Vita vya Mini Van (MPV) kutoka Japan: Ipi ni chaguo lako?

Vita vya Mini Van (MPV) kutoka Japan: Ipi ni chaguo lako?

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
31,139
Reaction score
88,800
Kuna wapenzi wa mini vans kwa matumizi ya familia, biashara (private/special hire) au misele mjini.

Hizi nyingi zina seat 7 kwa configuration ya 2 + 3 + 2, na milango mitano. Ni spacious, kwa abiria na zina boot kubwa kwa mizigo. Pia zinakua na nguvu ya kutosha kabisa kuhandle uzito wa abiria na mizigo yao.

Leo naomba tuziongelee tano na kwa aliewahi kua na experience nazo anaweza toa ushahidi au kama una mtazamo wa kuimiliki siku unaweza changia pia.

1. Toyota Noah / Voxy / Esquire

Noah family ndio mini van maarufu sana Tanzania. Tumeona zinatumika sana kubeba abiria kuanzia mijini na vijijini, pia ni reliable roho ya paka na rafiki kwenye ulaji wa mafuta.

Noah ndio basic, Voxy ni sport version ya Noah wakati Esquire (ila ipo discontinued ) ni luxury version ya Noah, ila vingine engine na trans wanashare components nyingi.
IMG_6393.jpeg

Noah ina generation nne, ya kwanza kabisa ni ya mwaka 2001 ina option moja tu ya engine ya 2.0L 1AZ na trans either automatic ya 4-gears au CVT.
IMG_6394.jpeg

Generation ya pili ilianza 2007, yenyewe ina engine 2.0L 3ZR na CVT transmission tu.
IMG_6404.jpeg

Generation ya tatu ilianza 2014 kukiwa na 3ZR ya 2.0L engine na CVT transmission, ila ikaongezwa na hybrid ya 2ZR yenye 1.8L engine na eCVT transmission.
IMG_6396.jpeg

Ya nne ya mwaka 2022 ina engine ya 2.0 M20A au 1.8 2ZR hybrid.

2. Toyota Alphard /Vellfire

Bila maneno, hii pia ni best mini van na imependwa sana Tanzania. Hii ni luxury zaidi uku swala la fuel efficiency ikiwa sio case yake ingawa wana hybrid version, bado sio efficiency sana.
IMG_6402.jpeg

Generation ya kwanza ya Alphard (AH10) ilianza 2002 hadi 2008. Ilikua na 2.4L i4 engine, 2.4L hybrid na 3.0L V6 engine, na eCVT au automatic transmissions.
IMG_6403.jpeg

Second generation (AH20) ya 2008 - 2015 yenyewe ilikua na engine ya 2.4L, 3.5 V6 engine na 2.4L hybrid zikija na 6 speed, 7 speed na eCVT transmission.

Kimuonekano Gen ya kwanza na ya pili hazikupishana sana wengine wanasemaga gen 2 ni kama 1.5 version tu.
IMG_6404.jpeg

Generation ya tatu AH30 (2015 - 2023) ilikua na mabadiriko makubwa kimuonekano ndani na nje na kwenye engine.

Kwa engine ilikuja na 2.5L 2AR, na 3.5L 2GR V6, na 2.5L 2AR hybrid. Pia ilikuja na either transmission ya 6 speed, 7 speed, 8 speed au eCVT.
IMG_6405.jpeg

Generation ya nne (AH40) ni latest zaidi, ni ya mwaka 2023 - hadi sasa. Hii kidogo ilitoka kwenye kundi la “Alphard” kwasababu wamechukua platform (chasis) ya Lexus LM MVP ambazo ni luxurious department ya Toyota.

Hii ina engine za 2.4L na 2.5L pia zipo hybrid na plugin hybrid engines, zote i4 wameachana na V6. Pia transmission ni mbili tu, 8 speed na eCVT kwa hybrids.


3. Honda Step WGN

Honda Step WGN sio maarufu sana Tanzania, ila kwa nchi ya Japan ni moja ya best selling mini van. Hii ina generation zaidi ya 6, kuanzia mwaka 1996 hadi leo.

Honda Step WGN ni cheaper, ila sio luxury kama Alphard wala siwezi sema ni reliable kuzidi Toyota Noah ila ni reliable sana.
IMG_6390.jpeg

Generation ya tano na ya sita ndio zinazovutia zaidi. Zinakuja na engine ndogo za 1.5L, 1.5L turbo, 2.0L na hybrids zake wakati transmission ni CVT.

4. Nissan Serena & Elgrand
IMG_6409.jpeg

Nissan Serena na luxury /premium yake Elgrand nazo ni best selling mini vans. Zina generations zaidi ya sita kuanzia mwaka 1991 hadi leo.
IMG_6410.jpeg

Kuna engine options za aina nyingi kuanzia 1.2L, 1.4L, 1.5L, 2.0L na 2.5L zikiwa na technology mbalimbali kuanzia normal hybrid hadi e-power.

Mchawi ni CVT transmission ya Nissan, haina reputation nzuri sana ila sio case ya leo.

5. Honda Odyssey & Freed
IMG_6406.jpeg
Honda Odyssey sio gari ya kuiona kila siku hapa Tanzania, ila ni moja kati ya best car mini van kuuzwa Japan. Ina generation zaidi ya nne, ila latest ni ya kuanzia 2013 na ndio ambayo mtu unaweza inunua ata bei yake sio ya moto sana.
IMG_6408.jpeg

Honda Freed yenyewe ina generation tatu tu, kuanzia 2008 hadi leo.


Ipi chaguo lako, generation (mwaka upi)?

Kwa upande wangu, nimeipenda sana Honda Step WGN especially 6th generation 2022 - hadi sasa.

IMG_6391.jpeg

Engine zipo za cc 2000 ambazo ni hybrid (e:HEV) na zipo za cc 1500 sio hybrid.
IMG_6392.jpeg

Inamuonekano mzuri ndani na nje, engine reliable (LFA ya Hybrid ndio imetumika kwenye hybrids za Accord, CR-V, ZR-V, Civic, Prelude etc, kwahiyo ni engine ambayo imefanyiwa manoresho mengi) na transmission CVT ya Honda ni reliable ukifananisha na wengine.
 
Uchambuzi umetulia sanaa...
Ukiwa na familia kubwa inafaa zaidi uchukue 2.5L kuanzia noah,alphad na vellfire
Kuna alphad za 1.8 ( nyuma zinakuwa na nembo ya G) hizi gari zinachoka mapema Sana engine kwasababu zinabeba mzigo usiweza kudumu, Kwa upande wa nissan ELGRAND ni more comfortable, performance kuliko noah
 
Uchambuzi umetulia sanaa...
Ukiwa na familia kubwa inafaa zaidi uchukue 2.5L kuanzia noah,alphad na vellfire
Kuna alphad za 1.8 ( nyuma zinakuwa na nembo ya G) hizi gari zinachoka mapema Sana engine kwasababu zinabeba mzigo usiweza kudumu, Kwa upande wa nissan ELGRAND ni more comfortable, performance kuliko noah
Nikionaga Nissan then CVT mwili unasisimka
 
Nissan kwenye CVT wameshindwa Kwa kila njia.
Kampuni ya nissan wanahitaji miaka 100 kwenye technology ya CVT
Gari nyingi hapa Tz zitaishia kubeba lawama tu kwasababu mafundi wetu wapo nyuma sana kiteknolojia, barabara mbovu,vumbi, spea na oili feki.

Gari pekee za uhakika ni Toyota, gari nyepesi zaidi kutengeneza, zinazohimili mikiki kiasi hadi zinatumika vitani, 😀

waka wa 5 huu nina Toyota gereji naenda kwajili ya service tu, tatizo likinipata hata bush nina uhakika wa mafundi, sina stress kabisa kuhusu gari.
 
Gari nyingi hapa Tz zitaishia kubeba lawama tu kwasababu mafundi wetu wapo nyuma sana kiteknolojia, barabara mbovu,vumbi, spea na oili feki.

Gari pekee za uhakika ni Toyota, gari nyepesi zaidi kutengeneza, zinazohimili mikiki kiasi hadi zinatumika vitani, 😀

waka wa 5 huu nina Toyota gereji naenda kwajili ya service tu, tatizo likinipata hata bush nina uhakika wa mafundi, sina stress kabisa kuhusu gari.
Huko sahihi 100%.
 
Back
Top Bottom