Vita ya 3 ya dunia (WW3)

EngFDM

Member
Feb 2, 2017
13
28
Dunia imeshakumbwa na vita nyingi sana, ila kwa mujibu wa historia zipo vita kuu mbili zilizoigawanya dunia kwenye pande mbili, vita zilizosababisha vifo vya mamilioni ya watu, vita ya kwanza ya dunia(WW1) na vita ya pili ya dunia (WW2).

Tangu kuisha kwa vita ya pili ya dunia mnamo mwaka 1945, dunia bado haijapitia vita kubwa iliyoyagawa mataifa ya dunia katika pande mbili, ila kwa yanayoendelea sasa, kuna uwezekano mkubwa wa dunia kuingia katika vita kubwa ambayo inaweza kupelekea kiama (dunia kufika mwisho).

Je nini mtazamo wako wa vita ya tatu ya dunia(WW3), Kipi kitakuwa chanzo? Na dunia itakuwa na sura gani mara baada ya hii vita kuisha??
 
Vita ya 3 ya dunia itaanzia Israel, na itaanzishwa na mataifa ya Ukata kuishambulia Israel, ila haitapiganwa kwenye mataifa mengine, itakuwa ni vita kati ya mataifa ya ulaya, middle East, Africa, America dhidi ya Israel, USA itakuja kupata rais ambaye hataitambua Israel ingawa atakuwa rais mwenye asili ya Israel na ndo atatoa kibali cha Israel kushambuliwa baada ya Israel kukaidi na kukata kutimiza matakwa ya USA ya kuunda mataifa 2, Israel na Paledtina, kwa sababu mpango wa nchi 2 itabidi Israel apoteze nusu ya nchi yake na miji muhimu kama Yerusalem, Nazareth, Bethlehem iende Palestine, tajwa hilo Israel atalikata katu na atasema hatuko tayari kutoa ardhi, tuko tayari kwa lolote, na hapo ndi mabomu ya nuclear yatapigwa, Israel ndo ataanza kutumia bomu la nuclear baada ya kuona mashambulizi kutoka kila mahari
 
WW3 haitokuja kutokea mana hakuna nchi inayotaka vita kwenye ardhi yake ndio mana hakuna mbabe atakayempiga mbabe mwenzake.

Mataifa makubwa/wababe wanapigana kupitia migongo ya wengine na hicho kinachofanya WW3 isiwepo.

Mtasikia tuu USA amepeleka makombora Ukraine au Israel ili kumpiga Palestina au Russia lakini kamwe huwezi kuja kusikia USA ameipiga Russia.
 
Back
Top Bottom