Puyugu 01
JF-Expert Member
- Feb 3, 2018
- 573
- 455
Katika pitapita zangu kwenye baadhi ya mitandao mbalimbali, nimekutana na taharifa ya kufunguliwa kwa nyimbo za Roma ambazo hapo awali tuliambiwa zimefungiwa coz zimemomonyoa Maadili ya watanganyika, nimekumbuka ule msemo usemao "Vita vya Panzi furaha ya Kunguru", na hii ni baada ya Battle kali kati ya SHONZA Vs CHIBU iliyopelekea top wa wizara ya Habari, Utamadu, Sanaa na Michezo ndugu Mwakyembe kuwaita wawili hao na kuwapatanisha juu ya mzozo uliolandana na ule wa Roma, mzozo huo wa Shonza vs Mondi mnyama uliozuka mara baada ya Shonza kufungia nyimbo za Chibu kwa niaba ya Serikali hali iliyopelekea taflani hadi wizara husika kuzifungulia nyimbo za chibu na hatimae kumnufaisha Roma pia, kama sio battle ya panzi hawa, hakika Kunguru (Roma) asingepata mlo siku hio.
Nimalizie tu kwa kusema kuwa CHIBU ni nembo ya tz ktk Sanaa ya muziki mana anaweza kumkomboa msanii mwezie bila mkombolewa kujijua kuwa anakombolewa na CHIBU.
Shikamooo Mondi mnyama.
Nimalizie tu kwa kusema kuwa CHIBU ni nembo ya tz ktk Sanaa ya muziki mana anaweza kumkomboa msanii mwezie bila mkombolewa kujijua kuwa anakombolewa na CHIBU.
Shikamooo Mondi mnyama.