sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,682
- 1,110
Vita kubwa ambayo itagharimu maisha ya wananchi ni migogoro ya ardhi iliyoshika kasi kubwa kwa sasa hapa nchini mwetu.Utendaji mbovu na tamu inayosababishwa na njaa za watendaji waliopewa dhamana hiyo,inapelekea taifa letu kuingia kwenye mgogoro mkubwa.Limekuwa sasa ni jambo la kawaida kwa watendaji wa serikali kupitia wizara hiyo kuwagawia wananchi viwanja bila kufuata utaratibu.Hali hiyo iliwahi kumtokea hata mkuu wa nchi kugaiwa kiwanja ambacho tayari alikwisha pewa mtu.Kama si hekima ya mheshimiwa rais,tayari ulikuwa mgogoro uliopandikizwa na wachumia tumbo wachache ambao ungechafua heshima ya rais.Sheria zipo wazi kabisa,tatizo nini linalosababisha kiwanja kugawanywa kwa watu zaidi ya watatu.Watendaji hao tunawajua,serikali nayo inawajua lakini hakuna sheria zinazochukuliwa dhidi yao.
Hali ni mbaya kwa nchi yenye kufuata utawala bora,ikiwa hali hii itaachiwa kama ilivyo sasa bila kuwawajibisha watendaji hawa.Yanayo jiri huko Mbarari ni matokeo ya wasomi wetu tuliowaamini lakini wakashindwa kujua kuwa cheo ni dhamana.Waatalamu hawa waliosomeshwa kwa kodi za Watanzania leo hii wamekuwa wachonganishi kati ya serikali na wananchi wake,kwa kugawa maeneo yaliyokuwa yana milikiwa na wananchi.Migogoro mingi tumeiona huko Babati kati ya mwekezaji na wazawa.Serikali imenyamaza kimya kwa kujua kuwa watendaji wake ndiyo waliotufikisha hapa tulipo.Machafuko haya yakizidi kushika kasi itakuwa zaidi ya Zimbabwe.
Tunabinafsisha ardhi yetu bila kunufaika na chochote,ardhi ipo chini ya wageni,nchi inakabiliwa na njaa kubwa.Hatuna miundo mbinu ya kuinua kilimo chetu ili kuwawezesha wananchi wasitegemee mvua na kuepukana na janga la njaa linalotukumba kila mwaka.Maandalizi haya ya zimamoto kwa serikali yetu kukabiliana na baa hili haina tija kwa wananchi wake,kiasi cha kauli mbiu ya kilimo kwanza kuwekwa kwenye makaratasi bila kufanyiwa kazi.Ukitazama hata vipau mbele katika bajeti yetu iliyopita,kilimo hakikupewa kimbau mbele cha kwanza kama ambavyo tunaaminishwa na wanasiasa hawa.Hatupendi kulalamika kwa kila jambo ila tumechoshwa na mipango mibovu ya serikali kwa kuwalinda watendaji wake bila sababu za msingi.
Ardhi yetu leo hii imekuwa sababu ya kuwatanguliza wazawa mbele ya haki kabla ya muda uliopangwa na Mungu.Nasema hivyo nikimaanisha kuwa wawekezaji waliohodhi ardhi yetu wanatumia nguvu kubwa kuwauwa wazawa kwa kisingizio cha wazawa kuingilia maeneo yao.Wakati mwingine chombo chetu cha dola kinawasidia wawekezaji hawa kufupisha maisha ya wazawa kwa kuwapiga risasi za moto kama yaliyokwishatokea huko Nyamongo.Serikali mpaka leo imekuwa ikishirikiana na wageni hawa kiasi cha kushindwa kutolea maamuzi.Mbaya zaidi zinaundwa tume kwa kutumia kodi za walalahoi matokeo yake ripoti zake zinaliwa panya kwenye makabrasha.
Serikali isipokuwa makini kwa hali inajionyesha sasa ni hatari kwa mustakabali wa amani yetu.Wananchi wamechoshwa kugombanishwa kwa kupambanishwa viwanja.Ipo siku watakuja lipa deni la usaliti.Wananchi wamechoshwa kinachofuata ni kujichukulia sheria mkononi,kwani wamekosa mtu wa kuwatetea ilichobaki watajitetea wenyewe kwa njia watakazoona zinafaa.Ardhi ni rasilimali ndiyo maana hata mwalimu alitoa kipau mbele cha pili kitakacho muwezesha mtu apige hatua za kimaendeleo.Rasilimali watu ni kubwa lakini maendeleo hayo yatapatikana vipi ikiwa ardhi inaporwa na wageni kwa kisingizio cha uwekazaji.Zama za mwalimu tuliamini kilimo ni uti wa mgongo wa maendeleo ya nchi yetu.Zilionekana juhudi binafsi kuhakikisha ardhi inatumika vizuri kwa manufaa ya wote,tena mbaya zaidi hata zana tulizotumia zilikuwa duni lakini kilimo kilikuwa na tija,kilichomuwezesha mlalahoi kukidhi matakwa yake na kumuwezesha kulipa kodi ya maendeleo.
Vyama vya ushirika vilikuwa nguzo kuu na muhimu kilichotumika kama soko na chombo cha kumkomboa mkulima huyo wa jembe la mkono.Hata kama serikali ikitumia nguvu kubwa kuvisimamisha viwe na nguvu kama zamani bado tatizo lipo kwa wanachama wake ambao ndiyo wakulima.Tunaitaka serikali iliangalie suala hili la ardhi kwa mapana na marefu vinginevyo vita kubwa nchi mwetu ni vita ya ardhi.
Mnyonge mnyongeni kilicho chake abaki nacho,na ndicho atakachojitetea nacho.