa nasoma na kuviacha njiani ama kutopendezwa navyo au kwa kusahau tu. Vitabu vingine huwa vitabu rejea na huvirudia kwa ajili ya mafunzo ili kufanya maamuzi Fulani Fulani au kwa ajili ya ibada (kwa mfano Quran) au kwa sababu nyenginezo. Nafurahi kuwa hivi sasa kwenye mitandao duniani kote watu wamekuwa wakiorodhesha vitabu ili kujengana katika utamaduni wa kusoma. Barack Obama yeye alianza kuweka orodha yake mwaka 2015 na tayari ameshaweka orodha ya mwaka huu. Obama pia huweka orodha ya muziki aliyopenda mwaka huo. Inavutia.

Mwaka huu nimesoma vitabu 49 (kutoka vitabu 36 + 3 vya mwaka 2017). Wakati natoa orodha yangu 23/12/2017 nilikuwa bado nasoma riwaya za Jumba Maro ya Ally Saleh na The Feast of the Goat cha Mario Vargos Llosa ambazo nilizimaliza nikiwa Maputo, Msumbiji. Pia niliweza kuongeza Simulizi iitwayo Zeitoun ya Dave Eggers kuhusu kimbunga cha Katrina huko New Orleans, Marekani. Hii ni simulizi ya wahamiaji kutoka Syria walivyoshiriki kuokoa makumi ya watu kutoka kwenye maafa ya Hurricane Katrina.

Mwaka 2018 nimesoma mchanyato kidogo kuliko mwaka 2017 ambapo dhima (themes) kadhaa ziliniongoza. Hata hivyo bado njaa yangu ya kuwasoma madikteta duniani iliendelea kuniongoza kwa lengo la kupata ufahamu na maarifa ya namna ya kuchangia katika kuzuia nchi yetu kuangukia kwenye utawala wa Imla. Pia nilijaribu kutafuta majawabu ya changamoto hizo. Kwenye dhima hiyo nilisoma:

- The Death of Democracy: Hitler’s Rise to Power
Benjamin C Hett

- The Plots Against Hitler
Danny Orbach

- Franco: Anatomy of a Dictator
Enrique Moradiellos

1 The New Sultan: Erdogan and the Crisis of Modern Turkey
Oner Cagaptey

- How Democracies Die
D Ziblatt and S Levitsky

Kama nilivyopata kusema, ninapenda na kujivunia sana historia ya ukombozi dhidi ya ukoloni barani Afrika na haswa Ukombozi wa Kusini mwa Afrika. Mwaka huu niliongeza maarifa katika eneo hilo kwa kusoma sio tu habari nzuri za vyama vya ukombozi bali pia baadhi ya makosa waliyofanya viongozi wetu. SWAPO Captive kilichoandikwa na Bwana Angula ni simulizi muhimu sana kusoma ili kuona namna baadhi ya watu walivyoonewa kwenye harakati za ukombozi. Kwa jina la ukombozi watu huonewa, huteswa na hata huuwawa. Pia nilisoma kuhusu mashujaa wa ukombozi na athari kwa familia zao. Katika dhima hii ya Ukombozi nilisoma:

- Cuito Cuanavale: 12 Months of War That Transformed a Continent
Fred Bridgland

- Africa Tomorrow
Edem Kadjo

- Umkontho we Sizwe: The ANC Armed Struggle
Thula Simpson

- Mozambique: Sowing the Seeds of Revolution
Samora Machel

- 491 Days
Winnie Mandela

- Thabo Mbeki
Adekeye Adebajo

- Umkontho we Sizwe
Janet Cherry

- Chris Hani
Hugh Macmillan

- Being Chris Hani’s Daughter
Lindiwe Hani and Melinda Ferguson

- SWAPO Captive: A Comrade’s Experience of Betrayal and Torture
Oiva Angula

Pia nilisoma vitabu vya hali ya sasa ya Afrika Kusini baada ya ukombozi:

- No Longer Whispering to Power: The Story of Thuli Madonsela
Thandine Gqubule

- How to Steal A City: The Battle for Nelson Mandela Bay, An Inside Account
Crispian Olver

- How to Steal A Country? State Capture and Hope for the Future in South Africa
Robin Renwick

- Coalition Country: South Africa After the ANC
Leon Schreiber

Kama Mtanzania ninayejiandaa kwa majukumu muhimu ya kitaifa nimekuwa nikipenda kupata maarifa Zaidi kuhusu Historia ya Zanzibar. Mwaka 2018 niliongeza maarifa kwa kusoma vitabu kadhaa ikiwemo:

- The Threat of Liberation: Imperialism and Revolution in Zanzibar
Amrit Wilson

- Social Memory, Silenced Voices and Political Struggle: Remembering the Revolution in Zanzibar.
(Ed) W. Cunningham and M. Fouere

Vitabu vinavyofuata ni mchanyato wa riwaya, historia za watu na mataifa mengine, mafunzo ya uchumi na kadhalika. Vitabu vinavyohusu Marekani na utawala wao mpya chini ya Trump ni kwa lengo la kujifunza nini kinaendelea huko. Kitabu cha Deng Xiaoping nilipewa na ndugu yangu Harith Ghassany katika mjadala wa kisomi wa kutafuta modeli sahihi ya kimaendeleo kwa nchi zetu za Afrika.

- Pakistan: Personal Story
Imran Khan

- Making Africa Work: A Handbook for Economic Success
Gregg Mills, O Obasanjo, et al

- Sidetracked
Henning Mankell

- In Praise of Blood: The Crimes of Rwandan Patriotic Front
Judi Rever

- Thomas Sankara Speaks
Thomas Sankara

- A Higher Loyalty
James Comey

- State Secrets: Deathly High Stakes in the Corridors of Power
Quintin Jardine

- Deng Xiaoping and The Transformation of China
Ezra F Vogel

- Gorbachev: His Life and Times
William Taubman

- Tell Tale
Jeffrey Archer

- The Growth Delusion
David Pilling

- CTRL ALT DELETE: How Politics and The Media Crashed Our Democracy
Tom Baldwin

- Unhinged: An Insider’s Account of The Trump White House
Omarosa Manigault

- Fire and Fury: Inside The Trump White House
Michael Wolf

- Why The Dutch are Different
Ben Coates

- The French Revolution: What Went Wrong
Stephen Clarke

- An Extra Ordinary Life: A Passion for Service
V J Mwanga

- Uwajibikaji Ndani ya Kalamu Isiyokuwa na Wino
Ludovich Utouh

- Betting the House: Inside Story of the 2017 Elections
Tim Ross and Tom McTaguwe

- In Defence of Bolsheviks
Max Shachtman

- The Future That Works: Selected Writings of A M Babu
(Ed) Salma Babu and Amrit Wilson

- Our Commonwealth: The Return of Public Ownership in USA
Thomas Hanna

- Democracy, Direct Action and Socialism: A Debate of Fundamentals
Michael Foot and Sean M

Mwaka huu ukiwa unaelekea ukingoni, Wachapishaji wa Vitabu Mkuki na Nyota Publishers walichapisha upya vitabu vya harakati za Willy Gamba, mpelelezi maarufu barani Afrika. Rafiki yangu katika kusoma vitabu Fadhy Mtanga (ambaye pia ni adui yangu kwenye soka – maana yeye ni shabiki mandazi wa Manchester United FC na mimi shabiki wa mabingwa watarajiwa Liverpool FC) alininunulia vitabu vyote 4 vya Mzee Elvis Musiba. Nilikuwa na muda wa kutosha na kuvisoma vyote bila kuweka chini. Namshukuru sana Fadhy kwa zawadi yake murua kabisa. Vitabu hivi ni:

- Kikosi Cha Kisasi
A E Musiba

- Njama
A E Musiba

- Kufa na Kupona
A E Musiba

- Hofu
A E Musiba

Kitabu changu cha mwisho mwaka 2018 ni :

- Dear Ijeawele OR A Feminist Manifesto in 15 Suggestions
Chimamanda Adichie

Vitabu 3 vilivyonigusa sana
The Death of Democracy
: Hitler’s rise to power cha Benjamin Hett kilinigusa sana kutokana na namna wanasiasa wanavyoweza kufanya makosa yenye kudidimiza nchi kwa sababu tu ya kulinda madaraka. Katika kitabu hiki somo kubwa ni namna Wabunge wa vyama vyote vya Siasa walivyomruhusu Adolf Hitler kutunga sheria inayompa mamlaka makubwa wakiamini kuwa Hitler ana nia njema na atawalinda. Wabunge wa Chama cha SDP ndio pekee walikataa, walizomewa, kuzodolewa na hata kuuwawa. Wengine walikimbilia uhamishoni. Ndani ya miezi michache, hata wale waliomwunga mkono Hitler walishughulikiwa na Taifa la Ujerumani likaingia kwenye taharuki kubwa na hatimaye vita vya pili vya dunia. Waliompa madaraka Hitler waliamini kuwa watamdhibiti. Hawakuweza. Historia kama hii ipo lakini wanaadam hatujifunzi tunarudia makossa hayo kila wakati katika nchi mbalimbali duniani.

How Democracies Die cha Ziblatt na Levitsky kilinigusa sana kwa kuwa kinatoa majawabu ya changamoto za demokrasia kuanguka. Licha ya kwamba ni kitabu maalumu kwa muktadha wa nchi ya Marekani, kitabu hiki nilicholetewa na rafiki yangu Rakesh Rajani, kinatazama mifano ya nchi mbalimbali duniani kama Colombia na njia walizotumia kuhami demokrasia (walitumia sana Bunge na Mahakama), Venezuela (jinsi mgomo wa vyama vya upinzani kutoshiriki chaguzi ulivyotoa nafasi ubwete kwa chama tawala) na hata Ujerumani ambayo hali yake nimeeleza hapo awali. Somo kubwa kabisa kutoka kitabu hiki ni kwamba ni lazima wadau wote wa demokrasia kushirikiana pamoja kupambana na udikteta bila kujali tofauti ndogo ndogo au kubwa kubwa miongoni mwao. Bila ushirikiano dikteta husaga saga kila mmoja. Ni Kitabu nashauri kila mwana demokrasia akisome.

Dear Ijeawele Or A Feminist Manifesto in 15 Suggestions cha Chimamanda Adichie ni kitabu kidogo sana kwa idadi ya kurasa. Kwa hakika ni barua ambayo Chimamanda kamwandikia rafikiye ambaye amepata mtoto wa kike na anamshauri amkuze vipi mtoto huyu. Kijitabu hiki kimenigusa kwa sababu kinatoa changamoto kadhaa kwa sisi wanaume katika malezi. Kuna mambo ambayo tunafanya tunaona kama ni msaada kumbe inapaswa kuwa wajibu kwa familia. Kwa mfano, mara nyingi husikia wanaume tukisema ‘leo nafanya kazi ya kulea mke wangu kasafiri’ ama kwa kimombo ‘baby-sitting’. Chimamanda anatuambia hapa, Baba mtoto hafanyi ‘baby-sitting’ bali anatimiza wajibu wake kama baba. Pia kinachoitwa ‘gender roles’ kwenye nyumba zetu kiasi kwamba tunazuia watoto wa kike kukua na kukuza vipawa vyao vyote. Nashauri wenye watoto wa kike wasome kijitabu hiki, wababa na wamama kwani kinaweza kuchangia kubadili mtazamo wako wa namna tunalea watoto wetu wa kike. Mapendekezo 15 ya Chimamanda unaweza usiyakubali yote lakini yana mafunzo mengi ambayo yanaweza kukufaa kwenye malezi ya mabinti zetu.

Heri ya Mwaka mpya 2019

Zitto Kabwe
Dar es Salaam
30/12/2018
Uliza sasa hawa wahamiaji hapa nchini kama kuna kitu wamesoma...

1. JPM
2. Daudi Bashite
3. Kigwangala
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]HONGERA kwa list hii mkuu
Nipatie kitabu 2, 3 na 5 mkuu
Maana ni Engineer anayetaka kupaa border sio kushinda Chato

Sent using Jamii Forums mobile app

Nimeshavigawa kwa Watu wengine labda kama wakiwahi kunirudishia nitakutumia kutokea hapa Kisiwani Puerto Rico ninakoishi sasa mwaka wa 12 huu.
 
Hilo neno dikteta umelisema wewe sio mimi.
Wewe si ndiyo umesema tunataka kinyume cha dhaifu?Na kwamba Maghufuli ndiye mwenyewe!Nikakuuliza kwani dhaifu ni lazima awe dikteta? Unaleta pambio za "dikteta umelisema wewe", wtf, Bado tu unajikanyaga kanyaga!Tuliza ubongo na usome taratibu bila mihemko na kutaka kubandika tu humu. Nani amesema ulitaja neno dikteta?
 
Wewe si ndiyo umesema tunataka kinyume cha dhaifu?Na kwamba Maghufuli ndiye mwenyewe!Nikakuuliza kwani dhaifu ni lazima awe dikteta? Unaleta pambio za "dikteta umelisema wewe", wtf, Bado tu unajikanyaga kanyaga!Tuliza ubongo na usome taratibu bila mihemko na kutaka kubandika tu humu. Nani amesema ulitaja neno dikteta?
"Maghufuli" sijui ndio nani...
 
Tafadhali unaweza kutusaidia namna unavyoweza kusoma kwa speed, halafu yanakaa kichwani, wakati nafahamu fika una majukumu makubwa ya kisiasa na kitaifa.Maarifa haya yatasaidia wengine ambao tunasoma vitabu kumi kwa mwaka tuongeze bidii ya kuchuma maarifa zaidi.Pengine itasaidia kuelewa hata hivyo vitabu vina kurasa ngapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[http://mentalfloss]

MENU

ARROW

BOOKS

This Test Will Tell You How Many Books You Can Read in a Year

BY MICHELE DEBCZAK

JANUARY 17, 2019

[https://images]

ISTOCK.COM/ELENALEONOVA

It's tempting to compare yourself to others when pursuing a reading goal. According to the Pew Research Center, the average person in the U.S. reads about 12 books per year—but that number won't help you if you read at a different pace than the average American. To figure out how many books you should read in a year, Lenstore has come up with a test that measures your individual reading skills.

00:02

01:05

To start, click on the test below and read the passages that pop up at your natural reading speed. Once you've finished, you'll be asked a few questions about the reading to prove you understood it.

Lenstore gave the test to 1600 people and found that the average participant took 101 seconds to complete the passage. If a person reads for 30 minutes a day at that speed, they can get through 33 books a year (assuming book lengths average out to 90,000 words). Speedy readers who blast through the passage in 60 seconds can read 55 books in a year with 30 minutes of daily reading time—which comes out to just over one book a week.

If half an hour of reading a day sounds overly optimistic, you can see how your book goal would change based on your reading schedule. Lenstore also shows you how long it would take to read specific books based on your reading speed. They give examples of long reads that require many hours of commitment, like War and Peace, as well as quick books like The Color Purple.
After taking the test, check out our list of the best books of 2018 for some suggestions of what to read next.









Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na Mimi pia nimo nmesoma siku za mwisho za uhai wangu,rais anampenda mke wangu na machozi na damu by Erick shigongo
 
Based on your 2017-2018 liat you inspired me to rwad 60 books. ?.Thanks #zittokabwe below ia my 2019 list
60 YEAR BOOK CHALLENGE)
QUARTER ONE BOOKS
1.Bad blood-John carreynue
2.21lessons for 21st century- yuan Noah Marari
3.Factfulness-Hans Rosling
4.Emergency viruses (AIDS&EBOLA)..Nature &accident or intention-Leonard Herowitz
5.Opereshioni panama-Japhet nyamongo
6.50th law-50CENT&Robertgreene
7.JACKSONINC-ZACK.O.MARLEY
8.The10timesrule-Grant cardone
9.Dead aid-Dambisa Mayo
10.Built to last-Jim Collins
11.The amaizing S.A.S-Ian Macphedran(Still on it)
12.The7 habit of highly effective people--Stephen covey(still on it)
QUARTER 2 BOOKS
13.The wolf of wall street-jordan belfort
14.The art of war-SunTzu
15.Behind presidential curtain-Noble malala
16.The adventureof TinTin in the land of soviety-TinTin
17.I can I must I will(spirit of successz)-Reginald Mengi
18.The intelligent investor-Benjamin graham
19.Around the way giel-Taraj henson
20.Tanzania industrialization journey-A.A.mafuruki,Rahim Mawji
21.Freshwater Aquariu, for dummies-Maddy hargrove
22.The powet of habits-brian tracy
23.International konetary report on tanzania-imf
24.Richest men inBabyron-George s
25.Delivering happiness-Tonny hsieh
26.shoe dog-Phil knight
27.sales bible-Geffrey Gitommer
QUARTER 3 BOOKS
28.The subtle art of not giving a ***-Mat manson
29.Why great man fall-wayde Goodal
30.Allan quartemanrider Haggard
31.Secret-Rhonda bryne
32.The monk who sold his ferrari-Robin sharma
33.Who moved my cheese-spencer Johnson
34.Socrates in 90 minutes-paul Strathen
35.The 5 second rule-Mel robbinson
36.Truth doesnt have a side-Dr Bennet Ommaru
37.China Diplomacy and economic activities in Africa-Anja Rahtinen
38.Dictatorland (The man who stole Africa)-Paul Kenyon
QUARTER 4 BOOKS
39.Hurricane A memoir-Rick Ross
40.The Huawei story-Tian Tao wit WUcHUNBO
41.The Autobiography of GUCCI MANE with Neil-Martinez-Belkin
42.TIM COOK:The genious who took aple to next level-John Ive
43.My Journey into AI-KAI Fu Lee
44.New confession of economic hitman-John Perkins
45.Mind your mind-Remez sasson
46.The Psychological werfare-Michael stevens
47.The prince-Nocollo Machiaveli
48.Rosa Mistika-Euphrase Kezilahabi
50.Conversation with myself-Nelson Mandela
51.Kaptula la marx-Euphrasia Kezilahabi
52.Kochland(The secret history of Koch industries and corporate power in America)-christopher leornard
 
Back
Top Bottom