Maoni yangu kwa mgogoro wa Wasanii hasa diamond na wizara ya habari utamduni sanaa na michezo

PatriceLumumba

JF-Expert Member
Mar 9, 2016
426
578
MAONI YANGU KWA MGOGORO WA WASANII HASA DIAMOND NA WIZARA YA HABARI UTAMDUNI SANAA NA MICHEZO

Naomba nitangulize shukrani zangu kwenu wote wadau wote habari utamaduni na michezo
Pia nieleze kusikitishwa kwangu sana na mzozo huu unaoendelea.

MIMI NAONA HAPO WOTE WANA MAKOSA.

Kosa la Diamond
Diamond kosa lake ni moja tu ambalo naamini ni la kibinadamu zaidi Kosa lenyewe ni kumjibu Naibu waziri kwa maneno yale mitandaoni hilo tu Ila hilo linajulikana wazi mtu akiguswa kwenye maslai yake bila kufata utaratibu lazima akasirike sana hilo tu ndio kosa la Lake.

Hatua alizotakiwa kuchukua Diamond

Diamond angetoa malalamiko yake kwa Waziri na Wizara na BASATA kwa kutumia vyombo vyombo vya habari na pia kuandika barua kuomba BASATA kukutana na wasanii wote waliofungiwa pamoja na SERIKALI ili kutatua mgogoro huu.

Ushauri kwa Diamond
Diamond anatakiwa kwa sasa kuwa makini sana yeye yuko kwenye ngazi ya kimataifa na mtu ukifika ngazi hizo kuna maadau wengi ambao hutumia kila njia kutafuta kukuchafua na kukushusha kwahilo Basi anatakiwa kuwa makini sana kwa kila neno analolitoa kinywani mwake kwani Kwa sasa Ulimwengu haumjui NASIB ABDUL unamjua DIAMOND PLATNUMS.

Diamond sasa anatakiwa kabla hajatoa neno au kuposti kitu kwenye mitandao awasiliane na mshauri wake na mwanasheria wake kwanza ili wamshauri kwanza kuona madhara ya kitu atakachokisema na kama angefanya hivyo hili lizingetokea.Pia umefikiwa kuwa na watu hao yani washauri hasa wenye upeo mkubwa na dira ya mbali na wasomi wazuri.

Alipoteleza Waziri
Kwanza lazima tujue mara nyingi huwa Serikali Haikosei ila watendaji waliopewa dhamana yakuongoza serikali ndio wanaokosea mpaka kusababisha serikali kulaumiwa nasema hivi kwasabau misingi ipo sheria zipo ila wengi hawafati.

Waziri kwenye swala kama hili lazima ajue yeye na wizara yake ni walezi na wapatanishi sio mtoa hukumu ,Yeye atapatanisha tu kati ya mhusika na chama kinacho simamia kazi za msanii au mwanamichezo husika ndio maana hata wachezaji mpira wanafungiwa na TFFna sio serikali.

Mfano leo hii kuna nyimbo nyingi sana za Marekani na Nchi nyingine zinaonyeshwa na kupigwa hapa kwetu tafsili ya maneno yake na picha zake ni matusi makubwa sana hapa kwetu tena ya waziwazi mbona hizo hamzifungii?

Hatua alizotakiwa kuchukua Waziri
Waziri alitakiwa kuwakutanisha BASATA na wasanii waliofungiwa nyimbo zao ili kutafuta muafaka wa hilo.

Waziri kwa kupitia Wizara angewaambia BASATA watoe sababu za kimaandishi kila nyimbo na kila kipengele au mstari wa nyimbo uliosababisha kufungiwa ili msanii aweze kujitetea,Leo hii kama imefungiwa nyimbo kwa kumuonyesha mwanamke kavaa nguo ya ndani mbona zipo nyimbo nyingi za wasanii wa kwetu wanaonekana wanawake wakiwa wamevaa hizo na hazijafungiwa?.

Ushauri kwa Waziri BASATA

Kuwakutanisha BASATA na wasanii ili kumaliza tatizo hili.
Kuwaambia BASATA kufanya semina mara kwa mara na wasanii wote ili kuwakumbusha na kuwapa maelekezo zaidi njinsi ya kutekeleza kazi zao za muziki bila kuvunja sheria.

Kuwasimamia BASATA wasitumike ki maslai na watu wengine kwa kazi za wasanii.

USHAURI KWA BASATA

BASATA kwa sasa mnatakiwa kufanya kazi kwa weledi mkubwa simanishi hamfanyi hivyo lahasha ila uzidi,Kuna nyimbo nyingi sana ambazo ukizifananisha na hizo mlizozifungia hazina tofauti na zipo za Nje ya Nchi ndizo chafu kabisa sasa msifungie za ndani zenye afadhali mkaziacha za nje nyie na wizara ndio mnatakiwa kuwalea kuwaongoza na kuwasimamia wasanii wetu hata kazi ao zinapoibiwa nje ya nchi au wakiwa na migogoro wao kwa wao sio rudisha nyuma.

Leo hii nyimbo mlizozifungia tayari wasanii wameshalipa zaidi ya milioni 200 kama Diamond kwa mfano na pia kwenye hayo malipo tayari kodi mbaimbali zimeshalipwa sasa unapomfungia mtu kama huyo wewe mhusika ndio mwenye makosa (BASATA)Unaonekana hauna mpango kazi.Msanii anatoa nyimbo mpaka inakaa miezi 6 ndio unamfungia si sawa.

Fungulieni hizi nyimbo sio moja au msanii mmoja tendeni haki zote , pangeni kufanya kikao kikubwa na wasanii kujadili mambo haya yanayoleta shida pia toeni msamaha kwa Msani Roma najua wote kwenye hili wamejifunza.

USHAURI KWA WASANII
Wasanii sasa lazima kurudi kwenye mstari kweli wengi mlijisahau sana sasa ni wakati wa kurudi kwenye nyimbo zetu zenye Maadili yetu hata kama unataka kutoa nyimbo ya hadhi ya kimataifa sawa il bado usitoke sana nje ya asili yako kwa maneno na hata picha.

Wasanii msidharau pale inapotokea miito kwenye vyama vyenu, kama umepata simu au barua toka BASATA au kwa kiongozi yeyote husika ni wajubu wa kuitikia haraka au kama kuna sababu lazima iwe ya msingi kwani hao ndio wasimamizi wa kazi zenu.

Nyie ndio kii cha amii bila kujali unaumaarufu gani lazima uendani na maadili yetu ya KItanzania kama unaona huwezi basi una uamuzi wa kuomba ulaiya wa nchi nyingine ukatoe kazi zako huko ila sio hapa.

HITIMISHO
Sote kwa ujumla kama WaTanzania tuungane kuendeleza muziki wetu,Tusikubali watu wachache kwa maslai yako kutuvuruga tutumie sanaa yetu kutangaza TANZANIA.
Kwani sanaa ni Kiburudisho na Ajira pia.

MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU IBARIKI AFRICA
PATRICE LUMUMBA
 
IMG_3303.jpg

Done
 
Back
Top Bottom