Vita ya ufisadi: Wilaya ya Bagamoyo yatangaza operesheni ya kusaka mali za viongozi wa vijiji

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,817
4,058
Wilaya ya Bagamoyo imetangaza operesheni ya kusaka mali za viongozi wa vitongoji, vijiji na watendaji kutokana na baadhi yao kubainika kujipatia mamilioni ya shilingi kwa kuuza ardhi kinyume cha sheria na kuchochea migogoro mingi ya ardhi wilayani humo.
 
Viongozi wakubwa wa Wilaya wasijiweke pembeni ktk hili. Hasa ambao wamekuwepo tangu awamu ya 4, hapo wilayani. Kama kuna dhamira ya dhati basi wafalme muwe tayari kuvuliwa nguo. Kuna Orodha yenu mliojitwalia mapande ya ardhi Bagamoyo.
Wasimezwe dagaa pekee
 
Nimechoka na vichekesho vya nchi hii, kila leo wananivunja mbavu zangu. Waanzie kwa wakurugenzi, DC na wakuu wa idara huko ndo kuna uozo wote.
 
Kuna zile fisadi nzito nzto zinazohusisha mabilioni ya fedha kama Iptl,escrow,richmond etc

Mbona haziguswi?Tutaokoa pesa nyingi sana
 
Back
Top Bottom